Sumaye: Nimekubali utendaji wa Rais Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
%25255BUNSET%25255D.jpg

WAKATI Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli akitekeleza masuala mbalimbali aliyowaahidi Watanzania, ikiwa ni pamoja na kurejesha uwajibikaji na kupambana na ufisadi, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema hashtushwi na utendaji huo wa rais, kwani amekuwa akitumia baadhi ya hoja na mikakati ya Chadema kuongoza nchi.

Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea wa udiwani katika kata ya Isagehe wilayani Kahama, Sumaye ambaye alijiunga Chadema Agosti mwaka juzi baada ya kuachana na CCM, alisema mengi anayofanya rais ni sera za Chadema ila chama hicho cha upinzani hakikuwa na sera ya kubana na fedha.

Hata hivyo, Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema hakuweka wazi hoja na mikakati ya Chadema inayotekelezwa na Rais Magufuli ambaye tangu aingie madarakani ameweka msimamo katika suala la kubana matumizi ya Serikali, kudhibiti watumishi hewa na safari za ndani na nje zisizo na tija na rushwa.

Katika mkutano huo ambao pia Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa alihutubia, Sumaye alisema kama wananchi, wangemchagua Lowassa kuwa Rais, angewaletea neema ya hali ya juu kwa kuwa angekuwa na misingi katika sera anazozitekeleza.

“Mmechagua Rais mzuri (Magufuli), lakini anafuata sera za chama chetu (Chadema) ambazo tungezitumia kama tungekuwa madarakani. Wananchi wa Kanda ya Ziwa mnatakiwa kumtumia Rais Magufuli ili kufanikisha malengo yetu,” alisema huku akisisitiza kuwa hata Lowassa wananchi wangeweza kumtumia kufanikisha malengo yao.

Huku akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, John Luzinga, Sumaye aliwataka wananchi kutofanya makosa tena ya kuichagua CCM, ili wasije kujuta kwa maelezo kuwa watalazimika kuchagua diwani mwingine mwaka 2020.

Alisema Chadema kinaendeshwa kwa kufuata misingi ya demokrasia, huku akikosoa vyama kubanwa wakati nchi iriuridhia mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Akizungumzia sababu za kuhama CCM, alisema kulitokana na nchi kukumbwa na hali mbaya ya uchumi sambamba na kukosekana kwa utawala bora.

“Serikali pamoja na kubana matumizi, hali ya uchumi imekuwa mbaya. Inatakiwa kuachia fedha ili kuwafikia wananchi waweze kumudu ugumu wa maisha unaowakabili kwa sasa. Haiwezekani kila Serikali isijifunze katika hili wakati hata wataalamu wanazungumza na kushauri masuala mbalimbali,” alisema Sumaye.

Alisema kitendo cha halmashauri tatu za wilaya ya Kahama kuongozwa na CCM, huku diwani mmoja tu ndio akiwa wa Chadema, kitawafanya wananchi hao kukosa watu sahihi wa kuwasemea mambo yao.
 
Shika "adabu yako"

Kuna watu tangu Uhuru hawana huduma yoyote ya serikali tangu uhuru kuanzia Maji,Umeme,Shule na huduma nyingine yoyote hata usalama wa Mali na Maisha yao! Kwao Marais wote ni sawa kwa kuwa hakuna walichofanya.
Kuwalazimisha kuamini kama wewe unavyoamini ni ukosefu wa Adabu pia!
 
Usipomkubali JPM; ama hujui unachokitaka kwa nchi yako au ulikuwa mnufaika wa kansa ya JK almaarufu kama wizi, rushwa, ujangili na ufisadi; jirekebishe!
 
Wengine juzi walizuia mradi wa umeme usiende kijiji cha pili huku kijijini kwao nyaya za umeme zikipita juu kwa juu na wao kukosa huduma hiyo.
Kuna watu tangu Uhuru hawana huduma yoyote ya serikali tangu uhuru kuanzia Maji,Umeme,Shule na huduma nyingine yoyote hata usalama wa Mali na Maisha yao! Kwao Marais wote ni sawa kwa kuwa hakuna walichofanya.
Kuwalazimisha kuamini kama wewe unavyoamini ni ukosefu wa Adabu pia!
 
hivi huyo magufuli cha maana hasa alichokifanya ni nini. angeweza hata kubadili sharia mojawapo mbovu mimi ningemkubali, lakini kwa hali ilivyo, hakuna jipya
 
hivi huyo magufuli cha maana hasa alichokifanya ni nini. angeweza hata kubadili sharia mojawapo mbovu mimi ningemkubali, lakini kwa hali ilivyo, hakuna jipya

Waulize Mabosi wako waliokuwa wanagharamia Harambee wanauwezo huo leo baada ya Bomba mchepuko la Mafuta kung'olewa bandarini!
 
Usipomkubali JPM; ama hujui unachokitaka kwa nchi yako au ulikuwa mnufaika wa kansa ya JK almaarufu kama wizi, rushwa, ujangili na ufisadi; jirekebishe!

Kwa mfumo huu wa jpm, hamtasikia lolote baya kwasababu ni mfumo wa kibabe na hata likitokea baya kamavile ufisadi hutausikia, wewe jalibu kuchunguza mwenyewe, mbunge anapeleka mswaada wa kuwa na uwezekano wa kuwepo na ufisadi secta fulani, baada ya bunge kutafuta namna ya kuchunguza tatizo anatokea muhusika anadai ushahidi tena kwa jeuli unafikiri mfumo huu ungetumika kipindi kilichopita hata neno ufisadi msinge lisikia. EPA ilitokea kipindi cha awamu ya 3 lakini waliokuja kuiamsha ni akina lowasa na jk, tena mbaya zaidi watanzania wengi kwa kukosa elemu ya kung 'amua mambo tunawashutu viongozi wa awamu ya nne walioibua uwozo kama wao ndio wahusika, SASA DAWA YENU WATANZANIA NDIO HII YA AWAMU HII MSHANGILIE MATUKIO HADI MWISHO, NA IKIWA VITU VINAPANDA BEI NA SHILING KUENDELEA KUSHUKA. NA KWA MFUMO HUU HADI AJE KIONGOZI MWINGINE NDIO NTASIKIA MABAYA YA UTAWARA HUU, KAMA MLIZOEA KUONA BUNGE LINAJADILI MAFISADI HADI WANAONDOLEWA KWENYE NAFASI ZAO MSAHAU KABISA.
 
hivi huyo magufuli cha maana hasa alichokifanya ni nini. angeweza hata kubadili sharia mojawapo mbovu mimi ningemkubali, lakini kwa hali ilivyo, hakuna jipya
Hivi bunge limekaa lini ili serikali ipeleke miswada ya kubadili baadhi ya sheria zinazoliumiza taifa? Au mmeamua tu kuongea na kuropoka bila sababu za msingi? Bunge likikaa, serikali itakuwa na fursa ya kupeleka miswada ya sheria ambazo tunahitaji zibadilishwe, kumbuka hata Raisi alisema kuna sababu na haja ya kubadili baadhi ya sheria, mf. sheria za manunuzi...lakini mwenye mamlaka ya kubadilisha hayo sio Raisi, ni bunge..hope umeelewa!!
 
Kwa mfumo huu wa jpm, hamtasikia lolote baya kwasababu ni mfumo wa kibabe na hata likitokea baya kamavile ufisadi hutausikia, wewe jalibu kuchunguza mwenyewe, mbunge anapeleka mswaada wa kuwa na uwezekano wa kuwepo na ufisadi secta fulani, baada ya bunge kutafuta namna ya kuchunguza tatizo anatokea muhusika anadai ushahidi tena kwa jeuli unafikiri mfumo huu ungetumika kipindi kilichopita hata neno ufisadi msinge lisikia. EPA ilitokea kipindi cha awamu ya 3 lakini waliokuja kuiamsha ni akina lowasa na jk, tena mbaya zaidi watanzania wengi kwa kukosa elemu ya kung 'amua mambo tunawashutu viongozi wa awamu ya nne walioibua uwozo kama wao ndio wahusika, SASA DAWA YENU WATANZANIA NDIO HII YA AWAMU HII MSHANGILIE MATUKIO HADI MWISHO, NA IKIWA VITU VINAPANDA BEI NA SHILING KUENDELEA KUSHUKA. NA KWA MFUMO HUU HADI AJE KIONGOZI MWINGINE NDIO NTASIKIA MABAYA YA UTAWARA HUU, KAMA MLIZOEA KUONA BUNGE LINAJADILI MAFISADI HADI WANAONDOLEWA KWENYE NAFASI ZAO MSAHAU KABISA.
Dhana potofu!! Bunge kujadili ufisadi na mafisadi haitoshi; kinachotakiwa ni kuwachukulia hatua kali watuhumiwa wa uozo huo; kumbuka bunge la 9 na la 10 vilijadili ufisadi kwa kishindo kikuu nchi ikatikisika; je maazimio ya bunge yalitekelezwa?! Hapana hakuna zaidi ya Lowassa kujiuzulu ambaye hakufukuzwa kazi wala hajawahi kufikishwa kwenye chombo chochote cha sheria iwe Takukuru au Mahakama na mawaziri walioenguliwa hawajawahi kushitakiwa! Sasa JPM anaweka rekodi mpya ya kuchukua maamuzi magumu na kuwachukulia hatua makuadi wa ufisadi; ndio maana baadhi yetu tunaunga mkono kusitishwa kwa matangazo live ya TBC kwa sababu hatutaki kuona sinema za bunge bali kauli zinazofuatiliwa na matendo; hatua za utekelezaji. To walk the talk; keep it up JPM; PENYE JAMBO JEMA KUNA MASHETANI PIA!
 
Kama mmefundishwa kwa miaka 10 hamjaelewa basi acha muendelee kua wajinga hivyohivyo na hantapata wa kuwafundisha tena kuhusu kinachoendele katika nchi yenu, endeleeni kushangilia.

Nilijua huna intellectual stamina ya kutosha kusustain mjadala ulioshiba hoja! Umekata tamaa na kuamua kuingia chaka!
 
hivi huyo magufuli cha maana hasa alichokifanya ni nini. angeweza hata kubadili sharia mojawapo mbovu mimi ningemkubali, lakini kwa hali ilivyo, hakuna jipya
Taja sheria gani unataka aibadili... Na kwanini
 
Back
Top Bottom