mkonowapaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 1,492
- 772
Nalo neno.wakati mwengine unakuta hii ni mkakati wa kibiashara zaidi.
Yani lengo lao ni kuwachafulia jina lao (dar express) kibiashara kwa watu, ili watu wasiyaamini tena haya magari.
Mjini shule, SUMATRA kuhongwa na wamiliki wengine wa mabasi wafanye ivo hawashindwi.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesitisha safari za mabasi 14 ya kampuni za Dar Express kutoa huduma kati ya Dar es Salaam- Arusha na Arusha-Tanga kuanzia kesho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana, mamlaka hiyo kupitia kifungu namba 15 cha Sheria ya Sumatra namba 9 ya mwaka 2001, imeiagiza Kampuni ya Dar Express kusitisha utoaji huduma kwa magari yake yote yanayotoa huduma ya usafiri kati ya Dar - Arusha na Arusha- Tanga kuanzia kesho.
"Kutokana na kuwapo kwa matukio mengi ya ajali yaliyohusisha mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi 10, mamlaka inatilia mashaka sifa za madereva wa mabasi ya Kampuni ya Dar Express," inaeleza taarifa hiyo. Pia, taarifa hiyo ilieleza kuwa imebainika Kampuni ya Dar Express imekiuka Kanuni namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma kwa Magari ya Abiria za 2008.
"Kuanzia Januari 2011 hadi sasa, mabasi ya Kampuni ya Dar Express yamehusika katika matukio ya ajali maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo inatoa huduma za usafirishaji abiria. Matukio hayo ni kama lile la Januari 4, mwaka huu basi la Dar Express lilimgonga mpanda pikipiki na kusababisha kifo maeneo ya Kifaru- Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa taarifa za polisi chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi," ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa Septemba 22, mwaka huu, basi la Dar Express likitokea Arusha kwenda Tanga lilimgonga mtembea kwa miguu Ramadhani Hassan na kusababisha kifo eneo la Mkumbara - Mombo na Oktoba 24, basi jingine la kampuni hiyo liligonga gari jingine kwa nyuma kisha kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kitumbi - Korogwe. Katika ajali hiyo watu tisa walijeruhiwa.
Mwananchi
tuache kutetea maovu. kugonga mtu kwa gari ni kosa. sema sheria au kisu hiki cha sumatra kipite kwenye mabasi yote. air msae tangu apigwe chini amejirekebisha sasa hivi ndio metro check huduma zake kwenye basi lake la luxury. kuna mabasi ya njia nyingi mbali mbali hayafai hata kidogo. kila mtu anayesafiri anayajua sipendi kuyataja. kila week yanapata ajali na hata magazetini na kwenye tv hayatajwi mpaka eti basi liue watu wengi. ni mara ngapi umepata habari basi limekanyaga mpita njia mmoja kwenye magazeti au vyombo vya habari vyote. ? ni mara chache sana ila basi likiua watu wengi ndo inakuwa stori ya kuuzia gazeti au vyombo vyote vya habari. Watanzania tubadilike akifa mtu mmoja kwa kugongwa na gari mtasema alikuwa mlevi, oh mara wengine watasema alikuwa chizi wala hakuna mtu atakae mnyooshea dereva kidole. wakifa wengi unakuwa msiba wa kitaifa na mtaji wa kisiasa kwa watu wenginehivi huyu muzachai anaongea nini apo juu.........mi dar express ni usafiri wangu na wa wapenzi wengi wa safari zisizo na mashaka..masaa 9-10 barabarani!!mwendo mzuri/muda wa kuchuma dawa/lunch nzuri nz sina record yeyote seriuos ya mabasi haya achilia mbali siku hizi ajali za kaskazini zimepungua...........
kuna mkono wa sumatra hapa.si bure. yani hii nji hii nimeichoka.........kil akukicha ni visa dawa yenu ipo njiani anakuja nayo cameron
nauli zake haziendani na huduma wanazotoa. mfano kuna basi limepewa hadhi ya luxury na nauli ni shilingi 30,000 likiwa na maana ya full ac and tv. lakini ukilipanda neither tv nor ac. full vurugu. ticketi na namba ya basi ninayo kwa ushahidi hii ni fraud lakini watanzania huwa tunaona poa tu.
Nasikia kuna kampuni mpya ya yule kijana anapigiwa kelele na uvccm inaanzishwa. Pengine ndiyo mkakati sasa wa kuifungia Dar Express ili katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka watu watengeneze pesa! Dar Express imeleta mageuzi makubwa ktk makapuni ya usafirishaji abiria kanda ya kaskazini. Kwa kuiga mfano wa huduma nzuri na mabasi ya kisasa,kampuni nyingi zimebadilika sana na ajali za mabasi zimepungua sana ktk kanda ya kaskazini. Sasa kama imefungiwa,basi hakuna kampuni ya mabasi inafaa kusafirisha abiria ktk Tanzania.