SUMATRA zindukeni mtetee wanyonge wa nchi hii

H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,217
1,579
Nimejitolea kufanya utafiti mdogo wa nauli zinazotozwa na mabasi ya daladala katika baadhi ya njia za Jiji la Dar.

Nilichogundua ni kuwepo kwa nauli kutegemea maamuzi ama ya Dereva au kondokta
Nitatoa mfano wa barabara au njia mbili 1:Mbezi to Kawe na Mbezi to Makumbusho
2:Mbezi to Buguruni

Mabasi yaendayo Mbezi to Kawe kupitia Goba ambayo kurudi hupitia Moro Road haya nauli rasmi ambayo inatumika kwa mabasi yote

Mabasi yatokayo Makumbusho kupita Samn Nujoma hotoza nauli ya Tsh 400 mpaka Simu 2000 kituo chochote baada ya Simu 2000 hutoza tsh 500 mpaka kuishia Kimara na kituo chochote kuanzia Kimara hutoza tsh 600
Lakini yapo ambayo hutoza tsh 400 simu 2000 hadi Mbezi.
Sasa hapo abiria wako kwenye sintofahamu ya kujua nauli halali ni ipi na bahati mbaya website ya SUMTRA ambayo ungekuwa ya msaada bado ina taarifa za nauli za zamani.

Njia ya Makumbusho Goba Mbezi
Wao hutoza tsh 400 kwa abiria anayeshuka Mwenge, kituo chochote baada ya Mwenge hutozwa Tsh 500 hadi Goba na baada ya Goba ni Tshs 600 hadi Mbezi kwa abiria aliyeanzia Makumbusho na abiri wa njiani vivyo hivyo nauli ni kati ya mia 500 na mia 600 kutegemea kushika kabla au Mbezi.

Magari ya Mbezi Buguruni
Wao hutoza nauli ya 400 mpaka ubungo na kituo chochote kinachofuata baada ya ubungo ni Tsh 500.

Sasa basi kwa kuwa nimeshimdwa kuwasiliana nanyi kutumia anwani za kwenye website nikiamini hiyo website hamitumii tena kwa sababu ya kutokuwa na taarifa za karibuni hasa kuhusu nauli hivyo nimeona vema kutumia Jukwaa hili nikiamini mtatolea ufafanuzi wa hasa nauli za Dar es salaam kwa mujibu wa leseni za daladala ndani ya Jiji la Dar es Salaam ni zipi ili kupunguza ugomvi na malumbano baina ya Waendesghaji wa Usafiri wa daladala na baadhi ya abiria.

NB: Nimewahi kukuandikieni kuhusu nauli za UDART kati ya Mbezi na Kivukoni au Moroko pia Mbezi Gerezani.
Nikirejea mwongozo wa nauli ambao mmeuweka katika vituo vya Mwemdokasi inaonesha kuwa nauli kutoka Mbezi kwenda vituo tajwa, Moroko , Kivukoni na Gerezani ni Tsh 800 kwa MTU mzima

Na Tsh 200 kwa wanafunzi, lakini kinachoendelea kwa muda mrefu sana kwa sasa ni kwamba
watu wazima hutozwa tsh 1050 na wanafunzi hutozwa tsh 400.

Mimi napata kigugumizi kuamini kuwa SUMATRA hamlijui tatizo linalowakumba wananchi wa Mbezi kwa kipindi chote hicho au ukomo wenu wa utendaji kwa mabasi ya UDART unawazuia kusomamia nauli wanazotoza kiasi kwamba wanao Uhuru usio na mipaka katika kuamua mfumo wa ulipishaji wa nauli ?

Nategemea majibu ya wazi hapa hapa na kwenye njia zenu zingine.

Asanteni
 
Back
Top Bottom