Sureboy: "Hata Nikiacha Mpira Kesho Hakika Nimepata Mrithi Wangu" (Fei Toto)

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,287
9,923
Leo Niwape Story Fupi Kuhusiana Na Mimi Na Feisal Salum “FeiToto”.

Nakumbuka Ilikua Mwaka 2016 Wakati Tunaenda Zanzibar Na AzamFc Katika Kombe La Mapinduzi.

Wakati Tupo Njiani Wachezaji Wenzangu Mudathir Yahya & Abdallah Kheri Sebo Wakaniambia Kuna Dogo Yupo Huku Zanzibar Anajua sana Mpira Na Anakukubali Kweli Mpaka Na Yeye Anajiita “SUREBOY”

Nilitamani Kumuona Huyo Dogo Bahati Nzuri Agrey Morris Alikua Anajuana Na Uongozi Wake Wa Team Yake Ya Vijana.. Akawapigia Simu Wamwambie Aje Hoteli Tukiyofikia.

Dogo Mwenyewe Ndio Huyu Mnayemjua Feisal Salum Abdallah “Fei Toto”. Alifurahi sana Kuniona Tukapata Wasaa Wakukaa Pamoja Mchana Kutwa Kambini. Akiniambia Ndoto Zake Ni Kucheza Bara Tena Team Kubwa.

Nilimpa Moyo Na Kumuambia Akaze Aongeze Mazoezi. Kiukwel Alikua Ni Mcheshi Na Mskivu Sana Nikatokea Tu Kumkubali Kama Mdogo Wangu Wa Damu Kabisa.

Miaka Ikawa Inaenda Lakini Hatukua Na Mawasiliano Sana Ila Kila Anapokuja Dar Kwenye Mechi Zao Lazima Aje Chamanzi Camp.. Anisalimie Na Kama Kuna Vitu Vya Kusolve Viatu, Jezi, Nauli n.k

Miaka Baadae FEITOTO ni Mchezaji Mkubwa Sana Katika Nchi Hii.. Na Pengine Ni Mchezaji Maarafu Hata Kushinda Mimi. Lakini Heshima Yake Kwangu Haijawahi Kushuka.

Kipindi Tumesimamishwa Na AzamFc, FEITOTO ni Miongoni Mwa Wachezaji Walionipigia simu Na Kuniuliza “BABA Vipi Sikuoni Uwanjani” Ananiita Baba Kwa sababu Yeye Ni Feisal Salum na Mimi Ndio Salum 😅
Akaniambia Njoo Basi Baba Tufanye Kazi Wanachi.

Leo Hii Ndoto Za Kijana Mdogo Aliyenichukulia Kama Kioo Chake Zimetimia Na Tupo Pamoja Na Tunashinda Makombe Pamoja.

Mwisho Wa Story Usimdharau Mtu Yeyote Katika Maisha Hujui Anaweza Kuja Kua Nani Kesho Leo Hii Feitoto Ni Captain wangu.. Na Wakati Mimi Naminyana Na Kina Yaya Toure Taifa. Ananiambia Alikua Shule Ya Msingi Ananiangalia Kwenye TV.

All The Best My SON.. Hata Nikiacha Mpira Kesho Hakika Nimepata Mrithi Wangu
Nimepata Messages Nyingi sana Za Watu Kupenda Story Yangu Na Feitoto.


UPDATES
Na Maombi Ya Watu Wengi Niwe Nasimulia Story Mbalimbali Ili Watu Wajifunze Na Wajue Changamoto Za Ndani Na Nje Ya Mpira.

Ikiwa Mimi Ni Miongoni Mwa Watu Waliocheza Ligi Kuu Kuanzia Umri Mdogo Sana. Hii Itawa Inspire Vijana Wengine Walio Mtaani Kuona Kwamba Inawezekana

Kuanzia Kesho Nitaanza Kuandika Historia Tofauti Za Kuelimisha 🙏🏾

Nitaanza Na Mechi Ambazo Sitaweza Kuzishau Katika Maisha Yangu Ya Soka.


SUREBOY NA MECHI AMBAYO HATOISAHAU.

UPDATES
Ilikua Ni June 16 2013, Timu Ya Taifa Taifa Stars Tulikua Tunavaa Na Ivory Coast Katika Mechi Ya Kufuzu Kombe La Kombe La Dunia 2014.

Kiukweli Ilikua Ni Mechi Kubwa Sana Kwangu Na Taifa Kwa Ujumla Kulingana Na Ukubwa Wa Majina Na Viwango Vya Wenzetu Hapa Africa.

Ukiwa Kama Mchezaji Mdogo Ukiitwa National Team Swala La Kuanza Katika Kikosi Cha Kwanza Linakua Halipo Kichwani Kutokana Na Wakongwe Unaowakakuta Katika Kikosi Wana Experience Na Washacheza Mechi Kubwa Tofauti Na Mimi.

Basi Hadi Siku Ya Mechi Kocha Kim Polsen Hakutoa Line Up Mapema Nami Nikijua Kabisa Leo Sitokuepo Kwa Maana Ukiangalia Tu Nafasi Nnayocheza Kuna Watu Wabadi 😅 Athuman CHUJI, ABDI KASSIM, JABIR AZIZ, SHABAN NDITI na RAMADHAN CHOMBO.

Kwa Kuangalia Tu Hapo Hata Ungekua Wewe Usingeweza Kunipanga 😅 Kocha Kim Polsen Baada Ya Chakula Cha Mchana Akataja Kikosi, Hamad Bin Vuu Nimeanza Katika Starting LINEUP.

Kiukweli Nilishikwa Na Tumbo La Hofu Na Uoga Sana Kwa Maana Hata Saikoloji Pia Nilikua Sijajiandaa Kwa Ajili Ya Mechi. Aidha Ya Yote Nikajua Nitasimama Na Mtu Mkongwe Ambaye Ataziba Makosa Nikikosea Kocha KIM Pia Akamuanzisha Mtoto Mwezangu Mwingine .. Guess Who FRANK DOMAYO 🙌🏾

Cha Kwanza Kabisa Nilimpigia Marehem Mama Yangu Simu Kumpa Habari. Akaniombea Dua Na Akaniambia Niswali Rakaa 2 Kabla Ya Kutoka Kwenda Kwenye Mechi, Nami Nikafanya Hivyo.

Mechi Ilikua Ina Presha Kubwa Ukizingatia Unacheza Na Watu Ambao Tunawaona Kila Weekend Katika TV Kama Yaya Toure,Gervinho Na Mastaa Kibao, Na Ndio Ilikua Mechi Ya Kwanza Kucheza Na Mashabiki Wengi Sana Pale Taifa Na Nikiwa Bado Mdogo.

Hakika Ni Mechi Ya Kihistoria Sana Katika Maisha Yangu Niliweza Kuhimili Mpira Na Kufanya Kile Kocha Alikua Anataka.

Tulipoteza Mechi Hiyo Kwa Bao 4 - 2 Lakini Asilimia Kubwa Ya Mashabiki Wa Taifa Stars Waliridhishwa Na Kiwango Cha Wachezaji Wao.

Wakati Tupo Tunaelekea Vyumbani Legendary Edo Kumwembe Alituita Mimi Na SHOMARI KAPOMBE na Kutupeleka Kwa Mtu Mmoja Mashuhuri. Ni Nani Mwingine YAYA TOURE!!

Wakati Tunafika Kwa Yaya Walikuepo Viongozi Wa Mpira Kibao Pamoja Na Waandishi Wa Habari

Neno Lake La Kwanza Akamuuliza Rais Wa Tff Kipindi Kile Leodegar Tenga. Hawa Wanacheza Hapa Hapa? Jibu Lake Lilikua Ndio.. YAYA Akasema “Hawastahili Kucheza Hapa Kwa Ukubwa Wa Kipaji Chao.. Hakikisheni Mnalinda Hii Tunu” Na Nitawapa Contacts Za Rafiki Yangu Raia Wa Ufaransa. Na Baada Ya Mechi Nyingine Ya Marudiano Ivory cost Ningependa Tuwasiliane.

Kufupisha Story Miezi Miwili Baadae Mwanangu SHOMARI KAPOMBE Anasaini Ufaransa Ligi Daraja La Nne AS CANNES. Mimi Bado Nikawa Azam Fc.

SIKU NIKISTAAFU NITAWADITHIA WAJUKUU ZANGU STORY HII YA KUSISIMUA JUU YA KIPI KILIKWAMISHA NDOTO YANGU YA KUCHEZA ULAYA. Najua Wataumia,Najua Watalia Ila Ndio Soka Letu Kivyetu Vyetu 🙏🏾⚽️

Tusubiri Kitabu Ndugu Zangu..!!
 

Attachments

  • Screenshot_20220919-104702.png
    Screenshot_20220919-104702.png
    254.7 KB · Views: 11
Huwezi kuamini! Kuna watu watanuna eti baada kusoma huu uzi!
Binadamu ndivyo tulivyo mkuu ,lkn jamaa ajaandikaa baya la kumkera mtu ila kakumbushia tu maisha n watu na watu hao hao pia wanaweza kukufelisha kwa namna yyt ilee,mchango wa edoo kumwembe nimeuoana .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom