Sukari sasa ni shilingi 2,400 kwa kilo huku Dodoma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Hii ndio bei ya sukari niliyokutana nayo katika duka moja leo asubuhi,duka ambalo lipo mtaa ulio karibu kabisa na Dodoma town center ambapo bei ni shilingi 2,400 kwa kilo katika duka hilo.

Bei hii sikuitarajia na ilinibidi kurudi nyumbani kuongeza fedha ili niweze kununua kilo kadhaa za sukari asubuhi ya leo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Tuendelee kupiga makofi na kuimba hapa kazi tu!
 
Hii ndio bei ya sukari niliyokutananayo katika duka moja asubuhi ya leo hapa mjini Dodoma.Mwenye duka ananiambia nae kakuta bei imepanda kwa mfuko mmoja wa kilo 25 kutoka shilingi 48,000 mpaka 51,000.

Tuendelee kupiga makofi!
 
Mbona huku musoma bado kilo ni 2000. Pia bei inategemeana wewe umeenda kununua wapi!! Shopping mall, au maduka yetu ya reja reja ya mtaani. Kama hizo bei ni za shopping mall hakuna shaka hapo mkuu. Maana ndo sehemu husika za mafisadi kupunguza pesa zao..!!
 
Mkuu, ni duka la reja reja la hapa mtaani.
 
Mbona huku musoma bado kilo ni 2000. Pia bei inategemeana wewe umeenda kununua wapi!! Shopping mall, au maduka yetu ya reja reja ya mtaani. Kama hizo bei ni za shopping mall hakuna shaka hapo mkuu. Maana ndo sehemu husika za mafisadi kupunguza pesa zao..!!

Kwanini hawauzi kwa bei ya 1800/= ? Maana hii ndio bei waliopangiwa hao wafanyabiashara.
 
Ile sukari ya nje iliyozuiwa kuagizwa ilikuwa inasaidia sana maana tulinuua hadi kilo sh 1600/- Sasa tunalinda viwanda vya ndani huku makabwela wakiumia. Sio mbaya tuendelee kununua tu kwa being hiyo. Wenzetu kule Zbar mfuko wa kilo 50 bei sh elfu 70.
 
yawezekana mm mwenyewe siku kabla ya jana nimenunua kwa 2000Tsh huku mtaani kwetu!!!!!
 
Hii ndio bei ya sukari hapa Dodoma mjini ambayo ni shilingi 2400 bei ambayo sikuitarajia na ilinibidi kurudi nyumbani kuongeza fedha ili niweze kununua kilo kadhaa za sukari asubuhi ya leo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Moderator naomba mbadili heading isomeke shilingi 2400 na sio 4200.

Tuendelee kupiga makofi!
Hapa kazi tu !
 
Shida kla mradi ulio na mkono wa kigogo jpm anautakatisha ndio maana tunaumia sukari ni elfu 2200 ad 2400 wakat bei eleke 1800 hilo halitekelezeki wafanya biashara wameigomea serikali kimtindo
 
Back
Top Bottom