Mambo mengi yatachangia katika maamuzi yangu. Mwanaume wa kutembea mpaka anazaa na changudoa na bar maid ina maana huyo ni cassanova na mlevi wa kupindukia - mwanaume wa namna hiyo mke hua anajua tabia ya mumewe. Ndo maana utasikia baadhi ya wanawake wanasema kabisa hadharani kua mm namjua mume wangu ni malaya!
Kama hio tabia ya umalaya tayari ni dhahiri na bado unakaa nae - cha ajabu nini kusikia kazaa na hao wanawake (tena ukute hata kapakaziwa) hakuna haja ya kumuuliza watoto kama bado una nia ya kuishi nae maana utampa sababu ya kuwaleta hapo uwalee. kwa upande wangu tatizo ambalo halina ufumbuzi sioni sababu ya kulifungua iwapo nimeamua kumuacha naondoka zangu, za nini headaches....