MovingForward
JF-Expert Member
- Nov 10, 2009
- 489
- 49
Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba kila mwaka watu wapatao 1,600 hupoteza maisha kwa kichaa cha mbwa.
Hata hivyo, katika hali inayoshangaza, katika manispaa ya Sumbawanga na maeneo mengi ya mkoa wa Rukwa mbwa wanakatiza mitaani hovyo bila uthibiti wowote. Pamoja na matukio mengi ya watu kuumwa na mbwa yanayoripotiwa, hakuonekani kuchukuliwa tahadhari yoyote na kudhibiti kuzagaa kwa mbwa kunakoonekana.
Ni vyema mamlaka zinazohusika kulitupia jicho jambo hili la kuzagaa kwa mbwa mitaani, katika manispaa ya Sumbawanga na kwingineko.
Dar es Salaam. Watu 1,600 hasa watoto hufa nchini kila mwaka kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Hayo yalielezwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Mashingo.
Dk Mashingo alisema vifo hivyo hutokana na wagonjwa hao hasa watoto kukosa chanjo kwa wakati.
“Tuna vituo saba pekee hapa nchini vinavyotoa huduma hizo,”alisema Dk Mashingo.
Alitaja mikoa ambayo vito hivyo vipo kuwa ni Dar es Salaam, Tabora, Mwanza na Mikoa ya Kusini