Wadau wa MMU, Heshima kwenu
Kwa mara nyingine nimeamua kuwashirikisha hili.
Niliwahi ku post thread kuhusu binti niliyempenda sana Leah,
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/215780-niko-njiapanda-sijielewi-jamani.html,
Aliniacha na kunifanya niteseke sana.Maisha yangu yalikua ya hovyo mno tangu mwaka 2009 -2010 nilivoachana nae.Nimebadili wanawake sana nikidhani naweza tii kiu ya penzi la dhati la mtu ninaempenda lakini imekuwa sivyo.Pia niliwahi kuweka uzi huu
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/251439-nimebanwa-sasahivi-two-girls-in-my-home.html,
hii ni moja kati ya mapito niliyokua napitia.Ki ufupi nilikua na tabia mbaya (Umalaya/Call it uhuni) kwa kubadili sana wanawake.
Lakini katika kipindi chote hicho Leah hajawahi kutoka akilini na moyoni mwangu pamoja na kujitahidi sana kumsahau na kujitahidi kumpenda binti niliyekua naye.
Hivi karibuni kwa muda wa miezi minne iliyopita hadi sasa Leah amerudi kwangu,amerudi akidai kuwa hakuwa anahisi kunipenda kwa kipindi kile tulipokua pamoja ati alikua anajitahidi tu.Baada ya kupitia maisha mengine na boyfriend wake ametambua kwamba she belongs to me,ameamua kurudi innocently na anaomba nimuoe.
Kilichonishangaza kidogo alipokua na boyfriend wake huyo hawakuweza ku sex na alibaki kuwa bikira (She is 23 now).Na mimi nimefanikiwa kuwa mwanaume wake wa kwanza just two weeks ago.
Wadau hapa nahitaji ushauri wenu kwamba huyu msichana naweza kuendelea nae hasa ukizingatia jinsi alivoniacha mwanzo na kunitesa vile? Naona kama ana roho ya kinyama sana.Wadau,ninyi mnazo experiences mbalimbali naomba mnisaidie katika hili.
Thanks