Juzi nilikuwa na tsh. 100000/= kwenye mfuko wa shati nataka mbolea ya kupandia beans baada ya mvua kuanza kunyesha. Nikamtuma boda wangu aende anunue kwenye maduka ya pembejeo.
Akaambiwa kwa sasa hawaruhusiwi kuuza. Anauza tu wakala. Wilaya nzima yupo Wakala mmoja, ili upate mbolea lazima uwe ulijiandikisha na umepata sms.Nikafanya makeke nikapata namba kutoka kwa bodaboda. Hawa wamejiandikisha sana Ila hawana mashamba. Mziki ni hii foleni Sasa.
Imebidi nipande tu Bila mbolea.
Kwa akili yangu kwete, nilidhani wangeacha maduka ya pembejeo wauze Ila bei ndiyo waiwekee kikomoo.
Au sisi ambao tupo tayari kununua hata kwa bei yoyote watuache tununue tunakojua kuliko hivi tunakosa mbolea wakati hela tunazo mfukoni