suggestion Box

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Hamjambo?
Leo nimekikumbuka hiki kiboksi ambacho nilizoea kukiona sehemu mbalimbali ambazo zinatoa huduma, kama kwenye mabenki ofisi za serikali nk. Kwa ajili ya wateja kutoa maoni yao, kiboksi hiki huwa kimetengezwa kwa mbao, kimepigwa vanish halafu kina mlango/mfuniko uliofungwa kwa kufuli au vingine huwa na vitasa kama vile vya milango ya kabati.

Ingawa siku hizi sivioni sana viboksi hivi, bado kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba sikuwahi kuona siku wala mahala popote kisanduku hiki kikifunguliwa. Zaidi ni kwamba vyote nilivyoviona vilikuwa vimejaa vumbi mpaka kwenye matundu ya funguo. Je ni mimi tu mwenye mawazo haya? Au kuna mmoja wetu amewahi kufungua kisanduku hicho huko afanyako kazi?
 
Urembo tu, wangekua wanapokea maoni ya wateja/wageni wao na kuyafanyia kazi huduma zao zisingekua hovyo.
 
Urembo tu, wangekua wanapokea maoni ya wateja/wageni wao na kuyafanyia kazi huduma zao zisingekua hovyo.

Kuna kampuni palikua na manager wa kihindi, wafanyakazi wakaomba hilo box toka top management, likaletwa wakajaza maoni ndani ya siku mbili yule manager akaachia ngazi!
 
Kuna kampuni palikua na manager wa kihindi, wafanyakazi wakaomba hilo box toka top management, likaletwa wakajaza maoni ndani ya siku mbili yule manager akaachia ngazi!

Aliachia ngazi mwenyewe au alitemeshwa mzigo, hebu tuambie ili tujue kisanduku kilivyofanya kazi.
 
ingekuwa rahisi zaidi kama hao watu wangefungua website .. na watu watume maoni yao
through email au waache comment kwenye web.. siku zinavyoenda barua na vitu kama hivyo
vinazidi kupotea taratibu.. ( is just a suggestion )
 
Kuna maeneo wanaogopa kuweka kisa watu wataandika matusi. Vile ni muhimu sana. Kama ningekuwa boss sehemu ningeakikisha nakuwa na funguo mimi tu na suggestions zote ningekuwa nazisoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom