Submita kata Umeme

Submita kata Umeme

Kinaongeza matumizi kwenye main meter.Matumizi baada ya kukifunga yanapanda.
Ni Cha kijinga sana .
Wait....mie natumia main, halafu hicho nimewaachia wapangaji wanakishea watu watatu, ila wanalalamika matumizi yameongezeka.

Ni kweli kitakua kinawaongezea matumizi ya umeme?

Na kuna namna kinakata umeme? Niliweka 5.5 ikasoma 5.0 hizo point tano zilienda wapi sasa.
 
Hizi zinafanyaje kazi? au ndiyo kama hizi hizi zilizopo sokoni ambazo zinafanya counting tu ya matumizi ya umeme?
Asante sana kwa swali lako. Submita unatumia umeme kulingana pesa yako. Na ukimaliza umeme wako submita itakukatia Umeme yenyewe more 0757 838927
 
Raha ya hiki ki mita ufunge viwili. Kimoja kwa Ajili yako na kingine kwa Ajili ya wengine. Wakimalize watalala giza wenyewe. Bei ya 110,000. Karibu
0757 838927
Ukifunga viwili inaleta tofauti gani? Iwapo kikiwa kimoja mfano room mbili watumie sub meter room mbili watumie mita ya tanesco, italeta tofauti ipi kuongeza sub meter?
 
Hii mita nzuri sana ukiwa unaishi na watu ambao wanazingua kununua umeme....

Nlipata frem mahali, umeme ni wa kushea vyumba vya wapangaji na frem za biashara, changamoto inakuja umeme umekata mpangaji hayupo au yupo anakujibu hana hela.

Mi nikafunga haka kadude, kwahiyo umeme wao ukiisha unazima kwao mi wangu upo.

Changamoto yake....
1: umeme lazma uingize token kwenye mita ya tanesco kisha unascan msg kwenye app ya simu ili kupata token nyingine umeme uhame (usumbufu)
2: kuna siku waliweka umeme unit 5.5 ila hiki kimita ikasomeka 5.0 sasa hiyo 0.5 sijui ilipotelea wapi

All in all nakapenda mie kameniondolea kelele japo hawakataki make walikua wamezoea kitonga nawanunulia

Kwa hiyo ulifunga pekeyako wengine wakaendelea kutumia mita kuu?

Vipi mfano wote wasinunue kisha wewe ukanunua kwa ajili ya submeter yako ukajaza kwenye mainmeter na kuhamisha kwenye submeter, je huoni umeme kwenye main meter utawaka kwa watu wote bure?
 
Kwa hiyo ulifunga pekeyako wengine wakaendelea kutumia mita kuu?

Vipi mfano wote wasinunue kisha wewe ukanunua kwa ajili ya submeter yako ukajaza kwenye mainmeter na kuhamisha kwenye submeter, je huoni umeme kwenye main meter utawaka kwa watu wote bure?
Hizi submeter na zenyewe naona ufanisi bado majanga tu.....nliamua kuipiga kikono na kununua mita kubwa tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom