Sudan yawahukumu kifo wanajeshi waliowauwa waandamanaji

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,568
Sudan yawahukumu kifo wanajeshi 27 kwa kumuua mwandamaji

Mahakama moja ya Sudan imewahukumu adhabu ya kifo maafisa 27 wa vikosi vya usalama kwa kumtesa na kumuua mwandamanaji mmoja wakati wa maandamano ya kumpinga aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir

Kifo cha mwandamanaji Ahmed al-Khair, aliyekuwa mwalimu wa shule, wakati alipokuwa kizuizini mwezi Februari kilikuwa suala muhimu na ishara katika maandamano hayo ambayo hatimaye yalisababisha jeshi kumuondoa Al-Bashir madarakani.

Hukumu za leo, ambazo zinaweza kukatiwa rufaa, ndizo za kwanza kuhusiana na mauaji ya waandamanaji katika mapinduzi hayo.

Hukumu ya leo katika kesi dhidi ya vikosi vya usalama ilitolewa katika mahakama ya Omdurman, mji ndugu wa Khartoum, ambako waandamanaji kadhaa walikusanyika nje ya mahakama, wakidai haki kwa ajili ya Al-Khair.

Al-Khair alikamatwa Januari 31 katika mkoa wa mashariki wa Kassala na akaripotiwa kufariki siku mbili baadaye. Mwili wake ilipelekwa kwenye hospitali ya eneo hilo ambako familia yake ilisema ulikuwa na michubuko. Kwa wakati huo, polisi ilikanusha kufanya kosa lolote ikisema kifo chake kilitokana na ugonjwa, bila kutoa maelezo yoyote.

51834501_303.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom