Habarini,
Kipindi cha ugonjwa wa corona kutokana na shule kufungwa na daladala kukatazwa kujaza abiria yaani iwe level seat. Serikali ilitoa ruhusa kwa ma bus binafsi hasa yale yaliyokuwa yanasafirisha wanafunzi nayo yafanye kazi za daladala na ikaelekeza waombe vibali SUMATRA, unaomba kibali na kama una vigezo basi unalipia unapata kibali cha miezi minne minne.
Ajabu sasa hivi vibali havijaisha wafanyakazi wa SUMATRA wanasimama barabarani na kuanza kukamata magari na kuomba rushwa au kutishia kuipelea gari yard.
Swali langu hivi kama hivi vibali vimesitishwa kwanini wasitangaze magazetini au radioni tukaelewa kama tulivyotangaziwa wakati tunapewa hivi vibali. Kumbuka hivi vibali tumevilipia. Au si waseme kama kibali kikiisha iwe basi hakuna ku-renew tena. Kuliko kukamata kimya kimya na kusumbua magari.
Mfanyabiashara anafanya biashara na analipa kodi hivi unapomsumbua unakuwa na lengo gani. Atalipa vipi kodi. Au kufanya biashara ni dhambi? Hawa ndio wanaofanya wananchi wawe na chuki na serikali yao.
Usafiri wa Dar miaka yote ni wa tabu yaani abiria ni wengi kuliko idadi ya magari.
Sioni sababu ya kukamata au kusumbua gari ambayo ina vibali vyote halali vya serikali.
Tafadhali tunaomba Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Pamoja na Takukuru wafuatilie hili. Na ikiwezekana hawa watu wachukuliwe hatua. Tupo tayari kuwataja.
Asante.