SUMATRA Pwani nadhani mpo likizo

greater G

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
308
Reaction score
218
Kwa muda mrefu Wakazi wa Mkoani Pwani wamekuwa wakitozwa nauli zisizokuwa sahihi huku SUMATRA Mkoa wa Pwani mkiwepo.

Mfano ni Wilayani Kibiti, huku kulipokuwepo "watu wasiojulikana" nikiwa katika pita pita zangu za kusaka tonge nimebaini wamiliki wa magari na madereva wamekuwa wakitoza nauli ya tsh 1500/_ kwa umbali wa kilomita 16 kwa barabara ya kiwango cha Lami, wakati nauli halisi haitakiwi isizidi tsh 800/_

Nachojua Serikali imewapa vitendea kazi ili kuzungukia maeneo yote ya Mkoa huo kwa ajili ya kusimamia sheria zilizowekwa.

Ni vizuri mkatoka ofisi kwenye viyoyozi mkaja kusimamia haki.

Wananchi wenye kipato cha chini wanaumia.
 
nauli juu bei ya mafuta juu bei ya vipuri juu, iweje nauli pekeyake ndio ipunguzwe?
 
nauli juu bei ya mafuta juu bei ya vipuri juu, iweje nauli pekeyake ndio ipunguzwe?
 
Kuna kipindi niliwahi ona tangazo lao kwamba ikitokea abiria umekumbana na shida kama hii ni vema ukatoa taarifa kwa wasimamizi wa sheria ambao utakutana nao barabarani
Pia waweza toa taarifa kwa kutaja namba ya gari husika lililokutoza nauli hiyo ya juu ukiwa na ushahidi wa tiketi yako naamini watachukua hatua
Mimi ni shahidi kuna siku nikiwa mkoa fulani na abiria wenzangu tulitozwa nauli juu na tukafikisha lalamiko letu kwao lilifanyiwa kazi na tukafanikiwa kurudishiwa fedha zetu
Pia wana namba zao za kuripoti matukio ya aina hivyo kama vile
0800110019
0800110020
Piga bure bila malipo toa malalamiko yako watayafanyia kazi
Ni moja kati ya taasisi chache za serikali ambazo utendaji kazi wao ni mzuri na wakupigiwa mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…