Sumatra wahurumieni abilia barabara ya Ubungo-Mwenge

Sumatra wahurumieni abilia barabara ya Ubungo-Mwenge

Mubhende

Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
40
Reaction score
6
Inapofika saa 12 asubuhi wasafiri wanaotumia barabara ya Mandela na Samnujoma kuja mwenge utawaonea hururma jinsi wanavyohangaika kupata usafiri.Abiria wanaounganisha kuja Mwenge kutoka maeneo ya gereji,external,mabibo hostel na riverside wamelazimika kutembea kutoka riverside hadi either Sim 2000 au Kivulini, kufuata daladala za kuja Mwenge. Kituo cha daladala za kutoka Buguruni na Mbezi kilichokuwa pale darajani kimehamishwa kwa makusudi ili kuwapa ulaji madereva Bajaj. Hapa kuna mtu ananufaika, haiwezekani kwa hali ya kawaida kufuta kituo halali na kuwaacha Bajaj wakitoza nauli kubwa kwa abiria bila Sumatra kuingilia kati! Huu ni wizi na uonevu kwa raia wanaotumia barabara hii. SUMATRA watwambie sababu za Kufunga vituo hivi na kuwaachia Bajaj, Je hawaoni kuwa watanzania wanateseka kwa kutembea umbali mrefu kutoka Riverside hadi Mawasiliano? Nasikitika sana nikiona raia wanavozagaa barabarani mida ya asubuhi eti kisa atatizo la usafiri
 
Kazi ipo pale kunasiku na mi nimetembea kinoma pale kuuliza wananiambia stend imehama duuh
 
Back
Top Bottom