Waziri mkuu mwenye rekodi ya kukaa madarakani Kwa kipindi cha miaka kumi na baadae kubatizwa jina la Mr zero na wafuasi wa Chadema, sasa ameibuka.
Sumaye ambae alihama ccm na kujiunga na chadema mwaka 2015 ,ameweka wazi kwamba Magufuli anaiga kila kitu kutoka chadema.
Msimamo huu umeenda kinyume kabisa na bavicha wengi ambao kila kukicha wanaponda utawala wa Rais Magufuli.
Sumaye licha ya kuzaliwa na kuzeekea ccm, alikihama chama hicho na kutangaza kuwa ccm haijafanya chochote Kwa miaka 50 !! . Maneno haya aliyatamka huku akijua yeye mwenyewe amezaliwa, akabalehe na baadae kuzeekea ndani ya ccm !!
Sent using
Jamii Forums mobile app