Sukari ya matumizi viwandani yauzwa majumbani

Plate Number

Member
Dec 1, 2014
19
9
Kikosi kazi kilichokuwa kinafanya ukaguzi wa sukari kwa wafanyabiashara wakubwa na wa rejareja jijini Tanga, kimebaini kuwapo kwa sukari nyeupe inayopaswa kutumika viwandani badala yake imekuwa ikiuzwa kwa wananchi kwa kutumika majumbani.

Sukari nyeupe hutumika viwandani kutengenezea bidhaa mbalimbali ikiwamo vilevi na vinywaji vinginevyo na haipaswi kutumika moja kwa moja majumbani kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE, Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Sukari nchini, Togolai Diliwa, alisema kuwa ukaguzi huo unafanyika kwenye maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi za serikali ikiwamo Shirika la Viwango nchini (TBS),Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Diliwa alisema serikali kupitia Bodi ya Sukari, imeamua kufanya ukaguzi kwa waingizaji wa bidhaa ya sukari ili kubaini ubora wa bidhaa hiyo kama inafaa kwa matumizi ya binadamu na mahali inapotoka kutokana na kuingia kwa wingi nchini, hatua iliyoathiri soko la wazalishaji wa ndani wa sukari.

Diliwa alisema kuwa katika ukaguzi huo, wanalazimika kuchukua sampuli za sukari kwenda kupimwa kwenye maabara mbalimbali hasa kwa kuzingatia kuwa kumekuwapo na sukari nyeupe nyingi sokoni ambayo ilipaswa kutumiwa zaidi viwandani.

"Katika ukaguzi wetu wa awali, sukari ambayo tumeikuta sokoni kwa maana ile ya soko la ndani, ni sukari ya TPC tu basi na mbaya zaidi tumeikuta pia sukari nyeupe inayotoka nje ya nchi ambayo hutakiwa kutumika viwandani…tumechukua sampuli na tunaamini baada ya zoezi zima kwisha ndiyo mwelekeo wa nini kifanyike utapatikana," alisema Diliwa.

Kuhusiana na namna sukari hiyo inavyoingia nchini alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiingiza kwa njia za panya na bandari bubu kwa lengo la kukwepa kodi, hivyo kuiuza kwa bei ya chini kuliko sukari inayozalishwa kwenye viwanda vya ndani.

"Kwa Tanga tu, tunafahamu zipo bandari bubu nyingi sana ambazo hutumika kupitisha bidhaa hii pia na kwa namna moja imeathiri soko la ndani kwani sukari ya nje inauzwa rahisi kuliko ya ndani," alifafanua.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wa rejareja wakizungumzia zoezi hilo walisema kuwa serikali inapaswa kuwabana kwanza waingizaji wakubwa wa sukari inayotoka nje pamoja na kudhibiti bandari bubu zilizopo ambazo hutumika kupitishia magendo yote na kukwepa kodi.

Nipashe!
 
Back
Top Bottom