Sucess factor | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sucess factor

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Msamiati, Sep 4, 2012.

 1. Msamiati

  Msamiati R I P

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 1,076
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 0
  UNATAKA NINI KWENYE BISHARA?
  Kwa upande wangu mimi kuna vitu viwili naviona kwenye maisha ya biashara,
  Kwanza ni ufanyaji biashara kwa lengo la kufanya maisha yaendelee kuwepo
  Pili ni kufanya biashara kwa nia ya kuleta mabadiliko kwenye maisha

  Watu ambao wanafanya biashara kwa nia yakufanya maisha yaendelee kuwepo ni wale ambao biashara zao zipo kwa lengo la kuendeleza usalama wa maisha yao na familia zao, Best Goal kwao ni kuhakikisha Basic needs kwenye familia zinakuwepo muda wote, yaani familia inapata chakula, inapata malazi, Matibabu, Nauli na ada za watoto, mavazi, pamojaa na huduma kwa watu wengine wanao wategemea
  Hawa huwa wanakuwa na malengo madogo madogo ambayo huyaweka kwa kipindi kifupi cha siku tatu mpaka tano, Huwa wanakuwa ni watu wenye kuridhika kwasababu hawapati tabu kwenye kutimiza malengo yao siku zote biashara yake hupigania mahitaji yake ya kila siku na kuyatimiza bila shida. Mara nyingi mtu wa namna hii Huamini kuwa mabo makubwa yanayo fanywa na watu wengine kama Bakhresa Mengi na wengineo ni Bahati ya mtu, Kiuhalisia ni kwamba watu hawa wameona haiwezekani kufikia malengo makubwa, wamekata tama wanafikilia walipoishia, Na kauli ya kishujaa “To Give Up does not show you are weak, But you are strong enough to leave it for others” imewakaa kichwani masaa 24.

  Lakini kwenye jamii hii hii, Dunia hii hii wapo watu ambao wao Tafsiri ya Biashara kwao ni ya tofauti, Wenyewe hushughulika zaidi na kuleta mabadiliko kwenye maisha na jamii.

  Maisha kwao si kula kulala au kuvaa bali ni Mabadiliko gani yaliyoletwa na biashara yake, Picha aliyo nayo ni kuona kuwa mafanikio ambayo yamefikiwa na watu kama Usuph Manji au Mwanamziki Diamond ni Jambo dogo sana kwake na mara zote huwa na ndoto za kufanya mambo makubwa zaidi Ndani ya miaka michache ijayo.
  Huku akiwa na imani kuwa kama wengine wameweza Basi yeye hana sababu ya kushindwa

  HUYU NDIE MTU MWENYE MTIZAMO WA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA

  Kama mtu ana maelezo yoyote yanayoweza kusaidia kuchochea mafanikio kwenye maisha ya biashara asisite kushare na mimi hapa

  WELLCOME !
   
Loading...