talentboy
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 2,104
- 2,069
Habarini wadau wa jukwaa la celeb.
Leo imeamua kumleta kwenu kijana kutoka zanzibar, anaeitwa Sultan King, ni msanii wa miondoko ya bongo flavor/zenji flavor, huyu siwezi kusema ni underground la hashah, ila ni kijana mkali ambae alichelewa kuziona fursa zitokanazo na mziki mzuri anaoufanya, kwa kujikita zaidi katika soko la zenji tu bila kutanua wigo wa soko lake la mziki nje ya visiwani.
Kiukweli jamaa ana kipaji kikubwa sana cha kuimba na utunzi wa mashairi hasa wenye vionjo vya pwani (simaanishi taarabu), ni kule kupanda na kushuka kwa tenzi zake wakati akiimba. Na utunzi wake naufananisha kwa kiasi kikubwa na utunzi wa mkali CEO wa WCB diamondplatnumz, kwa mpangilio mzuri wa mizani na vina. Msikilize utajionea mwenyewe!
Kwa kuwa sasa hivi ndo ameamka kutoka usingizini ambapo alikuwa amelalia kipaji chake, na kuamua kufanya muziki serious basi naamini na tumuombee afanikiwe kwa sababu ana kila sababu ya kuwa msanii mkubwa kama au kuliko wale ambao kwa sasa wanahit, kama watoto wakali kutoka WCB, i.e, harmonize, rayvany, mavoko nk.
Kwa sasa kupitia uongozi wake Tausi Talents (TT) anajitahidi kuzipromote kazi zake hasa kwa upande wa Bongo ambako ndo soko la mziki limeshika khatamu. Na aminini nawaambia huyu dogo akipata upenyo kidogo tu atasumbua sana katika tasnia yetu pendwa ya Bongo flavor.
Wadau tukisapoti hiki kipaji kwa kila tuwezavyo ili kipaji chake kisife bure kwa kukosa sapoti. Kwa sasa ana hit na kibao chake kipya kinachoitwa Sitaki Lawama pamoja na Shikilia. Pia aliwahi kuhit na ngoma kama vile, Baby Hellow, Unanitosha ft mr. blue, Kiroho Safi, Mahari n.k. Zote hizo zinapatikana Youtube, lets support good music and true talent.