Hata kama zawadi kutoka kwa mama yangu mzazi kama siipendi nitasema hasante, halafu nitamueleza nikiwa namuangalia usoni kwamba SIIPENDI na sitoitumia.
Hahahahahah Roulette na jpili inatakiwa uivae ili yeye aridhike so utaivaa?Pokea tu. Be happy for the efforts she put in it. Baadae (few days) unaweza kuongea nae na kumwambia unacho fikiria kuhusu zaawadi. Kumbuka kumshukuru na kumsifu kwa efforts zake, halafu mwambie angetaka ufurahi zaidi maybe angetafuta ambayo iko hivi, na hivi. Just find the right time and her right mood before you discuss.
Lizzy well said ila saa ingine inatokea unaghafilika mimi nakumbuka tukiwa kwenye u boy friend na u girl friend nilishawai kumnunulia mpenzi wangu nguo ya ndani yenye msg ya I LOVE U nikiamini ni bonge la zawadi kumbe hakuipenda na kuniambia alishindwa yaani mpaka nimekuja muoa ndo nagundua bado ipo sandukuni.Kabla ya hapo inabidi watu tujifunze kuwasoma wenzi/ndugu na marafiki zetu. Jua style yake ya mavazi na mapambo, vitu vya ndani, aiana ya mitoko mpaka na vyakula anavyopendelea.
Yani ukimpa mtu kitu huna wasiwasi moyoni, unajua kabisa atapenda tena sana.
BTT. . .ntashukuru ila ntamwambia haitonipendeza/haiendani na mimi. Ntajitahidi aelewe kwamba kanifurahisha sana japo siwezi kuivaa.
I like it.kwa mie binafsi nitaipokea kwanza nampongeza kwa zawadi aloniletea, kadri cku zinavoenda ntakuwa najitahd kumwambia vitu ninavyopendelea. dada Lizzy kaongea vyema kwamba ni vizur kuwasoma wenzi wetu,kwa kujazia pia ni vizur pia kuwa na tabia ya kuuliza anapendelea nini. mf. unaweza kujitanguliza "baby me huwa napenda skin jeans, hv we wapenda jeans aina gan atakujibu" cku ya cku utakuwa umepata jibu mwez wako anapendelea nini,pia unaweza kuangalia nguo zake huwa anapendelea nguo/viatu...