nadhani sio busara kumteua tena kwa kuwa tayari jamii imeyajua mapungufu yake na tayari imani kwa wanajamii imepungua hivyo kila akiwa katika kazi yake jamii inautazama udhaifu wake. Labda kama rais huyo anapenda ufisadi, mfano Kikwete akimchgua tena Lowasa atakuwa yeye amepunguza imani kwa wananchi kwa kuwa tayari alitangazia umma kujiuzulu kutokana na tuhuma za Richmond.
MH Mungai mbunge wa Mufindi enzi zile za 1978 MWalimu Nyerere akiwa Rais ( Wengi hapa Baba zenu walikuwa bado wanawagwaya mama zenu wakiwa na mipango ya kuwachumbia) aliwajibishwa na kuamuliwa kujihuzuru Uwaziri wa Kilimo kutokana na upotevu wa sukari ya mabilioni SUDECO. Baada ya Nyerere kufa Mzee huyu aliteuliwa na Swahiba wake Nkapa kuwa waziri tena. Ndipo alipo amua kutimbanga Elimu ya Secondari Tanzania kwa mara nyingine.
Uchunguzi wangu wa juujuu hapa US unanionyesha kwamba yeye naye digrii zake ni zina tia shaka, nimwasisisi wa digrii za ovyoovyo. Alikuja Marekani 1978 akiwa High School Graduate kwa Muda wa miaka2 aliweza Kufanya First digree na Masters huko Colorado Univ Na Havard Univ. 1978-1980( Nisahihishwe kama nimekosea)
Naamini kabisa Kikwete atawateua tena Mafisadi waendelee kutwanga na kupepeta katika serikali yake.
Naona wengi mmekwisha sahau kwamba MH Kikwete naye yuko kwenye Timu yetu ya Mafisadi .First 11 Hillsider Boys:first:
Fisadi namba moja ni Rais wa nchi TUNA SHANGA nini Chenge na Lowassa wakiwa Mawaziri??
Tumekwisha Fanywa tayari, akiingia Chenge na Lowassa ndani ya baraza la mawaziri tutakuwa tunfanywa kwa mara ya pili na ya tatu.:becky::becky::becky:
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.