Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,734
- 215,917
Habari za leo,
Hii ni stroy niliyopewa na swahiba wangu, yaliyomtokea wiki iliyopita. Majina nitakayo tumia katika story hii ni ya kufikirika.
Travis ni mwanaume wa 35-40 ameoa ana watoto watatu, wote yeye na mke wake ni waajiriwa. Travis na mke wake wanamiliki nyumba maridadi katika mitaa iliyotulia, kutokana na sababu wanazozifahamu wenyewe, wameamua hawatakuwa na dada wa kazi, wana kijana wa kazi za ndani na mlinzi wa langoni.
Watoto wote wa Travis wako shule ya msingi, mipango ni kuwa watoto wakitoka shule jioni, bibi yao mzaa mama anawachukua kwa kuwa hakai mbali na shule, anakaa nao mpaka wazazi wao wanapokuja kuwachukua.
Familia ina gari moja, usiniulize kwanini, lakini mke wa Travis anawahi kutoka kazini, hivyo anapanda mabasi mpaka kwa mama yake, huko anakaa na watoto mpaka Travis anapokwenda kuwachukua, mara nyingi mama yao anafanya homework na watoto wakimsubiri baba.
Ofisini kwa kina Travis ameajiriwa dada wa miaka 24-26, anaitwa Veronica, binti huyu katika usaili alionekana uhodari wake uliowazidi wenzake, kwakweli katika jopo la kuchuja kila mtu alimpa binti huyu marks kuanzia 90-100%. Binti huyu alikulia Gaborone pamoja na kuwa ni mtoto wa ki-Tanzania.
Vijana wengi kazini walimpenda Veronica, wenyewe watoto wa ushuani wanasema alikuwa na class. Veronica bado anaishi kwa wazazi wake, mama yake ni wale ma aunt wa mjini wale wa handbag na wallet lazima vimatch. Mama anamdrop Veronica asubuhi na kumchukua jioni anapotoka kazini.
Siku moja wakiwa wamemaliza kazi, Travis alimuona Veronica anasimamisha tax, alimuwahi na kumuuliza yaliyojiri, bi mkubwa amepatwa na nini leo haji kukuchukua, Veronica alijibu kuwa mama yake mkubwa amepata dharura na hivyo mama yake amemwambia na yeye pia akitoka kazini aende kwa mama mkubwa watakutana huko, Travis alioffer kumpeleka Veronica kwa mama yake mkubwa.
Wakiwa kwenye gari, ndipo alipogundua kuwa mama yake mkubwa Veronica haishi mbali na anapoishi yeye Travis, alimwambia Vero kuwa kama hatajali kuna document za muhimu anazihitaji nyumbani kwake, walipoingia ndani, Travis alimwambia kijana wa ndani asafishe gari, yeye aliingia ndani na mgeni.
Alimkaribisha na kumwambia kwa kuwa wanafanya kazi ofisi moja, si vibaya ampe tour ya nyumba anaoishi, cha ajabu tour hii ilianzia na kuishia kwenye en suite ambayo inatumika kama chumba cha wageni.
Mke wa Travis siku hiyo kichwa kilikuwa kinamuuma, aliamua kumpigia simu mume wake ili akawachukue mapema, simu zaidi ya kumi ziliingia kwenye voice mail, mwisho mama wa watu aliamua kuchukua tax.
Travis aliniambia wakati Veronica akiwa anaoga bafuni ndiyo anasikia sauti za watoto wake wakishindana kupanda ngazi "you can't catch me". Kushtuka ilikuwa takribani saa mbili usiku.
Nikieleza baada ya hapa kilichotokea nitakuwa ninatunga, kwani kwa maneno ya Travis yaliishia hapa aliitwa, story iliingiliwa.