Suluhu pekee ni Reforms na kumuachia Lissu

Suluhu pekee ni Reforms na kumuachia Lissu

fasiliteta

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
2,598
Reaction score
4,471
Maana kwa sasa ni pamoto sana, Mama Samia muachie Lissu, fanya Reform na ingia kwenye uchaguzi bila kuogopa kitachotokea na ndiyo heshima kubwa utaiachia nchi hii.

Wananchi watakutetea sana, ila makada unaowaamini na umekaa nao ndio hao sasa kina slow slow wamezanza kutoka na wapo wengi mpaka wameanza kujiamini, mtu pekee atakusaidia kurudisha democracy ni Lissu na Chadema (SISI WANANCHI TUNAONA na SI WALE MATAPELI DHAMBARAU NA CHAUMMA UVAMIZI).

Ulianza vizuri sana na ulikua unaenda vizur sana ila mwaka mmoja huu sijui kimetokea nini! washauri pia kua nao makini maana mawe unatupiwa wewe wao wanapiga zao per diem's.

Mama Samia bado unanafasi kubwa sanaaaaaaaaa,Wanachi wapo radhi hata kusogeza mbele miaka 3 ili reform zifanyike.

Ni wazi uchaguzi huu ukifanyika utakua wa aibu kubwa tangu vyama vingi kuingia, tena hata enzi ya chama kimoja kulikua na afadhali.
 
Mama Samia wakati huu ndo wakati muafaka wa kuacha legacy yako.
Weka Reform,peleka mbele 3yrs za reform na katiba Kisha weka uchaguzi mkuu.
Hakika utakumbukwa Daima
 
Back
Top Bottom