Supu ya kupika kipindi hiki

Binti1

JF-Expert Member
Jul 8, 2013
662
1,745
Karibuni I'm enjoying a soup na nimependa share nanyi recipe.Tamu sana.
MAHITAJI (kwa mtu mmoja waweza ongeza ku fit idadi ya walaji)
Ndizi ama viazi 2,kuku wa kienyeji(nusu),vitunguu maji vitano vikubwa,ndimu,carrott,soy sauce,swaumu punje 2.

JINSI YA KUANDAA: Osha kuku na weka kwenye sufuria achemke(wa kienyeji huchukua muda kuiva tofauti na wa kisasa).Andaa vitu vingine kwa kuosha,kumenya na kukatakata.

Kuku Akisha chemka na kuelekea kuiva ongeza vitunguu swaum na vitunguu maji(raha ya hii pishi ni vitunguu).Ongeza pia na Ndizi ama viazi.Viiiiva weka carrott na umalizie kwa kuweka soy sauce na (ajina moto kidogo). Wacha vichemke na kublend vizuri kabla ya kutoa tayari kwa kuliwa.Waweza ongeza ndimu na pilipili.Enjoy like I did!!!
28a1c1e7001edcf4b18c96088822be7d.jpg
 
Mashallah!!

Supu inavutia,nitajaribu siku moja
Hapo kwa juu ukinyunyizia pilipili manga ita noga sana
Asante ndugu kwa ujuzi huu!!
 
Akiwa kuku wa kisasa step zake zikoje wakuu. Nataka nikaungurumishe jioni hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom