mabereng'ombe
Member
- Nov 22, 2013
- 70
- 18
Watu wengi wanaamini kuwa vyakula vinavyouzwa katika Supermarket ni bora na salama, lakini wanakosea sana!
Katika hali ya kushangaza na kutisha sana, katika Supermarket moja iliyoko kwenye jengo la kituo cha mafuta Oilcom pale eneo la Vertenary wilayani Temeke kunauzwa unga unaoitwa wa lishe ambao umeharibika.
Unga huu unazalishwa na kampuni moja ya Fortune Food Products una wadudu.
Mimi nilinunua unga huo, nikagundua kuna wadudu weusi. Nikawapa watu wa TFDA waufanyie kazi lakini nasikia hawajachukua hatua zozote.
Nimeulizia naambiwa kampuni hiyo iliomba kibali lakini haijapewa baada ya kukosa vigezo. Sasa inakuwaje watu waliokosa vigezo waendelee kuruhusiwa kuzalisha chakula? Lakini pia ni utaratibu gani ambao --------- na hizi Supermarket kupokea vyakula na kuviuza? Sijui kama wasimamizi wa sheria wanalijua hili. Watanzania wanalishwa vyakula ambavyo havina ubora, havina TBS lakini eti vinauzwa katika Supermarket. Hii ni aibu na usanii mkubwa!