Kwa wale ambao wanaotaka mpira wa kujilinda ugenini basi msahau kwa Gamond

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,357
2,497
Baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Belouizdad kuna maneno mengi ya kiuchambuzi kuwa Yanga walifungua turbo wakati wapo ugenini jambo ambalo limepelekea kufungwa magoli. Baada ya mechi ile Gamond hakubadilisha falsafa yake aliingia kwenye mechi ya Al Ahly kwa mchezo ule ule wa mpira wa kushambulia kwa kasi, mechi ya ugenini dhidi ya Medeama ikawa vile vile japo Yanga ilinyimwa goli la halali la ushindi.

Leo nimejaribu kusikiliza interview ya Gamondi, aisee huyu jamaa mpira kwakeni burudani anapenda sana afurahie na afurahishe watu kwa soka safi na sio kupaki treni au kubutua butua mpira. Tumsikilize mwenyewe anachosema:

“Kucheza na Al Ahly sio jambo rahisi, tunafahamu ukubwa wa klabu hii na tupo tayari kupambana, ni wasaa wa kuonesha sanaa ya soka letu ni matarajio yangu kuona mchezo mgumu wa kimbinu naheshimu sana daraja la Ahly lakini niwahakikishie hatuna hofu yoyote tumekuja kushindana sio kukamilisha ratiba, malengo yetu ni kushinda mchezo huu” Miguel Gamondi

“Mimi sio kocha ambaye napendelea kuzuia timu kwa kukaba dakika 90, mpira kwangu ni kama tamasha la maonesho nafikiri mkinifuatilia utagundua niliwahi kuja hapa zamani, soka langu ni la kushambulia na siwezi kubadilisha sanaa ya soka langu bila kujali nakutana na mpinzani wa namna gani nitaheshimu wapinzani wangu lakini kwangu heshima sio hofu”

“Kila ninapoandaa timu naanda timu kushinda na si vinginevyo mimi ninawaamini wachezaji wangu kwa kiasi kikubwa nimewahi kucheza na Al Ahly nikiwa na Platnumz Stars na kuwa klabu ya kwanza kuifunga Al Ahly kutoka Afrika Kusini, Kwahiyo sina wasiwasi wala hofu ya kucheza dhidi ya timu kubwa” Miguel Gamondi

Mwisho wa kunukuu kocha wa mpira burudani.
 
Even more . Check his success curve in sofa score . Yanga is his 3 carrer peak
Umesema hana kipya Africa, sasa kocha asiyekuwa na kipya anawezaje kupata mafanikio? Kama asingekuwa na jipya basi ungeona yupo vile vile kama alivyokuwa anafundisha timu zingine. Ila mpaka anapata mafanikio ina maana kabadilika kimbinu na kiufundi na kifalsafa. Usiishi kwa kukariri past. Maisha yanaende mbele
 
Umesema hana kipya Africa, sasa kocha asiyekuwa na kipya anawezaje kupata mafanikio? Kama asingekuwa na jipya basi ungeona yupo vile vile kama alivyokuwa anafundisha timu zingine. Ila mpaka anapata mafanikio ina maana kabadilika kimbinu na kiufundi na kifalsafa. Usiishi kwa kukariri past. Maisha yanaende mbele
Well kapita team zote kubwa Africa. The game needs fresh blood new tactics . Sioni Akitoka unless afanye makubwa Sana Kama to win caf champions league
 
Kushinda ndio kiwe kipaumbele...

Hatua ya robo fainali itakuwa na ahueni kiratiba endapo Yanga ataongoza kundi na ndio Al Ahly hesabu zake huwa hivyo pia miaka yote...
 
Well kapita team zote kubwa Africa. The game needs fresh blood new tactics . Sioni Akitoka unless afanye makubwa Sana Kama to win caf champions league
Tena kaskazini huko kaishapita sana..
 

Attachments

  • FB_IMG_1708932028393.jpg
    FB_IMG_1708932028393.jpg
    15.4 KB · Views: 1
"mpira kwangu ni kama tamasha la maonesho nafikiri mkinifuatilia utagundua niliwahi kuja hapa zamani, soka langu ni la kushambulia na siwezi kubadilisha sanaa ya soka langu bila kujali nakutana na mpinzani wa namna gani nitaheshimu wapinzani wangu lakini kwangu heshima sio hofu”
👏👏👏👏👏👏👏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom