SUMATRA wamejaa wezi, Mh. Rais tupia macho

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Tusaidie eneo hili linalogusa maisha maisha ya wanyonge wengi. Maafisa SUMATRA mikoa na wilaya wanafanya kazi kimazoea na hawataki kubadilika, wanafikiri bado tupo awamu ya wapiga dili. Wameacha kufuata kanuni za kukokotoa nauli wanatumia rushwa kupanga nauli kwa wenye mabasi wakati kanuni zipo wazi.

Utakuta mafuta yameshuka bei lakini nauli hazishuki na kama zinashuka basi sio proportionally. Wao hawafuati kanuni iliyopo, mfano serikali imeweka utaratibu njia za vumbi kilometa moja nauli iwe kati ya tsh. 40- 50 na njia za lami kilometa moja nauli iwe kati ya tsh. 25- 35.

Wao wanakula dili na wenye mabasi kipande cha lami cha km 100 abiria wanalipishwa hadi tsh. 4500-5000 huu ni wizi, wakati kipande hicho nauli halisi inatakiwa iwe 2500 hadi 3500 na abiria anabakiwa na sh. 1000 -1500 ambayo anaweza kununulia chumvi na kiberiti vya kufikia nyumbani.

Mh. kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya tusaidieni kuwatumbua maafisa SUMATRA taifa, mikoa na wilaya hili ni eneo linalogusa wanyonge wengi.

Mkurugenzi kama huyu wa SUMATRA akifukuzwa kazi si wakumlalamikia mtumbuaji ni dhahiri hafanyi kazi ya kuwafuatilia wa chini yake akajua uozo uliopo huku chini.
 
Akikulipisha hiyo 2500 unamsaidia kununua tairi,kulipia insurance, kuwalipa tigopesa barabarani? Mimi sidhan wanapaswa kutumbuliwa kwa kosa hill ila ni kulazimisha kupanga nauli na kukimbia ile misingi ya biashara ya demand and supply. Wakutumbuliwa in tanroads kwa kutokwenda na wakati. Leo hii matajiri wanaogopa kuleta magari mazur yenye injini nyuma kwa wasiwasi Wa kuzidi uzito minzani. Imagine unazuia kutoingiza basi 6*4 kwa vigezo ambavyo havieleweki. Tukitaka kuendelea ni sharti misingi ya biashara ifuatwe. Mfano Wa nauli za ndege hutegemeana na muda na wakati.
 
Umeandika vitu vingi ambavyo ni ngumu mtu kukuelewa, tulia uandike vizuri inawezekana una wazo zuri.
 
Back
Top Bottom