Suluhisho la umeme kwa watanzania wote liko wazi: Vijijini na mijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suluhisho la umeme kwa watanzania wote liko wazi: Vijijini na mijini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nsimba, Apr 18, 2011.

 1. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni kweli kuwa kwenye mradi wa IPTL serikali inalipia tshs 152, 000, 000 kwa siku basi suluhishisho la kuwapatia wananchi wote wa tanzania umeme liko wazi-kama si ufisadi. Kwa msingi huo ni kuwa serikali inauwezo kifedha kuweka miundo mbinu ya kuweka umeme vijijini na mijini kwa watanzania wote takribani 43, 000,000 (tena umeme wa jua-clean energy).

  Nafikiri: kama tunalipa 152M kila siku ni sawa na ku-invest kiwango cha fedha kwa kila mtanzania cha kiasi Tshs 152M/43M kila siku: Yaani Tshs. 3.5M kwa kila mtanzania kwa siku moja tu. Kwa mwezi, hii ni sawa na ku-invest tshs 106M kwa kila mtanzania (3.5M x 30). Kwa msingi huo serikali inapoteza tshs 106M ya ku-invest kwa kila mtanzania kila mwezi, na kuwapatia mafisadi wachache through ITPL.

  SOLAR POWER inawaza kuwa suluhisho la kudumu la umeme tanzania kwa kutumia pato la ndani linalipwa IPTL. Kwa mfano, SOLAR PANEL ya watts 500 kwa kila kaya ya mtanzania hugharibu takribani tshs 1.65M (2.2 USD x 500 watts=usd 110-ona mchanganuo wa bei hapa: Hong Kong Solar Panel, Hong Kong Solar Panel Manufacturers, Hong Kong Solar Panel Suppliers and Companies on Alibaba.com )
  Hivyo, hata kama utaingiza usafiri haiwezi kuzidi 2M kwa kila panel, ikizingatiwa kuwa ushuru hautatozwa na serikali. Kwa msingi huo malipo yanayofanywa kwa IPTL ya siku moja (152M sawa na 3.5M kwa kila mtanzania), yanaweza kumpatia au kumuwekea miundo mbinu ya umeme SOLAR PANEL moja kila mtanzania ya tshs 2M yenye uwezo wa watts 500. Aidha, katika malipo hayo ya siku moja, fedha zitabaki kwa gawio la kila mtanzaia tshs 3.5M-2M=1.5M) kwa malipo haya yanayofanywa IPTL ya siku moja tu. Ikumbukwe hapa nimetoa mfano wa MRADI HUU wa SERIKALI wa kuweka PANEL moja ya watts 500 kwa kila mtanzania (lakini ikumbukwe kuwa hatuna kaya 43,000,000). Pengine twaweza kuewa na takribani kaya tufanye 20,000,000 (I guess). Hivyo MRADI huu waweza hata kugharibu kiwango kidogo cha fedha za nchi.


  Huu ni mfano mmoja tu miongoni mwa mifano mingi ambayo inaonesha jinsi taifa linavyoliwa na wachache na ukweli kuwa fedha za pato la taifa la Tanzania zikitumiwa vyema zinaweza kuibadilisha Tanzania kuwa kama London, New York, Beijing, Hong Kong, n.k. Tatizo kubwa ni jinsi ambavyo watawala msonge wamegeuza kutojua kwa watanzania kuwa mtaji wa kuwaibia na hivyo kuwafanya waamini kuwa umasikini wetu ni "MPANGO WA MUNGU". TAFAKARI, FIKIRI, na MWISHO--CHUKUA HATUA. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Late prof.nzali rip prof.aliyekuwa lecturer wa udsm electrical power engineering department and his fellow waliwaashaimbia serikali kwa proof ya tafiti umeme wa maji hauna tija waangalie vyanzo vingine kama upepo na jua serikali yako bishi haisikilizi mawazo ya wasomi ndo matokeo yake hayaaaa
   
 3. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Miradi 2 ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo upo uko Singida sijui kwa sasa umefikia kwenye hatua gani ambao mmoja ni wa Serikali na mwingine ni wa RA.
   
Loading...