SUMATRA, Mpinga, ina maana hamlioni hili?

soweto85

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
301
247
Habari wana JF,

Inasikitisha kila kukicha ni habari za ajali tu, inaumiza sana. Je, ule mpango wa kukaa na madereva wa magari makubwa ya mizigo na ya abiria kuongea nao uliishia wapi?

Mbona SUMATRA na kitengo cha askari wa usalama barabarani mnazunguka tu wakati issue ya kumaliza hili tatizo la ajali ni ninyi kukaa na madereva na wamiliki wa hivyo vyombo na kujadili kutafuta mwafaka wa tatizo badala ya kujaza adhabu kila uchao. Mnafikiri hiyo ndio solution? Mtu anapokoroga kila dizaini ya sumu mwishowe inamdhuru hata mkorogaji. Hivi hamjui kwamba tatizo kubwa liko kwa wamiliki wenyewe?

Madereva wameshalalamika mara ngapi kuhusu mazingira mabaya ya kazi lakini wahusika wanapiga danadana? Dereva apewe mkataba na mwajiri wake mwajiri anapoenda SUMATRA kusajirl gari yake kuanza route, anakua anatambulika na SUMATRA kwamba fulani ana gari fulani, hata linapotokea tatizo baada ya kulichunguza wanamchukulia hatua direct dereva, dereva ambae yuko ndani ya mkataba atafanya kazi kwa kujiamini na kuilinda gari pamoja na kuwa mwangalifu sana na hawezi kamwe kuendesha gari ambapo atagundua lina hitilafu hata kama mmiliki atamlazimisha afanye hivyo.

Je mnafahamu kwamba madereva wengi wanalazimishwa kuendesha gari hata kama amegundua gari ina hitilafu? Inabidi aende hivyo hivyo ili kulinda kibarua akigoma anashushwa na kupewa mwingine ambapo angekua na mkataba hali inakua tofauti.

Wenye magari ni viburi kupita maelezo, hulazimisha madereva kufanya kazi wanavyotaka wenyewe ikitokea ajali msala kwa dereva yeye ana bima kwa ajili ya gari yake madereva wanyonge kwa sababu ya tatizo la ajira.

Hekima inakosekana kwa wahusika wa upande wa pili adhabu zitawekwa mpaka zitaota manundu lakini ni bure endapo dereva hatajengewa mazingira ya kujiamini, kutokua na stress na kuithamini kazi yake.

MUNGU atubariki!
 
Back
Top Bottom