Sudan: Viongozi kadhaa akiwemo Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok wadaiwa kukamatwa. Jeshi lavunja Utawala wa Kiraia

Bashiri ndo alifukuzwa...then serikali ya mpito...alaf tena Jeshi....Tusubirie Guinea nako

Kumbuka Omar Al Bashir alikuwa mjeda na alipindua serikali ya Sadiq Al Mahdi
Yaani hapo Jeshi linalipa fadhila kwa mjeda mwenzao
Wanajeshi wanajuana sana labda kama wakishindwa kukubaliana kwa mambo kadhaa ila wanabebana sana
 
Kwa mujibu wa Kituo cha Al-Hadath TV, Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Abdallah Hamdok amewekwa katika kifungo cha nyumbani huku Viongozi kadhaa wa Utawala wa Kiraia wakikamatwa

Hali Nchini humo imekuwa tete tangu kushindwa kwa jaribio la kufanya Mapinduzi Mwezi Septemba. Kukamatwa kwa watu hao kumekuja wakati kuna mvutano kati ya Jeshi na Mamlaka ya Kiraia

Pia, kuna Ripoti zinazodai huduma ya intaneti ipo chini katika Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum

UPDATE: JESHI LAVUNJA UTAWALA WA KIRAIA

Jeshi la Sudan limevunja Utawala wa Kiraia, limewakamata Viongozi wa Kisiasa na kutangaza Hali ya Dharura. Waandamanaji wameonekana Barabara Mjini Khartoum, na kuna ripoti za risasi kufyatuliwa

Kumekuwa na mvutano kati ya Viongozi wa Kijeshi na Kiraia tangu Mtawala wa muda mrefu wa Nchi hiyo, Omar al-Bashir alipopinduliwa miaka miwili iliyopita

=======

Military forces in Sudan have put Prime Minister Abdallah Hamdok under house arrest and arrested several members of the country’s civilian leadership, according to Al-Hadath TV.

The Dubai-based broadcaster, citing unidentified sources, said a military force besieged the prime minister’s home early on Monday before placing him under house arrest.

It said those taken into custody include Industry Minister Ibrahim al-Sheikh, Information Minister Hamza Baloul, and media adviser to the prime minister, Faisal Mohammed Saleh.

The spokesman for Sudan’s ruling sovereign council, Mohammed al-Fiky Suliman, and the governor of Sudan’s capital Khartoum, Ayman Khalid, were also arrested.

The Associated Press said Sudanese officials who spoke to the news agency on the condition of anonymity confirmed the arrests.

Sudan has been on edge since a failed coup plot last month unleashed bitter recriminations between military and civilian groups meant to be sharing power following the toppling of the country’s long time leader Omar al-Bashir.

Al-Bashir was toppled after months of street protests in 2019, and a political transition agreed after his removal was meant to lead to elections by the end of 2023.

Al Jazeera’s Hiba Morgan, reporting from Khartoum, said “telecommunications access has been restricted” in the country “so it’s very hard to communicate with people here”.

“The military has also blocked all roads and bridges leading into Khartoum city. We’ve seen soldiers blocking access and they are telling us these are the orders they got. They are saying access to Khartoum city is to be restricted, and this is raising concern because that’s where the government institutions are, that’s where the presidential palace and the prime minister’s offices are located.”

There was no immediate comment from the military, with Sudanese state television broadcasting patriotic songs. But Al Hadath said Abel Fattah al-Burhan, the head of the Sudan sovereign council, was soon expected to make a statement on Monday’s developments.

Meanwhile, the Sudanese Professional’s Association, the country’s main pro-democratic political group, called the military’s moves an apparent military coup and called on the public to take to the streets.

“We urge the masses to go out on the streets and occupy them, close all roads with barricades, stage a general labour strike, and not to cooperate with the putschists and use civil disobedience to confront them,” the group said in a statement.

Last week, tens of thousands of Sudanese marched in several cities to back the full transfer of power to civilians, and to counter a rival days-long sit-in outside the presidential palace in Khartoum demanding a return to “military rule”.

Hamdok has previously described the splits in the transitional government as the “worst and most dangerous crisis” facing the transition.

More soon …

Source: Al Jazeera
Si mlisema kupinduana kunaleta maendeleo,endeleeni sasa na mapinduzi mpate maendeleo..

Wanajeshi kupindua serikali ni upuuzi wa Hali ya Juu , maendeleo hayawezi kupatikana kwa mtindo wa kishenzi kama huu.
 
Bashiri ndo alifukuzwa...then serikali ya mpito...alaf tena Jeshi....Tusubirie Guinea nako
Kaulize Guinea sasa ambako wanajeshi walipindua serikali,je wananchi Washapata maendeleo au nafuu ya maisha?

Ni mara mia Kuwa na utawala was kiraia ambao mambo yakienda mama unaweza hata kuandakana au kuwakoromea nk lakini sio wanajeshi,ukifanya fyatu wanaua hakuna mtetezi..

Wanaotakaga wanajeshi wapindue serikali basi wahamie hizo nchi Ili wakafaidi maendeleo.Duniani kote tawala za kijisehi ziko pembeni maana hakuna wanachoweza kufanya chenye tija ya maendeleo..
 
Yaani huwa nashangaa sana wanapotuma ujumbe kwa kuchoma matairi kwenye Lami waliojenga kwa jasho lao

Baadae tena hela zinawatoka tena kodi maradufu na bidhaa kupanda bei ila yote hayo hawayaoni

Kundamana bila kuunguza lami na kuchoma majengo inawezekana
Sasa unakuta majengo ya serikali hawawezi kuyafikia kirahisi maana yanalindwa.By the way hakuna kitu wataharibu afu kisijengwe tena kwa hiyo hakuna namna..

So Bora wanachoma lami je wangefanya kama South Africa ingekuaje?
 
Mbona ulaya na amerika hakuna upuuzi huu wa mapinduzi ya kijinga? Kule ukisikia mapinduzi ni ya viwanda na kilimo, hakuna upuuzi kama huu wa nchi za kiafrika kupinduana wenyewe kwa wenyewe
Shida moja Afrika watawala hawatendei wananchi haki na pia hawafuati katiba inavyosema. Shida nyingine ni kupenda madaraka. Wanajeshi kwa vile wana nguvu na kama wakitofautiana na mtawala, wanamwondoa tu madarakani.
Kama kungekuwa na chaguzi huru Afrika pengine haya yangepungua au yasingetokea sana. Baadi ya nchi kama Kenya, South Afrika, Botswana, Malawi, Ghana, Nigeria na zinginezo ambazo uchaguzi unakuwa huru angalau wanajeshi siyo rahisi kupindua nchi. Wenzetu wazungu wameshapita huko lakini na sisi tuko njiani tutafika tu siku moja.
 
Mbona ulaya na amerika hakuna upuuzi huu wa mapinduzi ya kijinga? Kule ukisikia mapinduzi ni ya viwanda na kilimo, hakuna upuuzi kama huu wa nchi za kiafrika kupinduana wenyewe kwa wenyewe
Hizo nchi zilishapita hii stage ambayo nchi zetu zinapitia sasa hivi.Democrasia ya USA haikuja hivi hivi kwa lelemama. Kuna baadhi ya Marais mpaka walishawai kuuwawa ndo unaona saiv watu wanaheshimiana
 
Duniani kote tawala za kijisehi ziko pembeni maana hakuna wanachoweza kufanya chenye tija ya maendeleo..
Statement nzuri ilifaa kuwa asilimia kubwa, Kwa sababu kuna wanajeshi wamezifanyia nchi zao makubwa Tu pamoja na ukatili wao.

General Park Chung hee aliitoa Korea Kusini kuwa nchi masikini mpaka kuwa nchi yenye uchumi imara kitu ambacho watawala waliochaguliwa kidemokrasia walishindwa.

Park Chung hee aliingia kimapinduzi 1961 na baadae kuuwawa Kwa kupigwa risasi 1979.

Kanali Muamal gadafi, mpaka mwaka 2010 kabla ya gadafi kuuwawa Libya ilikuwa ndio yenye pato la juu kuliko nchi yoyote afrika, Libya ilikuwa na Hali mbaya wakati WA utawala WA kifalme Kwa sababu mafuta yalikuwa yanachimbwa na kampuni toka nchi za nje.

General Chieng Kai shek WA jamhuri ya China(Taiwan), baada ya kufeli China bara Kai shek aliweza kuigeuza Taiwan kuwa nchi iliyoendelea na mzalishaji mkubwa duniani WA vifaa vya kiielektroniki hasa chips.

Japokuwa wanajeshi wengi ni majanga sana hasa huku afrika anzia Mobutu, Samuel doe, Museven, Kabila, Bihari na abacha, Al Bashir, Campaore na mwenzie Sankara, Idris debi, hosni Mubarak yaani listi ni ndefu. Ila kuna baadhi walitawala Kwa kufuata mipango sahihi kuinua uchumi.
 
Nashindwa kuelewa sudani iligawanywa ikawa sudani kusini na sudani kaskazini. Hii yenye mapinduzi ni ipi?
 
Abdel Fattah Burhan alikuwa anamaliza muda wake wa kuongoza baraza la kijeshi.

Uchaguzi umepangwa kufanyika 2023 na Burhan aona hiyo ni safari ndefu sana na madaraka ni matamu.

Ni jambo lililo wazi kuwa jeshi la Sudan haliko tayari kuwa chini ya serikali ya kiraia.

Burhan anafahamu fika kuwa nchi za Misri na Imirati zipo nyuma yake na mpaka sasa nchi hizo hazijatoa tamko la kulaani kitendo cha mapinduzi ya kijeshi.

Nyuma ya Burhan yupo mjeda mwingine aitwa Mohammed Hamdan Dagalo ambae ni kamanda wa kikosi saidizi Rapid Support Force ambae ndie alieunda kikosi cha Janjaweed kilichokuwa kikifadhiliwa na Al-Bashir kwenye mgogoro wa Darfur.

Hawa wajamaa wa RSF ndo walomkamata waziri mkuu bwana Hamdok na ndo wanoendesha operesheni za kuwakamata viongozi wenginewe na ndo tuwaonao mitaani wakifanya doria.

Ukizungumzia uhalifu wa kivita RSF hawakosekani.

Sidhani kama Sudan watapata serikali ya kiraia hivi karibuni.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom