Swali kuhusu mzunguko wa hedhi na ujauzito

Swali kuhusu mzunguko wa hedhi na ujauzito

dojonase

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
1,736
Reaction score
2,428
Mwanamke anayeingia hedhi mara 2 kwa mwezi (mzunguko wake kuvurugika) je anaweza kupata mimba siku yoyote mwezi unaofuata au unaanza kuesabu vipisiku zake?

Mfano January alingia hedhi tarehe 5 baadaye akaingia mwezi huo huo tarehe 24, tunahesabu vipi siku zake au mimba inaingia bila hesabu za siku?
 
Hedhi mara mbili kwa mwezi mpaka hapo tu hiyo ni hormonal imbalance kushika mimba sio jambo rahisi mpaka apate matibabu
 
Habari,
Kabla ya yote ni vyema kutanabaisha kama je huu ndio mzunguko wa hedhi kwa siku zote au imetokea kwa mwezi huo mmoja tu.

Pia, si shida kupata hedhi mara mbili kwa mwezi. Bali cha msingi ni urefu kati ya mzunguko mmoja mpaka mwingine kama itakavyoelezwa hapo chini.

1: Kama ndio mzunguko wake siku zote, basi yuko nje ya utaratibu halisi wa hedhi.

Mzunguko wa kawaida ni siku 21-35. Hii ni kutoka ile siku ya kwanza ya mzunguko mmoja mpaka mwigine. Kwa mfano ulivyoonyesha hapo ni siku kati ya tarehe 5 na 24 ambayo ni jumla ya siku 19.
Kama ni mzunguko wake wa siku zote si kawaida ni vizuri kupata huduma ya afya kwa hali husika.

2: Kama siyo mzunguko wake wa siku zote, kuna uwezekano kuna kitu hapa kati kilimtatiza na kuvuruga mzunguko wake. Hivyo hutaweza kujua ni lini anaweza kubeba ujauzito kwani hautaweza kujua urefu halisi wa mzunguko. Ili kujua hilo basi utahhutaji miezi mitatu ili uhesabu na kupata mwenendo wake.

3: Kuhusu ujauzito, namba mbili hapo juu ataweza kupata ujauzito ndani ya mzunguko unaofuata ila hutaweza kutambua ni lini kulingana na maelezo hapo juu.

Kwa namba moja uwezekano ni mdogo/nasita kusema neno HAUPO ingawa yuko nje ya utaratibu, ila ya Mungu ni mengi. Ukuu wake waweza kujitokeza hapo. Ingawa ki-sayansi tunasema si kawaida.
 
Ni kawaida, kuna watu walio na mzunguko mfupi wa hedhi. Mengi nimeyasahau ila ukienda hosp utashauriwa vzr. Wala msiwe na hofu.
 
Mwanamke anayeingia hedhi mara 2 kwa mwezi (mzunguko wake kuvurugika) je anaweza kupata mimba siku yoyote mwezi unaofuata au unaanza kuesabu vipisiku zake?

Mfano January alingia hedhi tarehe 5 baadaye akaingia mwezi huo huo tarehe 24, tunahesabu vipi siku zake au mimba inaingia bila hesabu za siku?
Kuna baadhi ya wanawake wanapata hedhi mara mbili kwa mwezi ( double menstrual) hili jambo muhimu kuzingatia so ili aweze kupata mimba inatakiwa ile siku ya kwanza kupata hedhi ndio ufanye naye tendo la ndoa ili aweze kushika mimba nitalielezea kwa upana nikipata time.
 
Back
Top Bottom