STRANDED!msaada tafadhali

Neno nalo

Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
67
Reaction score
54
Mimi ni msichana wa miaka 25.miaka minne iliyopita nlikutana na kijana flani nkiwa chuo,tukatokea kupendana tukawa wapenzi.muda haukupita sana,huyo kijana akaanza nionesha his true colours akawa mhuni mno.ikaanza kiburi na kikubwa akawa anacheat hadi ikawa inafahamika chuoni sababu kila kukicha kulikuwa na story kuhusu yeye na msichana flani.nliumia na kukonda sana sababu nlimpenda mno kupitiliza.nlikuwa nakosa usingizi,nakesha nalia kwa maumivu na vituko haviishi.mara nimpigie anikatie simu na kuizima kabisa hadi kesho yake akijiskia kuiwasha kumbe anakuwa yuko na binti mwingine.nkitishia kumuacha,anajirudi kwa siku kadhaa kisha anaendelea na uhuni wake.mchezo ukawa huo,nalia baadae namsamehe.na kipindi chote hicho sikuwahi cheat ingawa nlitongozwa mno na mi ni mtu ninaejiheshimu.mazoea na wanaume sinaga.nlimvumilia kwa miaka mitatu,siku akafanya tena nkajiskia moyo umechoka kabisa mateso nkaamua enough is enough nka break up mazima. Mara ya kwanza nlivomuacha hakushtuka,akijua ntarudi tu kama zamani.siku zilivoanza kukatika,akajua I was serious ndo akaanza kutapatapa begging me back kwa kila namna na mara kibao alikuja kwangu na kukesha nje hadi asubuhi akiomba nimsamehe.mi nkiamka majirani ndo wananiuliza imekuwaje wamemuona mtu kashinda nje kwangu usiku kucha.by then nkakutana na kijana mwingine anaenipenda sana na kikubwa nlichompendea huyu kaka,haoneshi kabisa kuyumbishwa na wanawake.ni mtu ambae anaweza mtukana msichana mbele yangu anaetaka kuleta mazoea,jambo ambalo sikuliona kabisa kwa ex wangu.ex wangu mara zote alikuwa bize na simu,kutwa anaflirt na wasichana.sasa saivi its already a year na ex hajaacha kuniomba nimrudie.katumia kila njia,kawafuata ndugu zake,kaenda kanisani,kawafuata ndugu zangu,amekuwa akinunua zawadi za kila aina.anatumia kila mbinu na amekuwa akiwaeleza watu amenikosea anaomba wamsaidie kuniomba msamaha.mimi kila nkiwaza kurudi,moyo unasita nkikumbuka the sleepless nights na nlivotesekea mapenzi.na kikubwa nna mpenzi who really loves me...
Naombeni ushauri,sababu at this point naona inaniweka in a sort of dilemma.najikuta naogopa kuja kuumizwa tena na my boyfriend,what if nae atabadilika huko mbeleni na my ex is really sincere anatubu.au nikaja mrudia ex,kumbe ni usanii tu akaja niumiza na hali nimemuacha a good man away who seemed to truly love me.
....Naombeni ushauri na si matusi!...asanteni.
 
Reactions: amu
Neno nalo ushauri wangu. Usirudiane nae. Mpe ukweli mwambie sasa haumpendi tena na hauko tayari kuwa nae na HAUTAKUWA nae. Mwambie asipoteze muda na nguvu zake, wako wasichana wengi ambao wako tayari kuwa nae.

Kufanya hivi sio kwamba unalipa kisasi ila ni reality. Ila mwisho wa yote mwenye maamuzi wewe. Kumbuka usiendeshwe na hisia tu, pia endeshwa na reality. Story yako inafanana na mdogo wangu wa damu ambaye amefanyiwa hivyo hivyo na BF(ex) wake wakati wako chuo hapo UDSM. Huyo ex akija home siku nyingine namtoa ubongo!

Never HURT a woman when she loves you!!
 
Last edited by a moderator:
Ulishachukua maamuzi inatosha. Acha kutapa tapa utakuwa huna msimamo.
 
huyo wa sasa hivi kakukosea nini? Live the present, the past is gone and the future is highly uncertain!
 
Reactions: amu
Achan nae huyo..Mtu asiyekuheshmu na ana uwezo wa kukucheat mpak unajua ni mbay sana..Hapo anapretend tu..Mkirudiana na mkazoeana lazma arudie kamchezo kake.
 

tabia haina dawa shost
tulia na huyo wa sasa,usirudi nyuma kamwe!!
 
Usirudi nyuma dada yangu, utakuja kujuta maisha yako yote ukimrudia huyo ex wako,hana lolote. Ngoja nikwambie kitu kuhusu sisi wanaume huwa hatubadiliki hata siku moja;huyo ex wako ni kicheche na hakuheshimu wala hakupendi na ukweli utabaki hivyo milele bila kujali sasa hivi anakubembeleza kiasi gani umrudie. Ukijiroga tuu kurudi utajuta,and it will be too late. Kinachotokea sasa ni vile tuu amemiss the way u used to cry and beg for him;the way u used to worship him(if i may say so),ile yeye kuwa na authority ya kukunyanyasa na wewe kuwa helpless about it,na hiyo huwa unaweza kumfanyia msichana anaekupenda kiukweli kweli sana,na akakuvumilia,sasa tangu umuache hana tena mtu wa kumfanyia hivyo,he will say all the words and he will do anything to get that back,ila haimaanishi kwamba anakupenda. Once he get that chance again, utakiona cha mtema kuni. Umempata mtu anaekupenda move on dada. Ukifanya kosa na kumrudia huyo ex utakuja kulilia chooni.
Ngoja nikumegee siri nyingine kuhusu sisis wanaume dada yangu, ukiona mwanaume anakucheat mpaka anaonyesha waziwazi kuwa anakucheat, na hajali wala haonyeshi kujutia hata ukijua kuwa ancheat jua kuwa huyo mwanaume hajawahi kukupenda,hakupendi wala hatakuja kukupenda maisha yote ya duniani na ahera, that is a fact. Ni hayo tu.
 
mmh....kimbia, he wasn't good for you then, he won't be good for you now or later
 
Pole bidada usiyumbe ukisema No maanisha No kweli hata hivyo ulimvumilia sana.
 
USIWAZE KUMRUDIA,USIMPE NAFASI YA KUWA KARIBU MWISHO USITHUBUTU KUMSOGOLEA
na hiyo ni rasharasha ya mapenzi tuuu utaumizwa sana so injoi uliyekuwa nae ya kesho hujui nini kitatokea
 
Dating your ex is same as doing the same thing in exactly the same way and expecting different results. Which is a perfect definition of insanity
 
Duuh unampenda pressure wewe....miaka yote umekuwa nae hakukups respect sasa eti anaomba msamaha na wataka umrudia...holy ----!

Bado kumbe hujawajuwa wanaume. ...rudi ukalizwe tena
 
nyie wasichana wabaya sana kumbe unaweza mpenda binti baadaye akarudiana na x wake.

wasichana kama nyie ambao amna msimamo amtakiwi katika jamii na utachezewa sana.

ebu jieshimu fata maisha yako achana na uyo x wako. nyie ndio mnaowaletea watu ugonjwa. unajua uyo x wako katafuna wangap!

ungekuwa karibu ningekukata kofi. achana na uyo x asiye na future. vitu vingine viko wazi aviitaj ushauri.
 
Vyovyote utavyoamua sawa tu...yote ni maisha yako.
 
inaonekana huyo uliyenaye humpendi kwa dhati bado unawaza kurudi nyuma.......miaka mitatu ya mateso mara ushasahau unaomba ushauri wakumrudia
 
Beibii! Be strong enough to fight with majaribu! Kinachokusumbua wewe ni HURUMA c mapenzi tena yaani unamhurumia huyo ex wako anavyotapatapa! Ngja nkwambie ki2 kuna tabia zingine za binadamu huwa hazibadiliki hasa za umalaya! Kama ameshindwa kujirekebisha kwa hiyo miaka 3 basi huyo ni skio la kufa! Anapretend tu hapo! Then mama kama umeamua kusonga mbele kamwe usirudi nyuma! Labda nkuulize:how do u feel with your new bf? Are you real in love with him? Unamwonaje? Kama unampenda na anakupenda! Plz USIMPE NAFASI huyo ex wako mwambie ukweli kuwa its over maziima!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…