Swali: Je, urais una sura?

Konakali

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
1,533
265
Habari za leo tena wandugu....!

Ilikuwa mida ya saa nne za asubuhi hivi, niko kwenye foleni kusubiri kupata dawa kwa ajili ya mtoto wa kaka yangu pale wodi namba saba katika hospitali ya Mount Meru. Nakumbuka tulikuwa zaidi ya 20; wake kwa waume, kwenye foleni ile, na ndio kampeni za uchaguzi mkuu uliopita zilikuwa zimeiva haswa ilishakuwa wimbo katika kila kijiwe, kila chombo cha usafiri na kila wakati kuhusu wagombea wa urais kati ya CCM na UKAWA.

Ghafla na kama kawaida stori zikaanza, na ubishi ukaongezeka kuwa nani angetufaa zaidi katika nafasi ya urais. Ndipo mdada mmoja, mwenye umri wa makamu hivi, akazungumza kwa sauti huku sote tukimsikiliza kwa makini, na akiwa mshabiki wa aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya UKAWA, akasema "Mgombea wa CCM hatufai kabisa, kwanza hana hata sura ya urasi".

Ghafla hapo nikajisikia kitu kimeni-click kwenye ubongo, nilishangaa sana na hapo hapo nikajikuta nikiingilia mjadala kwa kuuliza sura ya urais unaonekanaje. Kuanzia pale sikubahatika kujua muonekano wa sura ya uraisi hadi sasa.

Lakini kwa kujaribu kufikiri, na kuunganisha dots nikajikuta nikimtafisiri mzungumzaji kuwa ni mwanamke na kuunganisha uchaguzi mkuu wa 2005, ambapo aliyekuwa mgombea wa CCM alipita kwa kishindo kikubwa sana, pengine kuwahi kutokea katika zama za vyama vingi vya siasa.

Hapa nikajikuta pia nikijiuliza iwapo sura ya uraisi umefanana na sura ya Kikwete au Lowassa? Hata kaktika kupitapita na kutaniana na wadada, baadhi walikiri kuwa 2005 walipiga kura kwa kuangalia sura na si vinginevyo.

Ndipo nikapenda nililete swala hili hapa jukwaani, pengine tusaidiane kujulishana iwapo uraisi una sura, na kama ipo huonekanaje? Na je hii hulka bado ipo katika kizazi cha leo? Na kama bado ipo, je inatufaa? Na kama haitufai, tuiondoeje?

Karibuni wadau, lakini very sorry kwa maandishi mengi.
 
Mkuu hao ndo wanawake ,,wanapenda vitu vya kijinga jinga,,kwa hakika mheshimiwa aliyestaafu alipendwa sana na wadada Kwa rangi yake na mipasho,,alikuwa mtu wa swagga ambazo wakinamama wengi wanazikubali,,,
 
Kweli ni swali la kizushi!
Ndiyo ni swali la kizushi, lakini hali hii ilitugharimu kiasi gani kuanzia mwaka 2005?
Mkuu hao ndo wanawake ,,wanapenda vitu vya kijinga jinga,,kwa hakika mheshimiwa aliyestaafu alipendwa sana na wadada Kwa rangi yake na mipasho,,alikuwa mtu wa swagga ambazo wakinamama wengi wanazikubali,,,
Ndio utajua kuwa kumbe kuna kundi kubwa la watu wanaofanya maamuzi ya maisha yao kwa kuangalia sura tu na si vinginevyo....! Lakini la msingi ni je, hii sumu tuiondoeje?
 
Ndiyo ni swali la kizushi, lakini hali hii ilitugharimu kiasi gani kuanzia mwaka 2005?

Ndio utajua kuwa kumbe kuna kundi kubwa la watu wanaofanya maamuzi ya maisha yao kwa kuangalia sura tu na si vinginevyo....! Lakini la msingi ni je, hii sumu tuiondoeje?
Kaka kama ingewezekana kumaliza hii sumu basi biadhara zote zingekufa duniani,,,sababu mwanamke ni weakness unayotumika kuvutia kila kitu hata wewe unavutika zaidi Kwa wanawake ,,kiukweli huwezi shinda hii vita,,si tuu Tz na Ccm,,hata wangekuwa chademakutumia wanawake kwa kuvutia mpango wako nimkakati thabiti,,mfano uliona wakina wolper na wengineo,,,
 
Back
Top Bottom