Mghoshingwa
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 305
- 74
inatusaidia kujua tumezungukwa na watu wa namna gani ili tujue jinsi ya kuishi nao, mfano ukishajua mtu fulani ni mgomvi by nature utagombana nae wa nini?
Na tusio na makabila sijui tutapimwaje..?
Mkuu inasaidia sana mfano mm wakati posa inaletwa kwetu niliulizwa na wazee huyo mchumba ni kabila gani, nilipotaja kabila lake....walikaa wakajadili then wakasema kabila hili halina shida. Hii inamaana kuwa wazazi pia wanapenda kujua mtoto wao anaoa au olewa na mtu wa kabila gani ili waweze kumshauri jinsi ya kuishi na watu wa kabila husika hata kama hao watu hawana tabia hizo. kinga ni bora kuliko tiba.
Personally naona threads za makabila siyo mbaya... Lakini bora kwa mtindo ule ambao Zinduna huleta threads zake juu ya makabila zikilenga kuelimisha. Haipendezi kwa kweli mtu kuja na thread then anauliza kama hawa wana tabia ipi? Wengine wanakuja na majibu ya kizushi na kutopendeza kwa wanakabila husika... Mghoshingwa nakuunga mkono katika hili...
Tunaomba nao mods wajaribu kulitazama hili kwa undani.... CC to INNOVATOR, Roulette, Fang, Pruner, Moderator
Wana jf hususani wapenzi wa MMU, Heri ya mwaka mpya.
Nina andika ujumbe huu baada ya uchunguzi wa muda mrefu wa nyuzi mbali mbali (threads) zinazo wekwa na wadau mbali mbali.
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikikerwa na kushangazwa na nyuzi (threads) mbali mbali zinazotaka kujua tabia za makabila mbali mbali, jambo ambalo kwa karine hii na kwa jamii iliyo komaa kifikra kama ya Jf sidhani kama ni mahali pake. Kwa mfano utakuta mtu ame post : mabinti wa kiangaza, Tabia za wanyamwezi, wanawake wa kifipa n.k.
Hivi ina saidia nini kujua tabia za makabila hasa katika kipindi hiki ambacho ukabila sio kigezo cha msingi katika kuanzisha mahusiano? Kwanini mambo haya ya kikabila msiya peleke kwenye JUKWAA LA HISTORIA ( IF ANY).
Hii inanifanya nijiulize maswali mengi sana bila majibu.
1. Je nikweli mambo ya msingi ya kujadili hapa MMU yamekwisha kabisa.
2. Ina maana suala la kujua tabia za makabila mbali mbali ni burning issue kiasi hicho?
There is no good sense there in.