Nyamuhokwa
Member
- Feb 20, 2014
- 17
- 3
Raisi wa awamu ya tano ndugu John Pombe Magufuri, ameanza uongozi kwa kasi kubwa ambayo imefurahisha wananchi walio wengi. Ameanza kwa kubana ukwepaji kodi bandarini na sehemu nyingine chache. Lakini pamoja na jitihada zake, kuna baadhi ya taasisi zinamwangusha. Mfano mmoja wapo ni SUMATRA. Hawa ni kama hawajui majukumu yao. SUMATRA kazi yao ni kusimamia usafiri wa majini na nchi kavu. Kuhakikisha vyombo vya usafiri viko safi na salama. Na abiria wanapatiwa tiketi. Lakini cha ajabu suala la tiketi kwenye dala dala limesaulika kabisa. Makondakta kwa sasa hawatoi tiketi. Kitendo cha kutotoa tiketi kinachofanya na makondakta hao kinaikosesha serikari mapato makubwa. Chukulia mzunguko wa daladala nchi nzima je ni kiasi gani cha pesa kinapotea kwa siku, wiki, mwezi. Je SUMATRA Wanasubiri mpaka Raisi awakumbushe wajibu wao.