Leo nataka niwazungumzie SUMATRA katika suala zima la kukata vibali magari ya mizigo.
Kumekuwa na mtiririko wa kukamatwa barabarani kwa kupigwa faini kubwa sana ya sh 250,000 iwapo gari yako inayoanzia tani moja na nusu kama haina kibali cha sumatra, kazi ipo pale utakapoamua kukifuatilia hicho kibali ambapo kwa bei ni rahisi sana elfu 40 tu lakini kukipata kwake unaweza kupoteza zaidi ya laki mbili kwa usumbufu wa nenda rudi zaidi ya mwezi na nusu.
Cha kushangaza wamewaweka watu wao ambao ukimpa 150,000 tu kibali utaletewa ndani ya siku mbili au tatu,tunaamini wanachelewesha na kuwazungusha wahitaji makusudi ili vishoka wao wapate kugawana nao 150,000 wanazozipata kwa njia batili,tunawaomba wahusika wautambue mchezo huo mbaya unaofanywa unapotaka kukata vibali vya magari ya mizigo,watuambie jinsi gani unatakiwa ufuate utaratibu na ni siku ngapi kibali kinapatikana.