Subramaniam bado Work Permit

Enzi

New Member
Apr 21, 2011
4
0
Subramaniam aendelea na Kazi pamoja na kuwa na expired work Permit

Naona mchezo mchafu unafanywa kuhusu suala la uhalali wa aliyekuwa Meneja Mkuu wa Fedha wa kampuni ya IPTL, Dk. Magesvaran Subramaniam, raia wa Malaysia.

Ninanavyofahamu baada ya kumaliza mkataba wake wa ajira IPTL, na kukabidhi ofisi kwa uongozi, kibali chake cha kuishi nchini kilimalizika na hivyo kutakiwa kuondolewa nchini baada ya kulipwa haki zake zote alizostahili.

Uamuzi huo ulizingatia muda wa mkataba wa ajira yake ambao ni wa miaka miwili kuanzia Februar mosi 2009. Kibali chake cha kuishi nchini chenye Na. 079388 kilicholipiwa Dola 700 za Marekani kilimalizika muda Februari 19, 2011.

Inashangaza kuona hajaondoka na inavyoonekana, anahangaika kutafuta kubaki nchini kwa vyovyote. Ushahidi wa hilo ni kuendelea kila siku kufika IPTL na kufanya kazi.

Upo wasiwasi kwamba analindwa na kwa kuwa sasa inaendeshwa kwa utaratibu wa "ufilisi mahsusi" chini ya Wakala wa Usajili na Ufilisi (RITA) inayoongozwa na Phili Saliboko.

Zipo fununu jwamba kuna jitihada za kumpatia kibali kipya cha kufanya kazi nchini hatua ambayo ni kinyume na sheria ya Uhamiaji. Mgeni yeyote akimaliza muda wa kibali chake cha awali, anapaswa kuondoka nchini ndipo aanze utaratibu wa kupata kibali kingine. Hastahili. Nchi yetu ina wataalamu wengi wa masuala ya fedha.

Suala lake linahitaji kufuatiliwa na vyombo husika ikianzia na Idara ya Uhamiaji yenyewe, na Usalama wa Taifa. Ufuatiliaji uanze haraka chini ya usimamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ili kuzuia mbinu chafu.

Mfanyakazi Mzalendo
Independent Power Tanzania
Limite (IPTL)
Dar es Salaam

Source:
MwanaHalisi April 20, 2011
 
Siku njema, niliona jukwaa mada na haina inaonekana ya wafanyakazi au wafanyakazi wa aliandika barua hiyo na mwana hails kama wafanyakazi si kujua idadi ya kibali. Hii ni lazima baadhi ya mtu ambaye tu kujaribu kutu jina ya watu. nchi yetu ni maelewano na sisi welcome kila mtu kufanya kazi. Hivyo basi, mtu anayehusika kutatua suala hilo na siyo kuchukua gazeti kama faida kwa jina baadhi kutu ndio Mungu awabariki. !!!!!
 
Siku njema, niliona jukwaa mada na haina inaonekana ya wafanyakazi au wafanyakazi wa aliandika barua hiyo na mwana hails kama wafanyakazi si kujua idadi ya kibali. Hii ni lazima baadhi ya mtu ambaye tu kujaribu kutu jina ya watu. nchi yetu ni maelewano na sisi welcome kila mtu kufanya kazi. Hivyo basi, mtu anayehusika kutatua suala hilo na siyo kuchukua gazeti kama faida kwa jina baadhi kutu ndio Mungu awabariki. !!!!!

Duh mazee sijakuelewa hata moja hapo,unaweza kuedit na kufafanua unataka kutuambia nini,au wewe ndio Mr Subramaniam,swahili lugha gongana??
 
Haha, wewe! Sasa mimi kuwa mtu kwamba sijui labda ya ngono tofauti ... Nini!! Mimi ni mtu wa kidemokrasia sana! Anyway ambaye wasiwasi kwa ajili yake .... Hebu kuwa na furaha ... oldies ......
 
Back
Top Bottom