Sudan: Viongozi kadhaa akiwemo Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok wadaiwa kukamatwa. Jeshi lavunja Utawala wa Kiraia

Bashiri ndo alifukuzwa...then serikali ya mpito...alaf tena Jeshi....Tusubirie Guinea nako

Kumbuka Omar Al Bashir alikuwa mjeda na alipindua serikali ya Sadiq Al Mahdi
Yaani hapo Jeshi linalipa fadhila kwa mjeda mwenzao
Wanajeshi wanajuana sana labda kama wakishindwa kukubaliana kwa mambo kadhaa ila wanabebana sana
 
Si mlisema kupinduana kunaleta maendeleo,endeleeni sasa na mapinduzi mpate maendeleo..

Wanajeshi kupindua serikali ni upuuzi wa Hali ya Juu , maendeleo hayawezi kupatikana kwa mtindo wa kishenzi kama huu.
 
Bashiri ndo alifukuzwa...then serikali ya mpito...alaf tena Jeshi....Tusubirie Guinea nako
Kaulize Guinea sasa ambako wanajeshi walipindua serikali,je wananchi Washapata maendeleo au nafuu ya maisha?

Ni mara mia Kuwa na utawala was kiraia ambao mambo yakienda mama unaweza hata kuandakana au kuwakoromea nk lakini sio wanajeshi,ukifanya fyatu wanaua hakuna mtetezi..

Wanaotakaga wanajeshi wapindue serikali basi wahamie hizo nchi Ili wakafaidi maendeleo.Duniani kote tawala za kijisehi ziko pembeni maana hakuna wanachoweza kufanya chenye tija ya maendeleo..
 
Sasa unakuta majengo ya serikali hawawezi kuyafikia kirahisi maana yanalindwa.By the way hakuna kitu wataharibu afu kisijengwe tena kwa hiyo hakuna namna..

So Bora wanachoma lami je wangefanya kama South Africa ingekuaje?
 
Mbona ulaya na amerika hakuna upuuzi huu wa mapinduzi ya kijinga? Kule ukisikia mapinduzi ni ya viwanda na kilimo, hakuna upuuzi kama huu wa nchi za kiafrika kupinduana wenyewe kwa wenyewe
Shida moja Afrika watawala hawatendei wananchi haki na pia hawafuati katiba inavyosema. Shida nyingine ni kupenda madaraka. Wanajeshi kwa vile wana nguvu na kama wakitofautiana na mtawala, wanamwondoa tu madarakani.
Kama kungekuwa na chaguzi huru Afrika pengine haya yangepungua au yasingetokea sana. Baadi ya nchi kama Kenya, South Afrika, Botswana, Malawi, Ghana, Nigeria na zinginezo ambazo uchaguzi unakuwa huru angalau wanajeshi siyo rahisi kupindua nchi. Wenzetu wazungu wameshapita huko lakini na sisi tuko njiani tutafika tu siku moja.
 
Mbona ulaya na amerika hakuna upuuzi huu wa mapinduzi ya kijinga? Kule ukisikia mapinduzi ni ya viwanda na kilimo, hakuna upuuzi kama huu wa nchi za kiafrika kupinduana wenyewe kwa wenyewe
Hizo nchi zilishapita hii stage ambayo nchi zetu zinapitia sasa hivi.Democrasia ya USA haikuja hivi hivi kwa lelemama. Kuna baadhi ya Marais mpaka walishawai kuuwawa ndo unaona saiv watu wanaheshimiana
 
Duniani kote tawala za kijisehi ziko pembeni maana hakuna wanachoweza kufanya chenye tija ya maendeleo..
Statement nzuri ilifaa kuwa asilimia kubwa, Kwa sababu kuna wanajeshi wamezifanyia nchi zao makubwa Tu pamoja na ukatili wao.

General Park Chung hee aliitoa Korea Kusini kuwa nchi masikini mpaka kuwa nchi yenye uchumi imara kitu ambacho watawala waliochaguliwa kidemokrasia walishindwa.

Park Chung hee aliingia kimapinduzi 1961 na baadae kuuwawa Kwa kupigwa risasi 1979.

Kanali Muamal gadafi, mpaka mwaka 2010 kabla ya gadafi kuuwawa Libya ilikuwa ndio yenye pato la juu kuliko nchi yoyote afrika, Libya ilikuwa na Hali mbaya wakati WA utawala WA kifalme Kwa sababu mafuta yalikuwa yanachimbwa na kampuni toka nchi za nje.

General Chieng Kai shek WA jamhuri ya China(Taiwan), baada ya kufeli China bara Kai shek aliweza kuigeuza Taiwan kuwa nchi iliyoendelea na mzalishaji mkubwa duniani WA vifaa vya kiielektroniki hasa chips.

Japokuwa wanajeshi wengi ni majanga sana hasa huku afrika anzia Mobutu, Samuel doe, Museven, Kabila, Bihari na abacha, Al Bashir, Campaore na mwenzie Sankara, Idris debi, hosni Mubarak yaani listi ni ndefu. Ila kuna baadhi walitawala Kwa kufuata mipango sahihi kuinua uchumi.
 
Nashindwa kuelewa sudani iligawanywa ikawa sudani kusini na sudani kaskazini. Hii yenye mapinduzi ni ipi?
 
Abdel Fattah Burhan alikuwa anamaliza muda wake wa kuongoza baraza la kijeshi.

Uchaguzi umepangwa kufanyika 2023 na Burhan aona hiyo ni safari ndefu sana na madaraka ni matamu.

Ni jambo lililo wazi kuwa jeshi la Sudan haliko tayari kuwa chini ya serikali ya kiraia.

Burhan anafahamu fika kuwa nchi za Misri na Imirati zipo nyuma yake na mpaka sasa nchi hizo hazijatoa tamko la kulaani kitendo cha mapinduzi ya kijeshi.

Nyuma ya Burhan yupo mjeda mwingine aitwa Mohammed Hamdan Dagalo ambae ni kamanda wa kikosi saidizi Rapid Support Force ambae ndie alieunda kikosi cha Janjaweed kilichokuwa kikifadhiliwa na Al-Bashir kwenye mgogoro wa Darfur.

Hawa wajamaa wa RSF ndo walomkamata waziri mkuu bwana Hamdok na ndo wanoendesha operesheni za kuwakamata viongozi wenginewe na ndo tuwaonao mitaani wakifanya doria.

Ukizungumzia uhalifu wa kivita RSF hawakosekani.

Sidhani kama Sudan watapata serikali ya kiraia hivi karibuni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…