Swali Fikirishi: Je, vyama vya upinzani vinaweza kuishi bila ruzuku kwa miaka mitano, ikiwa vitaamua pia kususia Uchaguzi Mkuu?

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,335
5,184
Kwanza kabisa naungana na kupongeza maamuzi waliyochukuwa; madudu yalikuwa yamezidi zaidi, na vitu vya aibu vimefanyika bila haya.

Sasa nawaza tu nje ya boksi; je, hayo madudu yakiendelea hadi mwaka kesho kwenye uchaguzi mkuu hali itakuwaje, ikiwa wataamua pia kujiondoa? Wataweza kuishi bila ruzuku? Kwa maana kutoshiriki uchaguzi mkuu ni kwamba hapo hata ruzuku wataikosa. Hili wamejiandaaje nalo?
 
Naungana na kupongeza maamuzi walito chukua, madudu yalikuwa yamezidi zaidi, je, hayo madudu yakiendelea hadi mwaka kesho kwenye uchaguzi mkuu hali itakuwaje, ikiwa wataamua pia kujiondoa? wataweza kuishi bila ruzuka, make kutoshiriki uchaguzi mkuu ni kwamba hapo hata ruzuka wataikosa, hili wamejiandaaje nalo?

Tunaendeshwa nakatiba

Bahati mbaya kinara wetu haitambuwi katiba, haifuati wala haisimamii

Ruzuku ipo kwa mujibu wa katiba, sio hiari, sio hisani wala sio kwa utashi wa mtu.

Vyama vya siasa vyote kwa ujumla wake vipo kwa mujibu wa katiba yetu.

Fedha za ruzuku sio za mtu binafsi, zinatoka kwetu watanzania kuanzia mkulima mdogo kabisa, muuza karanga, mfanyakazi na mfanyabiashara (wote kwa pamoja niwanachama either wa upinzani au chama tawala au raia wasionachama chochote)

Ukichanganya hayo yote, sitegemei kinara wetu ajimilikishe uhalali wa kuipora haki ya watanzania nakuikanyaga katiba kwa kuendelea kupuuza kanuni, miiko na taratibu tulizojiwekea.

Na nivema tuelewe kila lenyemwanzo halikosi kuwa namwisho

Nibusara yakawaida kinara wetu afikirie kumaliza vizuri zaidi badala ya kutuharibia taifa na kumaliza vibaya.

Bora kukosa ruzuku, lakini kuhakikisha tunakusimamia utu, maadili, sheria na taratibu zetu....katiba iheshimiwe
 
mkuu umetoa maelezo marefu ya katiba, utapataje ruzuku bila kushiriki uchaguzi?

Hiyo ruzuku ndio imekuwa ikitumika kama fimbo ya kutishia vyama, hivyo vyama hata visipokuwepo tunaweza kufanya siasa na kamwe hatutaiunga mkono hiyo ccm, na nina bashiri hali ngumu zaidi kwa ccm kwani itabidi ilazimishe kupendwa huku ukiwa haikubaliki kabisa. Ninaamini pasipo shaka tutapata hali nzuri zaidi ya kisiasa kuliko ilivyo sasa.
 
Mkuu tindo, siyo wengi waliyo shiba kama wewe, na ambao wanaamini katika haya, kuna watu wataona bora kugombea humo humo ili wasije wakakosa ulaji wa miaka mitano, ila kwa mwanzo huu, madudu haya yaliyo fanyika, wangekaza hadi uchaguzi mkuu, sioni haja ya kutowakilishwa ngazi ya chini halafu, uje ugombee ubunge ili uwakilishwe ngazi ya juu, eti sababu kuna ruzuku

Vyama vya upinzani vinaendeshwa na wananchi wapenda demokrasia kama sisiemu inavyoendeshwa na serikali kwa njia za kifisadi.

CCM ndiyo ya kuonea huruma. Wakiondolewa madarakani ni kifo cha ghafla.
 
Mkuu tindo, siyo wengi waliyo shiba kama wewe, na ambao wanaamini katika haya, kuna watu wataona bora kugombea humo humo ili wasije wakakosa ulaji wa miaka mitano, ila kwa mwanzo huu, madudu haya yaliyo fanyika, wangekaza hadi uchaguzi mkuu, sioni haja ya kutowakilishwa ngazi ya chini halafu, uje ugombee ubunge ili uwakilishwe ngazi ya juu, eti sababu kuna ruzuku

Tatizo hata wakishiriki sisi wapiga kura tunaowapigia kura hatutapiga mpaka tupate uhakika wa kura zetu kwenye box la kura kuheshimiwa, hivyo watapoteza muda tu wakishiriki. Tunajiandaa kwa plan B bila kutegemea chama chochote cha siasa, maana hapa ndio penye tatizo la msingi. Tutaweka utaratibu uhalisia kupitia katiba ya rasimu ya Warioba. Nadhani umeona jinsi umma ulivyogoma kujiandikisha kwani tumegundua uchaguzi ni zoezi lililojaa ushenzi wa hali ya juu.
 
Kwa maoni yangu vyama pinzani vilianza bila ruzuku,hivyo ruzuku sio kipaumbele kwanza inaleta migogoro ndani ya vyama na ndio maana wananchi hawasikilizi hii ni kwa vyama vyote vya siasa Tanzania
 
kama JPM atakua ofisini 2020-2025 nchi yetu itakua kwenye mporomoko wa kiuchumi, sahau kuhusu ruzuku ya vyama, hata wewe hautaweza kununua sabuni, panado wala sukari.
 
Chama sio lazima kiendeshwe kwa ruzuku kwani inategemeana na chama kina rasilimali kiasi gani. Na miradi ya chama pia bahati mbaya sijui miradi ya chadema lakini ukija kwa rasilimali watu wako vizuri maana yake wataweza kupata michango kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali.
 
Kwanza kabisa naungana na kupongeza maamuzi waliyochukuwa; madudu yalikuwa yamezidi zaidi, na vitu vya aibu vimefanyika bila haya.

Sasa nawaza tu nje ya boksi; je, hayo madudu yakiendelea hadi mwaka kesho kwenye uchaguzi mkuu hali itakuwaje, ikiwa wataamua pia kujiondoa? Wataweza kuishi bila ruzuku? Kwa maana kutoshiriki uchaguzi mkuu ni kwamba hapo hata ruzuku wataikosa. Hili wamejiandaaje nalo?

..kunaweza kuibuka upinzani mpya usiohitaji ruzuku unaofanana na ule wa Tahrir Square au uliotokea Sudan hivi karibuni.

..upinzani wa aina ya cdm, act, cuf ni mzuri na una-guarantee stability ya nchi. CCM inakosea kujenga mazingira ya uhasama na uadui dhidi ya wapinzani.
 
haya mkuu

Back
Top Bottom