Suala la Hospitali ya CCBRT linasikitisha sana!!!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
865
(1)Kuanzia Mwaka 2012 Serikali iliipandisha Hospital hiyo hadhi na kuatangaza kuwa itakuwa Mwaajiri wa wafanyakazi

(2)Kuanzia hapo ikaanza kulipa mishahara kwa kuwapatia kila mfanyakazi Check yake na mshahara wake.Sambamba na hilo Malipo ya NSSF yana onyesha kuwa Muajiri ni Hazina ila kiwango kinachokatwa ni tofauti na mishahara wanayopata wafanyakazi.

(3)Wafanyakazi kadha wakaenda hazina na kupewa nakala za Chekizao na kubaini kuwa Hazina imekuwa inatuma Checki hizo CCBRT lakini Mwanamke anayeitwa Emelda Luena na Bi Aika wanachoma moto cheki hizo ili Wafanyakazi wasigundue.

(4)Baadhi ya wafanyakazi wakaenda mahakamani na hapo ni utawala wa Kikwete lakini sasa CEO ambaye anaitwa Erwin Telemana akawatuma akina Emelda na Aika kuhakikisha Wafanyakazi wote waliofungua kesi hiyo wanatafutiwa mizengwe na kufukuzwa.

Hivi sasa kuna mfanyakazi ameitwa jana kufukuzwa na suala hilo limesukwa na Emelda Luena.

(5)Hazina walipogundua mgogoro huo waliamua kuwaomba CCBRT kupeleka majina HAJINA na Wafanyakazi wote ili pesa za Mishahara ziingie moja kwa moja kwenye akaunt zao lakini CEO wa CCBRT akagoma hadi sasa na ikabaika kuwa tayari kulikuwa na watumishi hewa hapo na zaidi ta Tshs. 300 Bils zimetafunwa na Wazungu.

(6) Kuna Mtanzania alikuwa anatoa huduma ya chakula hapo amefukuzwa na kuletwa Mzungu ambaye ni ndugu wa CEO Telimani.

(7)Wafanyakazi hapo wanatukanwa matusi ya Wanyama na mzungu huyo wanadai haki zao.

Maswali Yangu:

(1)Ni kwa nini Serikali ya Magufuli imefumbua macho suala hilo wakati kuna watumishi hewa na Hazina wamesitisha mishahara.

(2)Kwa nini wafanyakazi waibiwe mishahara ambayo ni haki yao na ni kodi zetu??

(3)Kwa nini mahakama inasua sua kuhukumu kesi hiyo.

(4)Kwa nini wafanyakazi ambayo muajiri wake ni serikali wanafukuzwa na mzungu bila kujulisha serikali???

(5)Kwa nini Mzawa amenyang'anywa tenda na kupewa mzungu ambayo anapika chakula ambacho wafanyakazi hawataki?

(6)Kwa nini Suala la CCBRT ambayo ipo eneo jirani na Vyombo vya dolo halichukuliwi hatua wakati maeneo mengine kuna kasi kubwa??
 
Kwani Dr. Slaa hana tena mkono wake pale? Dr. Slaa rudi utatue hii changamoto, nakumbuka kuna Kipindi ilikuwa ni tegemeo kubwa kwa watanzania wengi na JK alishawahi kuzindua kitu fulani. Lakini sasa ndo mambo yenyewe yalivyo? Hapo ndo nachoka na wabongo maana ishu kama hiyo ni sensitive kiasi cha intelligence unit ingekuwa tayari ina report ya kutosha. Ni mzungu kweli kazipiga au ilikuwa sehemu ya kukusanyia pesa za uchaguzi?
 
Hapa si kuna wakati kuliibuka Tiffu la Kumng"oa Dr Slaa mpaka Jk akaingilia kati?
Na hii Serekali ni Vp ilipe Mishahara ktk Hospital hizi za Binafsi..
Wao hawana huduma kwa wasio na uwezo zaidi ya Kupiga tuu
 
Kuna vitu havipo sawa kwenye madai haya. Kwa uzoefu wangu haya ni majungu. Kama una mkataba na unajua mshahara wako kama makato ya NSSF yanaenda pungufu unaweza kuwasilisha malalamiko NSSF. Pamoja na uzembe wa NSSF lakini hili lilipaswa kuwa na sura hiyo na si majungu ya check kuchomwa moto wakati haina faida yoyote kuminya haki za wafanyakazi. Serikali kutaka kuweka mshahara direct ndio ingeondoa tatizo la makato ya NSSF? Tenda ya kupikia staff sidhani ni issue ya kuleta mitandaoni kulalamika, hicho chakula mnalipa au mnalipiwa na ofisi? Jengeni base ya malalamiko yenu badala ya kutajataja majina ya watu kimajungu tu. Tafuteni watu wenye akili wawasaidie kuainisha matatizo yenu na haki zenu kisheria badala ya hizi hadithi za Shigongo.
 
ingawa tunaweza tusijue kwa undani suala LA CCBRT,lakini ni kweli kabisa watumishi wengi hawajui kuwasilisha hoja zao kwa ufasaha.
Utakuwa watumishi wanajambo la msingi kabisa,lakini wanashindwa kuliwasilisha kwa ufasaha,mwisho wa siku unakuta wanajichanganya na hoja yao ya msingi kufa.
Mfano mzuri ni hoja ya mleta mada,kunaweza kukawa na jambo LA msingi apo ccrbt ,lakini ukisoma kwa makini katikati ya mistari utaona majungu ndani yake dhidi ya baadhi ya watumishi.
 
Hivi umiliki wa CCBRT ukoje wandugu maana mara serikali, mara binafsi, mara mpinzani wa enzi hizo Dr. Slaa ndani, mara JK anataka weka kitu sawa pale.... hivo.... mwenye kujua tafadhali. ...
 
Kila kona ni utapeli, mpaka kwenye maswala muhimu kama afya za watu. Sizani kama tutafika !!
 
Kuna dada mmoja pale ni mlemavu, bingwa wa kula rushwa hadi basi hasa kwa wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa operation ya macho
 
Kuna vitu havipo sawa kwenye madai haya. Kwa uzoefu wangu haya ni majungu. Kama una mkataba na unajua mshahara wako kama makato ya NSSF yanaenda pungufu unaweza kuwasilisha malalamiko NSSF. Pamoja na uzembe wa NSSF lakini hili lilipaswa kuwa na sura hiyo na si majungu ya check kuchomwa moto wakati haina faida yoyote kuminya haki za wafanyakazi. Serikali kutaka kuweka mshahara direct ndio ingeondoa tatizo la makato ya NSSF? Tenda ya kupikia staff sidhani ni issue ya kuleta mitandaoni kulalamika, hicho chakula mnalipa au mnalipiwa na ofisi? Jengeni base ya malalamiko yenu badala ya kutajataja majina ya watu kimajungu tu. Tafuteni watu wenye akili wawasaidie kuainisha matatizo yenu na haki zenu kisheria badala ya hizi hadithi za Shigongo.
Kwa mfano mtoa mada anasema wafanyakazi walioajiriwa na serikali wanatimuliwa na CCBRT; Inakuwaje mtu unafukuzwa na taasisi ambayo haijakuajiri??
 
Back
Top Bottom