Swali: kipi ungebadili kwa mpenzi wako?

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,820


Je ni kitu (vitu) gani ungependa ki(vi)badilike kwa mpenzi wako?

Wakati nipo hospitali namwuguza mpenzi wangu, wakaja watu kuona wagonjwa wengine ambao tulikuwa kwenye wodi moja

katika ongea ongea na salimia za hapa na pale, wakaanza kupiga stori baada ya mgonjwa kuwauliza kuhusu wapenzi wao

Kama kawaida ugonjwa wa Mapenzi ni wa Dunia nzima, kila mmoja analalamika kivyake vyake wengine wanatukana wengine wanalaani wengine wanakemea wengine kimya wanaangaliana, wengine wenye imani zao chanya wanawaongelesha wale wenye imani hasi kwa kujipa moyo wasikate tamaa, money penny na mgonjwa wangu tuna-zoom tu maungumzo, kiru!

Basi mgonjwa akawauliza, jamani naona mnalalamika sana asee, naombeni niwaulize kitu kimoja juu ya wapenzi wenu,

Je mkiambiwa mbadilishe chochote kuhusu wapenzi wenu, mtabadilisha nini?

Mgeni wa 1 (Msichana):
Mimi nataka Mpenzi wangu aache kuangalia wanawake wengine wanaopita njiani tukiwa wawili, tukiwa tunaongozana barabarani au kwenye gari, akipita dada/demu mzuri tu yeye hugeuka na kumwangalia,

Sikumoja kidogo amgonge mtu barabarani

Mgeni wa 2 (Dada Kaolewa):
Mimi nataka Mume wangu aache kuwapa ofa marafiki zake, kila weekend anatoka na marafiki zake, akitoka anaenda kumalizia pesa baa kwa kuzungusha vinjwaji kwa marafiki zake, kwakweli inanikera sana maendeleo mengi yamesimama kwa ajili ya kuwahudumia hao marafiki zake, huwa najiuliza ameoa au ameolewa hao marafiki zake hata siwapendi na kwangu nishawapiga marufuku lakini bado utadhani amechimbiwa dawa na hao marafiki zake


hio ndio kero yangu kubwa ambayo napenda ibadilike kwa Mpenzi wangu...

Mgeni wa 3 (Msichana):
Mimi nataka mpenzi wangu aache kuni-control, yani hata hajanioa lakini ana wivu balaa na anani-control balaa, hapa nilipo nawapa dk 10 mbele atapiga simu upo wapi, ah mimi sipendi,

Ijapokuwa service nzuri lakini sina uhuru nabanwa banwa saaanaa hapa nawaza akinioa sijui itakuwaje si atakaa ndani ataniachisha kazi kabisa,
maana nikitoka tu kazini yupo mlangoni

ananirudisha nyumbani, nikitoka nyumbani kwenda kazini yupo mlangoni, lunch time anapiga simu lisaa 1 anaongea tu na mimi kha!
nimechoka!
Alipomaliza tu kuongea akapigiwa simu na mpenzi wake, akawaambia wenzake haya sikilizeni akaweka loud speaker,
Mpenzi wake: Haloo, baby upo wapi nipo hapa kwako naambiwa haupo

wenzake: wakacheeekaaa! uuuwi, ikabidi huyu dada atoe loud speaker anamwambia mpenzi wake nipo Hospital Staff mwenzetu kazini alipata ajali ndio tumekuja kumwona,

Ni sheeedaaaah!

Mgeni wa 4 (Kijana wa Kiume):
Kusema kweli mimi nampenda sana mpenzi wangu, ila huu ni mwaka wa 2 yule msichana ni mchaaaafuuu na mbeeeaaaa,


tulipoaza mahusiano alikuwa vizuri sana kila engo, ila kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda naona anabadilika, kwasababu nampenda nikaamua kumpeleka masemina ya akina Chris Mauki, akina Aunty Sadaka na wengine wengi, akisema kitchen pati za shogazake nalipa ili tu ajifunza lakini naona huyu akienda huko anaishia kucheka na kupiga picha hali ipo pale pale... nikaongea nae akaacha kwa wiki 2 akarudi pale pale

nikamnunulia simu basi apunguze umbea sasa huko kwenye mitandao ilikuwa ni sheedah, anaongea ongea na kutukanana na watu nikaamua kukaa pembeni kwanza mpaka ajirekebishe huku natafuta demu mwengine

Mgeni wa 5 (Mume wa mtu):
Mimi nampenda sana mke wangu ila ana mashauzi hatari, kujiongeza ongeza kwa marafiki zake kuwa tuna mambo makubwa kumbe hatuna ndio kinanigharimu zaidi,


Isitoshe anadai vitu vikubwa nimpatie kuliko uwezo wangu na huku tunasomesha watoto,

Asione kitu kwenye mitandao ya kijamii anataka, leo Zari wa Mondi kabeba pochi ya mil 5 na yeye anataka,

Kesho sijui Wema kasuka weaving gani nae anataka, alafu ni Team Wema sasa, yani birthday ya Wema tunaimbiwa miezi 3 kabla, utasikia Wema ana Birthday yake nataka nimnunulie Gold chain au nimlipie Kodi ya nyumba mwaka mzima au nimpeleke Dubai kwa dadake

Ikifika wiki 1 kabla atakwambia nipe hela nimpeleke Wema au nimnunulie Wema hiki na kile

Yani huyu mwanamke natamanigi kumkata makofi na mangumi kabisa, Hapa nilipo ameshanifanya nimchukie Wema na Huyo mke wa Diamond Platnumz aitwaye Zari,

Kama nisingekuwa mkristo ningemuacha kabisa,
sijui yupoje?
sijui kapatwa na kichaa gani au kapagawa au ana mapepo hata simwelewi kabisa!

Mgeni wa 6 (Kijana wa Kiume):
Doh bora nyie, mimi mpenzi wangu ni Mjinga hakuna mfano, yani kwanza kamaliza form 4 na divishen 0. basi bora divishen 0 ya darasani utageuza shilingi useme maisha ni zaidiya divishen 0, lakini wapi, hana akili za darasani wala za maisha


wenzake wote wakacheka

Yani mpenzi wangu sijui anajifanya au ananisoma au simwelewi kabisa ,

Basi nilipokutanaga nae akaniambia yeye shule hawezi tena anataka afanye biashara, nikaweka mkono wangu mmoja nikamfungulia biashara,

weeee!
kila mwezi ni hasara, nikamvumilia miezi 6 lakini wapi biashara ikafa

nikiwa na washikaji zangu akija anaongeeeeea sana, hajui kama kuna mipaka, alafu vitu anavyochangia hajui anakuwa kama anabahatisha... anajishaua hapo anaongea kidhungu kidhungu chenyewe broken hakuna mfano wake, ni sinema tosha huyu demu

9-10 sasa nilimtambulisha kwa dada yangu mbona nilijuta, kumfahamu dadangu kila siku anawasiliana nae, kila mwezi yupo kwake mara 2

Nikimpa hela leo labda elfu 50 kesho imeisha, umefanya nini anakwambia saloon na vocha, kwa maisha haya magumu nimeona nikae pembeni... siwezi oa yule demu hata kwa bure.

Mgeni wa 7 (Msichana):
Akaongea kwa uchungu sana mpaka mgonjwa wangu akaguna eh pole!
Yani nyie mimi naona matatizo yenu madogo, nimekuwa kwenye mahusiano na huyu bwana mwaka 1 sasa, ndoa hataki najivumilishia, huwezi kusema mahusiano ni machanga lakini huu ni mwaka 1 sasa, nina haki ya kudai ndoa, ila huyu bwana kila tukiwa tunapeana raha, hanifikishi, nimefanya kila kitu wapi, tumeenda kwa dokta mwezi uliopita akajifanya amepigiwa simu ya ofisi, tukaacha na majibu, kesho yake nikaenda kufuatilia majibu naambiwa alishakuja kuchukua kumwuliza akakanaaa sijaendaaa, basi nikapotezea ila sasa wiki 2 zilizopita nimemfumania usiku wa manane ametoka nyumbani saa 8 usiku nikamfuata, akafika kwenye baa moja ipo kimara akanikutana na bwana mmoja maarufu sana hapa mjini, wakaanza kulana ndimi, moyo ukafanya paaaa, nikakaa kwanza chini huku nimejibanza, wakachukua chumba mimi nawaangalia tu, wakaingia ndani ya chumba, nikaenda nimekaza roho kufika mlangoni mwa kile chumba nikaanza kusikiliza, naskia tu watu wanalia na kupeana raha na misauti ya kila dizaini, nilizimia hapo hapo nikajikuta hospital na dada yangu akaja na yule bwana alikuwepo, nikamwambia kuanzia leo mimi na wewe basi, huwezi amini nina wiki 1 sasa nipo single... kwahiyo ukiniambia kitu cha kubadilisha kuhusu mpenzi wangu sina maana alikuwa rijali mchana usiku bwabwa/ shoga/ mchelemchele/ gay!


wenzake tobaaaa, lahaulaaa kila mtu anashangaa kivyake na kutukana kivyake

Mgeni wa 8 (Mwanaume):
Pole sana ndugu yangu usijali utapata bwana ambae ni rijali, mimi kusema kweli sipo mbali sana na huyu dada, mimi mpenzi wangu alikuwa mchawi!


Nilirudi toka kazini saa 5 hakujua nilikuja kuchukua document nyumbani niliisahau, nikakuta ameweka makorokocho yake hapo chumbani kitandani anajivundika na kusali macho kaweka juu kama anakata roho, kumwuliza mama unafanya nini akawa kama ameganda akaanza kujiliza, nikambwatukia, nachokumbuka ni kuchukua ile document na kuondoka sijawahi kurudi tena pale, kesho nataka niende na polisi nikachukue mizigo yangu na vitambulisho vingine vya muhimu nikazichome zile nguo moto, kwahiyo sina cha kubadilisha kwa mpenzi wangu

Mgeni wa 9 (Mwanaume):
Kusema ukweli Mpenzi wangu mimi anapenda sana kula, kha! yani ana kilo 200 lakini anakula balaa, hapo sijamuoa, hajazaaa nahisi nitatengeneza kitanda cha 10 kwa 10, kweli nampenda sana mpenzi wangu, tumeshaenda mpaka Gym ila akitoka tu Mazoezi anarudi kupiga chispi, kitimoto, pombe pale pale, alishasahuriwa kule mazoezini kama anataka kupungua ale vyakula hivi na vile lakini waaapi! hajapungua huu mwezi wa 2 sasa mimi nimepungua kg 5 yeye ni kama ananisindikiza tu huko mazoezini... nachopenda mpenzi wangu abadilike ni huo unene, maana tukija kwenye mechi anahema kama anakufa namhurumia sana hana pumzi nisije nikamuua bure mtoto wa watu



Mgeni wa 10 (Mwanaume):
Mimi mpenzi wangu ni Mnenguaji kwenye hizi show za kukatika bendi ya Twanga pepeta, yani hakuna kazi ngumu kama ile, kwanza hamlipi kivile, nimeshaongea nae haachi, nikampeleka kwa washauri hataki sijui kachomewa dawa maendeleo na ile bendi hata siyaoni kwake, hela anayolipwa siioni anaishia kubadilisha nguo na nywele kichwani na kununua viatu na vocha
kiukweli nampenda sana sana sana na sasa huu mwezi wa 6 kwenye mahusiano lakini naona sasa nitaondoka kwenye maisha yake


alafu sasa kiiila akienda kwenye show anarudi anaumwa kitovu, nitauguza kitovu weee akishapona tuuu anarudi kuneng'ua!

mechi zenyewe napewa kwa mwezi mara 1 maana sasa ni kuuguza tu kitovu, kha! hizi karaha za huyu mwanamke zimenishinda wajameni, kama atabadilika atoke kwenye hio ajira ya kunengua mauno nitashukuru ndio ombi langu kuu ningependa abadilike

Mgeni wa 11 (Mwanamke):
Yani nyie mnanichekesha sana, ila wewe uliepata bwana shoga bora yako kuliko mimi, mimi nilipata mpenzi huu mwezi wa 3 sasa, tumeanza vizuri ananipa kila kitu nachotaka wajameni mnisikie, laiki juzi hapa ndio tumejuaje, kujuana huko mbona kulinigharimu, katika malavi davi ya hapa na pale, yule bwana kumbe HAJATAHIRIWA!


wenzake wote wakacheka, maana doh hawakutegemea!

akaendelea, jamani hamuwezi amini na wala usikutane na machine isiotahiriwa! kha! ni kama kula ndizi na gamba, hata wa kuvaa condom ana afadhali mara 100 kuliko asiyetahiriwa

wala msitake kujua yaliyotokea lakini nachotaka kwa mpenzi wangu ni akatahiriwe!

Ahahahahahahhaha, uuuuwi Money Penny nilicheka mpaka mgonjwa wangu alinikasirikia!

Mungu wangu Tanzania yetu hii mbona ina vituko!?

Je ni kitu gani mpenzi msomaji ungependa kubadilisha kwa mpenzi wako mpendwa msomaji wa Jamii forum?!

 
Mie nataka awe kama no.3 na tukiwa mbali mbali video calls , selfies sometimes ....... I need to feel his presence hata asipokuwepo !!! Mtu kama huyu nasema wanaume wengine wote nawaona sketiiiiiii
 
uandishi wako sio mzuri sana, pengine mtu anaweza asivutiwe kusoma andiko lote.... punguza ukubwa ikiwezekana toa bold...
 
Asiwe ananuna nuna hovyo, sio kitu kidogo tu kanuna, hadi anasusa kula vilivyomo.
Mwanaume kununa haipendezi....Kama litoto vile.
 
Asiwe ananuna nuna hovyo, sio kitu kidogo tu kanuna, hadi anasusa kula vilivyomo.
Mwanaume kununa haipendezi....Kama litoto vile.
una maana anavimba

mwanaume kama huyo dawa yake moja tu
mtafutie opposite wake uone kama hajabadilika
pole
 
Back
Top Bottom