Tunaye muabudu wooote ni mungu mmoja basi dini ni kitu gani basi mbela za haki? Ndoa hufungishwa na mungu ila mungu hamchagulii mwanadamu mke au mume kwani ukiangalia alimchagulia adam mke na matokeo yake adam akamlaumu mungu kwa kumpa mke.....sasa ieleweke kuwa mungu ametupa nafasi ya kuchagua tukisha chagua yeye anabariki......matatizo katika ndoa yapo hata kwa wale waliopo katika dini moja.....mfano uliotolewa hapa wa mbuzi na ng'ombe hauna uhalisia wowote ule naomba utafutwe mfano mwingine......
I agree we all believe in one God but we don't believe in the same God.
Katika ndoa imani ina role sana wala hatuwezi kukataa, Kama wanandoa mnakua na dini moja inakua rahisi sana katika malezi ya watoto.
Tunajua kwamba chanzo ta taifa bora ni familia zilizo imara, chanzo cha kanisa bora ni familia zilizo bora na chanzo cha msikiti bora ni familia zilizo imara, huu ni ukweli ambao haupingiki. Mara nyingi tunasema watoto ni taifa la kesho lakini tunashindwa kuweka msingi imara kwa taifa hili.
Imani yenu ikiwa moja, inasaidia sana kuleta umoja na mshikamano katika malezi ya watoto.
Hili ni muhimu sana kwani mara watoto wanakua na reference moja wakijua nini kifanywe na nini kisifanywe. Dini zinapotofautiana watoto wanabaki kuchanganyikiwa kwa sababu baba anakua anakataza hili wakati mama analiruhusu or viceversa. Mchanganyiko huu hauwajengi watoto bali unakua unaleta shida na matokeo yake ni watoto wasio kua na msimamo katika dini yeyote.
Wengine wanasema watoto wengine watakua na dini moja na wengine nyingine. Hivi motto mmoja anapotoka madrasa na mwingine ametoka Sunday School inakuaje, kinaeleweka kweli katika hiyo nyumba? Watoto wanavyozidi kukua watakuja na maswali mengi tu sasa wanapokua na maswali kuhusu dini mnawajibu nini?
Just Imagine mkristo Mlokole na mwislamu wanaoana, hivi wanakaaje katika hiyo ndoa? Mwislamu anapotaka kuchoma Ubani na Kuzikiri, Huyu mkristo au Mlokole anakua amekaa wapi saa hizo, na Mlokole anapotaka kuimba pambio na kuomba mwislamu anakua amekaa wapi saa hizo. Haya siku Mkristo akipata hamu ya kutafuna kiti moto inakuaje katika hiyo nyumba? (Ingawa sio kitu muhimu sana kwa sababu anaweza kuacha kula kwa sababu ya ndoa).
Hivi vitu kwa kweli haviwezi kuchangamana kabisa, sijui Quran inasemaje katika hili lakini Biblia iko wazi na dhahiri kwamba Sahihi kufunga nira na mtu asieamini.
Unless nyie wanandoa ni watu msiojali habariza dini, Lakini ndoa za dini tofauti hazifai kwa malezi bora ya watoto.
Don't go into marriage just to satisfy yourself, think beyond that , think about the family you want to build, think about the legacy you want to leave behind. The decision is I your hand you can choose and make the right decision. Lakini kwa wale ambao tayari wako kwenye ndoa hizo mseto basi hakuna cha kufanya inabidi uendelee nayo ila kwa wale ambao hawajaingia, Please think twice.