Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,133
- 48,851
We unatukana walimu walionifundisha mimi ni mbumbumbu, maku konyo wee!!
NA WEWE NI MWALIMUWALIMU WETU NA ELIMU KUANZIA OKTOBA
06,2016
Binafsi sikutaka kabisa kuzungumzia suala la
walimu wa mafunzo /Field wakiongozwa na Frank
Msigwa kumtesa mwanafunz Sebastian katika shule
ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya(Mbeya Day)....
Watu mbalimbali wakiwepo walimu na marafiki
zangu kunitaka kuzungumzia jambo hili. Lakini Pia
katika makundi ya whatasaap ya Chadema,
makundi ya walimu ya whatasaap na hata Facebook
nimona Mawazo ya watu mbalimbali wengine
wakiunga mkono adhabu hiyo na kutetea walimu
kwamba ni halali adhabu hiyo kali na walimu
wameonewa kufukuzwa vyuo.
Wengine wameonekana kukerwa Sana na adhabu
hiyo ya kikatili kwa mwanafunzi na wengine
wameeleza kwamba kama Sebastian angekua
mwana wao wangewamaliza walimu Katika kundi
hili Walimu wametukanwa kila aina ya tusi ikiwa ni
Pamoja na kuitwa "MSHETANI" "HAWAIJUI LEBA /
CHUMBA CHA KUJIFUNGULIA", "MAJAMBAZI ", "
WAUAJI "," ****** WALIOFELI ", na matusi
mengine mengi Sana ya aibu mengine yakiwa ya
nguoni......
Baada ya kujiridhisha Maoni ya watu wa pande mbili
nimegundua kwamba kwa sasa elimu yetu
itaonekana upya na itaanza upya katika suala la
uhusiano wa walimu, wanafunzi na wazazi......
Walimu wameonesha kueleza kwamba wameonewa
Sana kupewa adhabu ya kufutwa vyuo na
kufunguliwa mashtaka. Walimu wanadai, madaktari
wamefanya operation na kusahu nyembe katika
mwili, wamesahahu sindano au vitu vingine lakini
hawajafukuzwa Kazi nk. Wamehoji mateso
aliyoyapata mwananchi mmoja Huko Mlowo Mbozi
kwa udhururaji kwa kipigo cha mbwa mwizi na
Polisi na kufariki hali iliyopelekea wananchi
kuandamana kukataa kuzika. Madhaifu ya wazi na
sirini yamejitokeza katika taaluma za uhandisi, jeshi
la polisi, Udaktari nk. Lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa dhidi yao. Ghorofa lililoanguka na
kuua watanzania Dar Es Salaam mwaka 2012 na
2013 mpaka leo hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi
ya wahandisi...
Nimeona walimu wameamua kuanzisha uhusiano
mpya Ili kulinda vibarua vyao. Walimu wanasema
kwamba kuanzia sasa Kazi ya mwalimu itakua ni
kufundisha tu.
Walimu wengi wanasema kwamba mwanafunzi aje
shule asije hatafuatiliwa. Mwanafunzi avute bangi
asivute hakuna wa kujihusisha naye. Mwanafunzi
akiwa na uhusiano wa kimapenzi asiwe na uhusiano
hakuna kumfuatilia. Mwalimu akitoa Kazi
mwanafunzi afanye asifanye hakuna wa kumfuatilia.
Mwanafunzi alewe asilewe hakuna wa kumfuatilia.
Mwanafunzi achelewe shule, atukane walimu,
wanafunzi wagombane, wanafunzi wakifanya
chochote wataachwa huru...
Mwalimu atafundisha na kuondoka. Hakuna adhabu
yoyote kwa mwanafunzi yeyote labda mwanafunzi
akipata mimba au kuacha shule mwenyewe lakini
walimu watajiondoa kuwa walezi /wazazi wa
wanafunzi. Hii ni kuepusha uhasama wa wanafunzi
na wazazi wao dhidi ya walimu. Walimu Kazi
wanayosema wamebaki nayo ni kufundisha tu,
Basi.... Mengine ni Kazi ya mzazi.
Uhusiano huu wa wazazi na wanafunzi dhidi ya
Walimu utawapa uhuru usio na mipaka wanafunzi
(Student's unlimited freedom) na matokeo yake
yanakuja....
Wazazi, walimu, wanafunzi na serikali tujiandaye
kupokea matunda na matokeo ya uhusiano huu
mpya wa STUDENT'S UNLIMITED FREEDOM.
Kama unakubali Mwl ni mlezi basi usipinge watoto wetu kuchapwa, lazima wachapwe maana hata wakirudi kwangu wajapofanya makosa lazima niwachape, sijalazimisha Mwl awe mlez naomba uelewe hiloKama mwalimu ni mlezi nikwa utashi wake,halipwi ili alee bali aelekeze. Sasa kama wakati anaelekeza kukitokea mambo yanayohitaji kuwa mlezi awe makini isimtokee puani.
Hapa naona umuhimu wa Serikali kukaa na kusort na Waalimu.Serikali na jamii mkae mkijua sisi walimu ni wanafiki sana! msifikiri tunavyowachekea ndo tumekubali tuuuu tunafanyaga action ambayo impact yake itaonekana miaka kadhaaa, hebu ona form form four wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika ila darasa la saba wana B+, Msicheze na walimu nyie
Mtapata dhambi mkifanya hivyoNmeipenda hyo walimu timizeni jukumu ambalo watu weng wanadhani mwalimu kaz take ni kufundsha tu. Tuone kizazi kitakachotokea
Huo ushenzi uko wapi?
Ni lini umesikia suala la ajabu ajabu limetokea shule binafsi?
Tatizo lenu walimu wa serikali mnafanya kazi kwa mazoea
Ulifundishwa jinsi yakulea na ukafaulu au ni utashi wako binafsi. Nikikushitaki kwa kumchapa mtoto nakumsababishia maumivu utatumia nini kujitetea?Kama unakubali Mwl ni mlezi basi usipinge watoto wetu kuchapwa, lazima wachapwe maana hata wakirudi kwangu wajapofanya makosa lazima niwachape, sijalazimisha Mwl awe mlez naomba uelewe hilo
Mtapata dhambi mkifanya hivyo
Bora dhambi watatubu kuliko dhambi wanayoipata kwa kuziakiwa kuitwa majina yacyokuwa na nafasi katika jamiiMtapata dhambi mkifanya hivyo
Kweli Dunia imepotoka, basi tuishie hapa mkuu " mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio"Ulifundishwa jinsi yakulea na ukafaulu au ni utashi wako binafsi. Nikikushitaki kwa kumchapa mtoto nakumsababishia maumivu utatumia nini kujitetea?
Fundisha na fanya yote yanakuhusu ktk kazi yako,suala lakujifanya polisi,mahakama na magereza achia wahusika wanaopewa mamlaka hayo na sheria za nchi. The best you can do kama mzazi anatoa ushirikiano mshilikishe yeye mwenyewe atoe hukumu.Kweli Dunia imepotoka, basi tuishie hapa mkuu " mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio"
We uliejiuliza hebu tupe majibu, si ushasema ni mambumbumbu sasa mbumbumbu unategemea awaze nini?Walimu mnazidi kujidhihirisha jinsi gani mlivyo mambumbu hasa walimu wa shule za serikali. Kwanini tukio kama lile haliwezi kutokea kwenye shule binafsi?
Kwanini mambo ya ajabu tu yanatokea kwenye shule za serikali?
Hivi amuwezi kujiuliza ni kwanini yanatokea shule za serikali tu?
Alafu unajifanya unajua kiswahili, vingine muwe mnakaa kimya tu.Sasa wewe ni mwalimu wa kiswahili halafu unaandika utumbo huko kwenye blue,wewe kuitwa MBUMBUMBU itakuwa ni sahihi tu.
Kwaiyo umenijumuisha kuwa Mwl. Unachanganyikiwa wewe mimi binafsi ruksa Mwl kuwa mlez kwa watoto wangu, kwa maana muda niutumiao mimi na watoto si sawa na ule autumiao Mwl kwa wanangu hivyo mimi ni mzazi yeye ni mlez wangu na ana mamlaka yote ya kufanya vile ambavyo mimi ningemfanya mwanangu Mara baada ya kugundua amepotokaFundisha na fanya yote yanakuhusu ktk kazi yako,suala lakujifanya polisi,mahakama na magereza achia wahusika wanaopewa mamlaka hayo na sheria za nchi. The best you can do kama mzazi anatoa ushirikiano mshilikishe yeye mwenyewe atoe hukumu.
Kwel kabsa,tena hii nchi huwa haioni faida ya walimu kabsa,kuna sku walishasema hata wakgoma anaweza ajiriwa wengne waliomaliza form tena kwa muda mfupiSerikali ya Tanzania hajawahi kuwahitaji walimu kwa umuhimu unaoutaja hapa
S.U.FSTUDENT'S UNLIMITED FREEDOM imekaa poa sana