BUBU MUONGEAJI
Member
- May 15, 2013
- 44
- 8
Kuna watu wameshaanza tayari ,nina uhakika watu hawa wanatumiwa.
Wanapinga Rasimu ya Serikali tatu kwa kigezo cha Gharama.
Eti Nchi itakuwa na Gharama Kubwa ku Run na Marais wa Tatu.
Watu kama hawa wanastahili Kukumbushwa kuwa kwa Sasa Nchi ina Ma Rais wa Tano na Wa Tatu wanatokea zanzibar.
Watu hawa wamekuwa wapofu kuona kuwa Tume ya Warioba imependekeza Baraza lenye Ma Waziri wasiozid 15.
Kwa Sasa Baraza lina Zaid ya Mawaziri 45, Mbona hawasemiGharama kubwa za ku Run the Current Baraza la Mawaziri?????
Hawaoni kuwa kwa Kupunguza Baraza la Mawaziri Mpaka 15 tUtakuwa tumeokoa Kiasi kikubwa sana Cha Fedha.
Watu wanaopinga Serikali 3 Hawastahili kuishi Tanzania,
TUSIMAME KUWAPINGA HAWA WACHUMIA TUMBO
labda umma wa kijiko.aliyewahi kuhojiwa kwa nini tanzania ni masikini wakati ina mali nyingi na kujibu hajui sio sumaye, ni mh. dr jakaya kiwete, msiwe mnapotosha umma
Refresh ur brain, sina muda wa kubishana na Mbululas, ndio maana hujui hata signature yangu ina maana gani!!
Mtu aliyepata division 4 point 29 inawezekana vipi leo awe na Masters ilihali hakuwahi kureset masomo? shirikisha ubongo wako kabla ya kubishana na akili kubwa utaishia kuumbuka na kupuuzwa mbulula.
Sumaye inaonekana anataka serikali 2 kwa kuwa anadai kama mungano wa sasa una matatizo yatatuliwe. Kwa mtazamo wangu hana hoja. Serikali mbili maana yake kwangu ni Tanganyika (TAN) na Zanzibar (ZNZ). Kwangu mimi mungano wa sSa umepitwa na wakati.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Ukiona mtu anatetea serikali mbili jua ni MNAFIKI na MZANDIKI!!! Jiulize kwa nini chako chako na changu chetu?
Huko CHADEMA aliko anaamini serikali ngapi? Ugeugeu na uchumiatumbo ni ugonjwa mbaya sana.Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.
chanzo: BBC
Angalizo: Nadhani ana hoja
Hilo la zenji kuwa mkoa au jimbo utaliotea ndotonihapa piga ua hatutaki serikali tatu ambayo ni mzigo kwetu tunataka serikali moja tu na zanzibar liwe mkoa au jimbo na siyo nchi.
SUMAYE huyu HUYU
du! comments za Enzi hizo Sumaye akiwa CCMAkili ya Sumaye ilishachoka siku nyingi, alishawahi kuhojiwa ni kwa nini Tanzania ni maskini akajibu hata yeye hajui ni kwa nini, imagine miaka 10 kama Waziri Mkuu hujui nchi ni kwa nini maskini ulikuwa unafanya nini kwenye hiyo nafasi?
Rasimu ya katiba mpya ni maoni yetu Wananchi yeye akafie Uyole kama anadhani hizi bado ni enzi za haambiliki.
aisee!wapo wachumia tumbo wanaona wamepata mbinyo wa maana. ukwel ni kwamba watz weng hawapend kufanya kaz, kujfunza nk.. sasa walitegemea mgongo wa aliyoko magogoni kuendesha familia.. mungu ni mwema sana, lazma tufanye kaz , Sio Kula juu ya migongo yetu. maana kuna maprofesa na madokta na mambumbumbu wanaoish kwa umbeya na fitna tu.,.. no longer at ease!!! huyu SUMAYE ana hak kusema ivo maana maslah yake( ndot za urais) yamekunwa!!
Kabisa...kwanini isiwe serikali moja?Nimemsikia Frederick Sumaye akisema Serikali tatu ni mzigo kwa Tanzania ambayo uchumi wake si mkubwa. Anasema hata waasisi wa Muungano waliliona hilo. Amezungumza akiwa Afrika Kusini.
chanzo: BBC
Angalizo: Nadhani ana hoja
Sijui alizingatia nini Lakini mimi ni mmoja wa wanaopinga serikali 2 na Tatu. Nataka serikali moja. Kama ASP na TANU ziliweza kuunda CCM kwanini naserikali za CCM zisiunde moja? Muungano alioutaka mwalimu ilikuwa kuunganisha nguvu ya mataifa machanga lakini sasa naona ni masilahi ya watu. Serikali moja itapunguza mzigo zaid kwa sababu kule Zanziba kutakuwa ni mikoa tu kama bara hivyo kutakuwa na makambi ya jeshe na secta zingine kama kawaida. Hakutakuwa na serikali ya mapinduzi inayobeba Baraza la wawakilishi, lakini pia msuguano wa nani awe Raisi kutoka upande gani haitakuwepo na viongozi hawatapata nafasi ya kuchochea vitu vingine kama tunavyoona sasa tofauti za mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. yapo mengi. Mimi napenda serikali moja.