IamPrince George
JF-Expert Member
- Nov 22, 2014
- 412
- 168
Mahaba waliyokuwa nayo wanachadema kwa Lowassa yamepotea kabisa baada ya kujua yafuatayo.!
~Alijiuzulu uwaziri mkuu sababu ya skendo ya ufisadi ya Richmond Iliyokuwa ikilipwa Milion 152 kwa siku kwa muda wa siku 730 yaani miezi 24. Sasa milion 152 mara siku 730...aisee alituchapa!
~Alijimilikisha ranchi nne za taifa akiwa waziri wa maji na mifugo
~Akiwa waziri mkuu huduma ya usafiri wa reli ulizorota sababu yeye anamiliki kampuni ya GMS yenye kumiliki scania 900 hivyo kama reli ingeimarishwa angekosa dili.
~Akiwa waziri mkuu tenda za halmashauri na manispaa zote katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro za uchapaji,chakula,usafi n.k alipewa dada yake kupitia kampuni yake ya ALPHA Co. Ltd
~Akiwa mkurugenzi wa AICC aliiba mali nyingi sana ikiwa kuuza magari na ubadhirifu wa fedha kiasi cha kurudisha nyuma ukumbi ule
~Akiwa waziri mkuu alipinga wazo la kujenga bomba la gesi badala yake akaleta wazo la mvua za kutengeneza huku akiwa muuza majenereta mkubwa kupitia kampuni ya Alpha iliyokuwa ikisimamiwa na Fred ambaye ni mwanaye
~Aliwahi kumpa mwanaye paundi laki nne kwenda nchini Uingereza kununua nyumba ya kifahari katika jiji la London akakamatwa
~Kampuni za Lowassa za Barare Ltd, Intergrated property management na Alphatel partinership ziliifanya Tanzania kukosa msaada wa kibajeti 2006 toka Uingereza kwa makosa ya utakatishaji fedha zilizokuwa zikanunue jumba la kifahari London
~Anamiliki kampuni za uchimbaji madini
~Akiwa mmoja wa wanahisa wa Vodacom Tanzania ametajwa kushiriki uwizi wa zaidi ya bilion 675 taarifa iliyotolewa na gazeti la kiingereza la hapa nchini hali iliyoifanya serikali kuu kupoteza bilion 125 kama kodi.
KIUFUPI JAMAA NI EBOLA KWA NCHI. TUMPE MUDA AENDE KUSIMAMIA BIASHARA ZAKE.
POLEPOLE UNAMTUMIKIA NANI?
Na Ally Rama.
Nimetoka kuangalia mdahalo kuhusu amani; umoja na haki kupitia star TV pale ubungo blue pearl hotel..
Kwa title ya mdahalo; niliamini watajadili kuhusu haki; umoja na amani lakini wakajielekeza kwenye uchaguzi mkuu bila kugusa vipengele husika..
Miongoni mwa hoja zilizotawala mjadala (si kwa Bahati mbaya) ni mjadala Wa urais kati ya wagombea wawili Magufuli na lowassa..
Polepole kwa nafasi yake; aliendelea kuonesha chuki zake kwa lowassa na alitumia mchakato Wa kupata katiba mpya kuelezea namna Lowassa alivyohujumu mchakato ule hivyo hafai kuwa rais na huo ndio ugomvi wake na lowassa ulipoanza..
Polepole kwa maelezo yake anasema; Lowassa ndie aliharibu mchakato na akaratibu harakati za kupinga kupatikana kwa katiba ya wananchi kwa kigezo cha kuwa mapendekezo Yale yanadhoofisha taasisi ya Urais..
Akaendelea kudai; walienda kumuomba akubali maoni yao lakini akakataa..
Nikaanza kuukumbuka mchakato ulivyokaenda na nikaja na maswali yafuatayo..
1: Lowassa ndani ya CCM hakuwa mwenyekiti wala katibu mkuu..
ndani ya serikali hakuwa hata Waziri..
Sasa nguvu ya kuhodhi mchakato ule bungeni aliitoa wapi?
2: hasimu wake kisiasa Mzee Sitta ndie Alikuwa mwenyekiti Wa bunge maalum la kufinyanga katiba ya wananchi..
Nae aliingizwa king na Lowassa??
3: mama Samia Suluhu Hassan ambaye leo ni mgombea mwenza Wa magufuli; nae aliingizwa king na lowassa afinyange katiba?
4: Mwigulu Nchemba; January na Vijana wengine Makini ndani ya CCM waliipinga rasim ya warioba; nao waliingizwa king na lowassa?
5: inajulikana hata adui mwingine Wa lowassa; paul Makonda alishadadia swala la kifinyanga maoni ya wananchi hasa kwenye kipengele cha muundo Wa muungano..
Akampiga Mzee warioba...
Akazawadiwa ukuu Wa Wilaya ya kinondoni..
Nae aliingizwa king na lowassa??
6: membe nae alipinga muundo Wa muungano..
Nae aliingizwa king na lowassa??
7: Mzee kikwete km rais Wa nchi aliishiwa nguvu ya kuhimili mihemko ya wabunge Wa CCM hadi akaelekea kibra..
Nae aliingizwa king na lowassa??
Aliwazawadia ukuu Wa wilaya Akina Makonda kwa kupinga katiba ya warioba..
Nae aliingizwa king na lowassa??
Eti kweli lowassa pekee ndie alikwamisha mchakato ule?
Kakangu Polepole; hebu kuwa mkweli hapa...
Hao unaowapigia kampeni ndio walokwamisha mchakato Wa katiba mpya..
Polepole Vaa uzalendo; Vaa utanzania..
Zungumza ukweli..
La sivyo tuambie unamtumikia nani??
Ni wazi kuwa Pole Pole hana Moral Authority ya kuwaambia Watanzania kuwa Lowassa aliingilia Mchakato wa Maoni ya Watanzania katika kuipata Katiba Mpya, Mchakato wa kuipata Katiba Mpya kama ni kukwamisha nadhani arudi kwa Mwenyekiti wa Ccm ambaye aliridhika na mambo ya kihuni yaliyopelekea kuvunja utu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Time ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Pole pole alikuwa mfuasi wa Katiba ya maoni inayoungwa Mkono na Wananchi ya Serikali tatu na aliipigania sana na ambayo inaungwa Mkono na UKAWA. Ni ajabu sana kuona anaegemeza matusi na hoja dhaifu kwa Mgombea Urais wa UKAWA ambaye anatetea Katiba aliyoipigania.
Tumpuuze kwa kuwa in dhahiri kuwa anatumika na Ccm.
Edited by,
pg.
Anawatumikia wazalendo wa nchi dhidi ya mafisadi wanaotaka kuwa viongozi