Swali kuhusu UKAWA

Swali kuhusu UKAWA

vidodi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2014
Posts
363
Reaction score
130
Swali naomba nisaidiewe jibu lake kutokana na Katiba ya nchi, Rais akiwa anatoka Bara makamu anakuwa anatoka Zenji na pia ni lazima wawe chama kimoja. Je! Kama mgombea urais akitoka CHADEMA, makamu wake atatoka chama gani? Kama ni wa CUF ina maana atahamia CHADEMA kama Katiba inavyosema lazima wagombea wawe chama kimoja au wote watatoka CHADEMA?

Makamu na rais? Sasa vyama vingine vitakuwa na kazi gani? Kama rais Slaa, makamu Seif Hamad, Je waziri mkuu atakuwa nani? Maana kati ya Lipumba au Mbowe nna uhakika mmoja lazima atataka kuwa hyo nafasi, Je mmoja wao atakubali kuiachia awe waziri wa kawaida? Ubunge wanasema wamekubaliana, Sawa, Je! hapa dar nani atakubali kumwachia mwenzake nafasi? Kama nafasi nyingi atapewa chadema, vyama vingine vitakubali?

Asanteni
 
please wait.......
time will tell.....
 
Kuwa Mwenyekiti wa Chama ni lazima kugombea Urais?

Kugombea Urais ni hobby?

Kwa nini Mbatia na Mbowe wasigombee Urais
 
  • Changamoto zinazosababisha kutoafikiana

    Miongoni mwa changamoto kubwa ambazo UKAWA inakabiliana nazo ni kuwa chama kinachotoa mgombea wa uraisi ndicho chama kitachotoa mgombea mwenza kulingana katiba na sheria za nchi. Hii maana yake ni kwamba mojawapo ya vyama hivyo kikubali mmoja wa wanachama wake achukue kadi ya uanachama ya chama kingine, ili awe na sifa ya kuwania. Hadi sasa hakuna chama kilichoonesha moja kwa moja dhamira ya kukubali chama chake kikose nafasi hiyo.

    Changamoto nyingine kwa UKAWA ni sheria za uchaguzi za Tanzania zinazotaka vyama vipate ruzuku kubwa kutokana na wingi wa kura ambazo mgombea wake wa ngazi ya uraisi na wabunge wamepata. Hii maana yake ni kwamba kama CDM kitatoa mgombea wa uraisi na si CUF, NCCR au NLD, wao watapata ruzuku kubwa zaidi baada ya uchaguzi na hivyo watakua na nguvu zaidi kuliko vyama vingine. NCCR safari hii watataka kusimamisha mgombea wa urais ili na wao wapate ruzuku na hawatakua tayari kutosimamisha mgombea uraisi kama miaka ya nyuma.

    SULUHISHO
    Nionavyo mimi kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu....ni wakati sasa wa UKAWA kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kuepuka migongano hii ambayo ni ya kimaslahi zaidi kwa vyama vyao na kuacha kumlenga mwananchi wa kawaida ambaye ni masikini​

Du mkuu umenena haya ngoja ifike right time tuone lkn maumivu ya kichwa huanza polepole
 
Cdm imejificha hapo ukawa bado wanasikillizia mziki wa act wekiona wanauweza watajitoa wajiona hawauwezi watakomaa huko huko . ndio maana wamezunguka nchi sasa hivi watakuwa wanafanya tasimini wamepata wanachama wangapi, na nguvu yao ikoje bila zitto.
 
UKAWA ni maslahi ya wananchin na si vyama. uliowataja si wao pekee wenye kupewa nafasi hizo ndani ya UKAWA. kumbuka hawakuungana kwa sababu ya madaraka bali kuwakomboa wanyonge wa Tanzania
 
Muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi Ukawa tumejipanga kuliko mnavyofikiria.
 
mcubic

Mtajitahidi sana kuleta propaganda zenu lkn hamtaweza kujua siri iliyoko kwenye ukawa.Ukawa wakipewa ridhaa watafuta katiba iliyopo na kuunda ya Warioba waliyoikataa CCM.
 
Last edited by a moderator:
Mtajitahidi sana kuleta propaganda zenu lkn hamtaweza kujua siri iliyoko kwenye ukawa.Ukawa wakipewa ridhaa watafuta katiba iliyopo na kuunda ya Warioba waliyoikataa ccm.

Tatizo sio siri tatizo ni kama ilivyosemwa hapo juu Je wapo tayari wakati inaonyesha haitawezekana? We njoo na facts usiseme ni propaganda hapa tunaangalia kama ukawa watawezana au vp
 
Mtoa madanenda kanye mana mawazo yako yakikoroni na mashaka kama ulikuwa unauliza maswali kama haya class ulipigwa sana
 
mcubic

Kwa sasa kuunda chama kimoja haiwezekani, time is not our friend

Mfumo wa sasa sio our friend, kwa itapigwa dana dana

Solution wanaweza kukubaliana kuwa baada ya uchaguzi na ushindi ukipatikana ndo Chama kilichotoa Raisi ndo kiwe chama kipya, wengine wavunje vyama vyama wajiunge na chama cha Raisi. Only after election winning.

Kazi ya Kwanza ya kufanya ni kuparalyse nguvu za sisiem mashinani
 
Last edited by a moderator:
Umeuliza swali na ukajijibu mwenyewe kutoka kwenywe kichwa chako bika kusubiri UKAWA wakupe majibu sahihi.mbaya zaidi unaanza kubisha hata kabla ya majibu kutolewa.what do you really want?
 
Cdm imejificha hapo ukawa bado wanasikillizia mziki wa act wekiona wanauweza watajitoa wajiona hawauwezi watakomaa huko huko . ndio maana wamezunguka nchi sasa hivi watakuwa wanafanya tasimini wamepata wanachama wangapi, na nguvu yao ikoje bila zitto.

Pole sana ndugu
Zitto ni kama mavi ya zamani kwa CDM
Halafu CDM haijaanza leo kuzunguka
Kama hulijui hilo pole kwa mara ya pili
 
Mtajitahidi sana kuleta propaganda zenu lkn hamtaweza kujua siri iliyoko kwenye ukawa.Ukawa wakipewa ridhaa watafuta katiba iliyopo na kuunda ya Warioba waliyoikataa ccm.

Soma tena post yangu......usikurupuke
 
Kiwa ndo nani? Ukawa wapo kwa ajili ya masilahi ya wananchi,yule anae angalia masilahi yake,ajuwe tu kuwa hayawezi kupatikana kamweeee,umoja ni nguvu, nyie ma sisiem msituchanganye ss!!!
 
Swali naomba nisaidiewe jibu lake kutokana na Katiba ya nchi, Rais akiwa anatoka Bara makamu anakuwa anatoka Zenji na pia ni lazima wawe chama kimoja. Je! Kama mgombea urais akitoka CHADEMA, makamu wake atatoka chama gani? Kama ni wa CUF ina maana atahamia CHADEMA kama Katiba inavyosema lazima wagombea wawe chama kimoja au wote watatoka CHADEMA?

Makamu na rais? Sasa vyama vingine vitakuwa na kazi gani? Kama rais Slaa, makamu Seif Hamad, Je waziri mkuu atakuwa nani? Maana kati ya Lipumba au Mbowe nna uhakika mmoja lazima atataka kuwa hyo nafasi, Je mmoja wao atakubali kuiachia awe waziri wa kawaida? Ubunge wanasema wamekubaliana, Sawa, Je! hapa dar nani atakubali kumwachia mwenzake nafasi? Kama nafasi nyingi atapewa chadema, vyama vingine vitakubali?

Asanteni

chadema na ukawa yetu tunaakili na tunajua mengi kuliko wewe,tulia utaona tunavyoongoza inchi.
 
Umeuliza swali na ukajijibu mwenyewe kutoka kwenywe kichwa chako bika kusubiri UKAWA wakupe majibu sahihi.mbaya zaidi unaanza kubisha hata kabla ya majibu kutolewa.what do you really want?

We kweli bogaz numejijibuje au hujasoma post vizuri unakurupuka tu
 
Back
Top Bottom