Suala la ACACIA funzo kubwa kwa wabunge wa CCM

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,163
1,308
Tanzania yetu ni nchi ya neema sana, sababu tumejaliwa na utajiri mkubwa wa rasilimali . Mpaka sasa Watanzania hatujanufaika na rasilimali zetu , Hatujanufaika sababu ya watu wachache kutanguliza maslahi yao binafsi au ya kichama zaidi.

Tumeshuhudia mikataba kama vile ya madini ya gesi kila ikipelekwa bungeni ,wabunge wa tawala huwa wanapitisha sheria mbali mbali bila kufikiria masuala ya Taifa zima kwa ujumla . Wengi wao huwa wanatishwa au wanoagopa kuitwa wasaliti pindi wanapoenda kinyume na viongozi wa serikali yao.

Kwa lolote lile analifanyo RAIS Magufuli lenye madhara kwa Taifa utaona linafurahiwa sana wakati suala hilo lingeweze kutatuliwa miaka 15 au 20 iliyopita. Ni wakati wabunge wa CCM wakatanguliza maslahi ya Taifa kwanza halafu chama baadae . Hivi leo tungekuwa kwenye dunia nyingine na kuachana na kuwa omba omba
 
Hawa hawasikii, bado wanadumisha fikra za mwalimu,
Huyu jamaa alishayajua haya
 
Attachments

  • VID-20170526-WA0002.mp4
    4.9 MB · Views: 49
Si nyinyi ndio mlikuwa mnashangilia wakati Trump aliposema afrika itawaliwe tena directly.
 
Ukishakuwa ndani ya CCM huna tena mamlaka na AKILI au UTASHI wako...

Maamuzi mengi ambayo wamekuwa wakiyafanya collectively especially wabunge wao kupitia vikao vya Party Caucus ni maamuzi ya KIJINGA hata mtoto hawezi kuyafanya.

Mfano Zitto alivyoibua issue ya Buzwagi badala wajadili anachokisema wakamfukuza na kumfumgia kuhudhuria vikao vya bunge. Badae ukweli ukajulikana that Zitto was right.

Angalia juzi uchaguzi wa EACL.. Wabunge wa Afrika Mashariki walivyowafanyia Chadema.
Yani kwao kupata wabunge bora kwa ajili ya Nchi isn't an issue..!!

Ukoo wa Mapanya.
 
Hao jamaa hawawezi kimujifunza kitu chochote kwa cheap kauli kama ya kwako. Nini kilitokea kuhusu radar? Ndege? Escrow? Kama wanaweza kupitisha sheria ya ajabu ya habari kwa buku ten itakuwa hii?
 
BARRICK / ACASIA for years wamekuwa wakigharamia chaguzi za maccm ... jiulize kwanini? kinachoendelea ni zaidi ya kiini macho! Mungu amtangulie JPM ...
Tanzania yetu ni nchi ya neema sana, sababu tumejaliwa na utajiri mkubwa wa rasilimali . Mpaka sasa Watanzania hatujanufaika na rasilimali zetu , Hatujanufaika sababu ya watu wachache kutanguliza maslahi yao binafsi au ya kichama zaidi.

Tumeshuhudia mikataba kama vile ya madini ya gesi kila ikipelekwa bungeni ,wabunge wa tawala huwa wanapitisha sheria mbali mbali bila kufikiria masuala ya Taifa zima kwa ujumla . Wengi wao huwa wanatishwa au wanoagopa kuitwa wasaliti pindi wanapoenda kinyume na viongozi wa serikali yao.

Kwa lolote lile analifanyo RAIS Magufuli lenye madhara kwa Taifa utaona linafurahiwa sana wakati suala hilo lingeweze kutatuliwa miaka 15 au 20 iliyopita. Ni wakati wabunge wa CCM wakatanguliza maslahi ya Taifa kwanza halafu chama baadae . Hivi leo tungekuwa kwenye dunia nyingine na kuachana na kuwa omba omba
 
Suruhisho ni katiba mpya. Mfano kile kipengele mbunge akivuliwa uanachama na chama chake abaki na ubunge wake, ingeondoa uoga wa wabunge kuwa na fikra huru. Kwa sasa wabunge wa ccm wameshikiwa akili na chama
 
Hakuna kumbukumbu zzt zile zinazoonesha kwamba huyu aliyeko madarakani aliwahi kukataa kushiriki upitishwaji wa sheria na miswada mibovu - kwa sasa anaonekana shujaa vilevile kama walivyomuona shujaa Mkapa na Kikwete na kampani zao akina Chenge wakati wanapitisha haya yanayoonekana leo mabaya. Sijui akili huwa zinawatoroka ,ccm ni janga aiseeeee
 
Hii kasumba ya wabunge wa CCM Anasimama na kusema napongeza serikali na napongeza hili na lile pia napongeza blah blah blah halafu anakaa chini
Yaani hatoi. Mawazo mbadala ni u...........
 
Fikiria Zitto Kabwe aliwahi fukuzwa bungeni baada ya kusema Karamagi alikwenda kusaini mkataba hotelinni UK. Leo mi-CCM inasema eti siyo mzalendo. Tundu Lissu hadi alifunguliwa kesi eti kwa sababu anawatetea wananchi waliokuwa wana nyanyaswa na serikali kuwafukuza kutoka maeneo yao ya kuishi ili wapishe wezi wachukue dhahabu??

CCM ni janga na ndo imetufikisha hapa. Kama JPM anania ya dhati na nchi hii basi aanze na kubadiri sheria na hapa aanze na rasimu ya pili ya jaji Warioba.
 
ukishakuwa mbunge wa ccm jua ww ni mbunge wa chama. utaunga mkono hata pumba ilimradi zimeletwa na ccm. binafsi siwezitumikia wananchi wangu kwa uhuru nikiwa mbunge kupitia ccm
 
Yameharibu kwa ndiyooo leo eti yanataka tuwe kitu kimoja kwa maslahi ya taifa!!!hv nikisema hawa watu hawajitambui nitakosea? Isemeni kweli hata mauti yanazama kwa ujinga leo yanataka wote tukazame umeona wp?shem.
 
kwa mienendo hii inaonesha kabisa nchi huwa inaendeshwa na mawazo ya mtu mmoja (rais) nasema hivyo kwa sababu kama ingekua inaendeshwa na angalau chama,haya yote yasingekuwepo,check mawazo ya mzee aliepo sasa hv mfano angeonesha kupinga wakat ule wa kupiga makofi tu,naamini asingekua peke yake,ila kwa sababu wabunge woooote si wa upinzani wa tawala huwa wako recessive kwa rais,na hii itatugharimu vby sana na tayar imetugharimu,check nape alisimamia kidete kuzima live bunge hayakua mawazo wala matakwa yake,leo anajuta karma is a bitch

my take: rais jpm nampongeza lau kwa kuliibua hili hadharani na kuonesha nia njema kwa taifa lakini angeweka upinzani pembeni akaomba ushauri kwa kina lisu na wengine wataalam ili atembee safely kisheria
na kubwa zaidi kama kweli ana uchungu na nchi hii Katiba iletwe ile ya warioba na kuiboresha zaidi,tunataka nchi iende mbele kwa vitendo si mateno tu.
 
Back
Top Bottom