Stuka, kila mke/mume ofisini ana bebe wake

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Niende moja kwa moja kwa mada inayosema stuka, kila mke na mume ana bebe wake ofisini.

Narudia tena stuka, kuna baadhi ya wake au waume za watu ila kwa ofisi wana bebe kule, huyo anachukua nafasi ya wa nyumbani Tena kwa kujali zaidi.

Huwezi elewa yaani wanakuwa na ukaribu Fulani ambao wanaweza kuchambua karanga wote kwa pamoja.

Picha linaanza pale anapoingia asubuhi mke au mume anakaribishwa na tabasamu matata na mfanyakazi mwenzie.

Wengine wanaenda mbali zaidi kwa kulumbatiana na kukisi.

Njoo sasa ule muda wa chai yaani wanakaa pamoja, wanaandaliana chai, hapo kumbuka vitafunwa mkeo/mumeo alishambinilia mwenzie.

Utamu unaanzia pale chai inanywea kwa mapozi mbalimbali, ambayo hata nyumbani unaweza usiyapate hahaaa...

Mchana wapo tena pamoja, yaani hapa mkeo au mumeo anapelekwa kwenye mgahawa wanakaa pamoja kwa furaha na kula chakula kwa pamoja.

Haitoshi jioni wanaotoka kazini Tena pamoja wanasimdikizana yaani ni wanamahaba mvua kuliko ya nyumbani.

Bado Kuna vile vizawadi vidogodogo kama pipi, biscuit, Ice cream ambazo analetewa mkeo pale kwa job na dume mwenzako.

Bado akirudi nyumbani wanachat kwa WhatApp yaaani ni mahaba tele..

Stuka, mkeo au mumeo ana bebe wake wa kazini ambaye anamjali kulio wewe...



Donatila
 
Hii kitu ni mtego sana.

Unajua mume/mke mfanyakazi anatumia muda mwingi na mfanyakazi mwenzake kuliko mwenza wake nyumbani

Hii inaleta ukaribu sana na mfanyakazi mwenzake wa jinsia tofauti kifuatacho ni kunyanduana

Ninafanya kazi na wake za watu, kikweli wengi huwa wakija kazini na stress za ndoa zao lazima wataanza kutafuta mahali pa kueleza hisia zao na kuomba ushauri mara nyingi ni kwa wafanyakazi wenzao wanaume.

Basi mambo huanza na ushauri mpaka kumlala, hapo sijazungumzia safari za kikazi. Ndoa ni utapeli wakuu

Golden rule;
Never date a co-worker
 
Back
Top Bottom