Swali kuhusu walioghushi Vyeti

Swali kuhusu walioghushi Vyeti

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,168
Reaction score
48,446
Kwa mfano mtu alighushi cheti akawa Askari Polisi, akamkamata mtu, huyo mtu akafunguliwa Mashitaka Mahakamani, Mahakamani akahukumiwa na Hakimu aliyeghushi cheti chake pia, akapelekwa Gerezani ambako nako kwa wakati fulani alilindwa na Askari Magereza aliyeghushi cheti. Je mtu huyu anaweza kushitaki kwa kukamatwa isivyo halali, kuhukumiwa na mtu asiye na sifa na kushikiliwa kifungoni na Askari Magereza aliyeghushi cheti?

Mzazi anampeleka mtoto wake shule ya Msingi, sekondari na mpaka chuo kikuu. Huko kote kwa wakati fulani alifundishwa na waalimu walioghushi vyeti. Huyu mtu usomi wake ni halali au ni haramu. Kitendo cha kufundishwa na waalimu walioghushi vyeti kinachukuliwa kama ni kosa?

Mama mjamzito kafika Hospitali, kapokelewa na Muuguzi aliyepata kazi hiyo kwa kughushi cheti, akaandikiwa dawa na Daktari aliyeghushi cheti na hatimaye akasaidiwa kujifungua na Mkunga ambaye naye alighushi cheti chake hata akaupata huo ukunga. Mama huyo ana haki ya kufungua mashitaka dhidi ya serikali kwa kuhatarisha maisha yake kwa kuajiri watu walioghushi vyeti?
 
Acha niendlee kuwaza!
 
Hiyo ni Tanzania pekee ndio hivi vitu vinaweza kutokea.
 
hakuna sheria inayobana hayo mambo ila kwa mawakili ikijulikana na mahakama kuwa wakili aliekua anasimamia kesi X ameghushi vyeti kesi yote inaondolea mahakamani na yale yote aliyoyaongea yanafutwa haijalishi kesi ilikua hatua gani
 
Hata kuwa wadadisi tunakatazwa?
Utaitwa mchochezi.....ila kwa mtazamo wangu ni kuwa Mr. Uchwara anavisasi na watu hasa ktk pita pita yake huko shuleni, labda alikuwa harassed at some point na mtu mwenye cheti feki. Labda ...labda alitoswa na Demu mwenye cheti feki....anamuwinda amuoneshe yeye ni TIC ( Top in Country)

moto2012
 
Huyo mama mjamzito nae atakuwa feki,amejifunguaje sasa kama mkunga feki!
 
Uhusiano hauna madhara!mf.askari akimkamata mtu kinachofuata sheria kufuata mkondo wake,kama hakimu yuko naye hiyo mara nyingi sheria inaupenyo wa hukumu yake ku-be revied kwa hiyo serikali iendelee na program yake ya kushughulika na hao watu feki.
 
Huyo mama mjamzito nae atakuwa feki,amejifunguaje sasa kama mkunga feki!
Kina mama huko vijijini kila siku wanajifungulia majumbani na hakuna shida. Kujifunga ni tendo ya kibaiolojia na wala halijali anayekusadia kujifungua ni Mkunga ama si mkunga au ni mkunga feki!!
 
Nchi hii hata Rais alisaidiwa kughushi matokeo na mwendelezo wa mfumo huo huo wa walioghushi vyeti..!!
Bongo neno kughushi ni sawa na ujasiri au ujanja unaomfanya mhusika atoke kimaisha...
Wengi wetu humu kwa nyakati tofauti tulishashawishiwa kuuza au kugawa aidha vyeti au majina yetu... Na ukikataa kata kata unaonakana kama mchoyo mwenye roho mbaya..!!
 
Kwa mfano mtu alighushi cheti akawa Askari Polisi, akamkamata mtu, huyo mtu akafunguliwa Mashitaka Mahakamani, Mahakamani akahukumiwa na Hakimu aliyeghushi cheti chake pia, akapelekwa Gerezani ambako nako kwa wakati fulani alilindwa na Askari Magereza aliyeghushi cheti. Je mtu huyu anaweza kushitaki kwa kukamatwa isivyo halali, kuhukumiwa na mtu asiye na sifa na kushikiliwa kifungoni na Askari Magereza aliyeghushi cheti?

Mzazi anampeleka mtoto wake shule ya Msingi, sekondari na mpaka chuo kikuu. Huko kote kwa wakati fulani alifundishwa na waalimu walioghushi vyeti. Huyu mtu usomi wake ni halali au ni haramu. Kitendo cha kufundishwa na waalimu walioghushi vyeti kinachukuliwa kama ni kosa?

Mama mjamzito kafika Hospitali, kapokelewa na Muuguzi aliyepata kazi hiyo kwa kughushi cheti, akaandikiwa dawa na Daktari aliyeghushi cheti na hatimaye akasaidiwa kujifungua na Mkunga ambaye naye alighushi cheti chake hata akaupata huo ukunga. Mama huyo ana haki ya kufungua mashitaka dhidi ya serikali kwa kuhatarisha maisha yake kwa kuajiri watu walioghushi vyeti?
Leo umekuja na vitu vigumu sana lakinj kwakuwa mimi ndie bongo experience ngoja nijipange nije na majibu sahihi
 
Hili suala linahusiana na kwamba kuna watu hapa wataadhibiwa, lazima tujue nafasi ya waliohudumiwa na waghushi vyeti ikoje!
 
Kwa mfano mtu alighushi cheti akawa Askari Polisi, akamkamata mtu, huyo mtu akafunguliwa Mashitaka Mahakamani, Mahakamani akahukumiwa na Hakimu aliyeghushi cheti chake pia, akapelekwa Gerezani ambako nako kwa wakati fulani alilindwa na Askari Magereza aliyeghushi cheti. Je mtu huyu anaweza kushitaki kwa kukamatwa isivyo halali, kuhukumiwa na mtu asiye na sifa na kushikiliwa kifungoni na Askari Magereza aliyeghushi cheti?

Mzazi anampeleka mtoto wake shule ya Msingi, sekondari na mpaka chuo kikuu. Huko kote kwa wakati fulani alifundishwa na waalimu walioghushi vyeti. Huyu mtu usomi wake ni halali au ni haramu. Kitendo cha kufundishwa na waalimu walioghushi vyeti kinachukuliwa kama ni kosa?

Mama mjamzito kafika Hospitali, kapokelewa na Muuguzi aliyepata kazi hiyo kwa kughushi cheti, akaandikiwa dawa na Daktari aliyeghushi cheti na hatimaye akasaidiwa kujifungua na Mkunga ambaye naye alighushi cheti chake hata akaupata huo ukunga. Mama huyo ana haki ya kufungua mashitaka dhidi ya serikali kwa kuhatarisha maisha yake kwa kuajiri watu walioghushi vyeti?
Hii n hadisi au maana ni ya kufikirika sana kuna sehemu nyingine ukigushi lazima utagundulika kaa udaktari na fani nyingine za kutumia akili

Ila ktk fani za kutumia uzoefu tu na nguvu hzo kidogo uwezi kugundulika mapema

Lakin pia n ngumu kukuta kila sehemu unayopita kuna vyeti feki cz ukifanya hesabu ya kawaida tu waliokamatwa na vyeti feki na wenye vyeti original utaona vyeti feki ata 10% ya original havifiki
 
Guru1902 waliokamatwa haimaanishi ni hao tu ndiyo wenye vyeti feki. Unakumbuka lile sakata la Kigwangala? Halafu kama unadhani uchache wa jambo ndiyo ukubwa wa madhara yake utakosea sana. Kwani ni asilimia ngapi ya watanzania wanauza madawa ya Kulevya? Hata asilimia moja hawafiki, lakini madhara yake si unayaona?

Halafu kuamini kwamba kwenye fani ya Udaktari huwezi kughushi,pia unakosea. waulize watu wa Muhimbili watakwambia kama haiwezekani!!
 
Back
Top Bottom