Story ya mapenzi: Karibu Uani

Story ya mapenzi: Karibu Uani

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
521
*STORY*: KARIBU UANI
*MTUNZI*: JK
0718274130

*SEHEMU YA KWANZA*
**************
Saa 12 asubuhi, tayari nilikua njiani kama kawaida yangu. Nilikua katika pikipiki yangu ambayo mara zote ndio huwa naitumia katika safari zangu zote, ikiwemo hii ya kazini. Kwakuwa nilikua mbali na mjini, ilinilazimu kutoka mapema saa 12 kasoro kila asubuhi, ili niweze kuwahi kazini vizuri. Ningeweza pia kutoka hata saa 1 kasoro na nikawahi mapema, lakini sikupenda kuendesha mwendo wa kasi sana kwa jinsi pikipiki yenyewe ilivyokuwa. Ilikua haina uzima wa kuaminika.

Nikiwa naendesha mwendo wangu mdogomdogo, huku nikiwa nimevaa begi langu la mgongoni, masikioni nikiwa na 'earphone' zinazotoa mziki laini kutoka katika simu iliyokuwa katika suruali yangu, nilipitiwa ghafla sana na gari iliyokuwa ikienda kasi mno katika njia hii ya vumbi. Vumbi lote likajaa usoni kwangu na kufanya niyafumbe macho yangu ghafla...

Pikipiki ikakosa muelekeo na kunifanya nijikute nimeingia pembeni mwa barabara. Nikiwa bado sijafumbua macho yangu,nikijaribu kupunguza gia nifunge breki kisha nisimame.. Nilisikia sauti kali ya kike ikipaza sauti "Mamaaa nakufaaa".

Nikalazimika kufunga breki ghafla na kufumbua macho, sijaamini nilichokiona mbele yangu.

************************

Naitwa Kidunya Jumaa, mwenyeji wa Jiji la Tanga ninayefanyia shughuli zangu hapahapa Tanga. Kama wanavyosema mcheza kwao hutunzwa, nami najaribu kuisadifu hii kauli kwa vitendo..

Baada tu ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu pale mkoani Arusha, sikuona sababu ya kujipoteza mbali na nyumbani.

Nilirudi nyumbani na kuamua kuwekeza katika kilimo kupitia moja ya mashamba aliyotuachia baba yetu aliyefariki dunia miaka sita iliyopita.
Nikaanza kujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji, kwa muda wa miaka zaidi ya miwili.

Rafiki zangu kadhaa ambao walishakua na nafasi mbalimbali katika taasisi mbali mbali za binafsi na serikali, ambao wanafahamu vizuri uwezo wangu, wakaanza kunishawishi nijaribu kuomba kazi katika taasisi hizo. Mimi binafsi sikuwaza kuhusu kuajiriwa, lakini wao walitaka niendelee kufanya shughuli zangu lakini pia niwe nafanya kazi za kuajiriwa.

Kwa msaada wao nikafanikiwa kupata kazi katika moja ya ofisi za serikali. Lakini niliendelea kuishi mbali na mji kwa sababu ya mifugo yangu pamoja na kilimo ambacho nilikuwa naendelea nacho.

Ilinilazimu kila asubuhi kutumia usafiri wa pikipiki ambyo niliinunua mwaka mmoja tu baada ya kuanza shughuli za kilimo. Kila siku nilitoka nyumbani mapema sana ili niwahi kazini. Na mnamo saa tisa alasiri niliwahi kurudi nyumbani haraka ili shughuli zangu za kilimo nisiziache nyuma.

********************************
Akili yangu moja kwa moja ilinituma kuwa tayari nitakuwa nimegonga mtu, kutokana na kelele ile ambayo niliisikia..

Nikasogea pale alipokuwa amelala yule dada pembeni mwa barabara. Nilishindwa kuitambua sura yake kwani alikuwa amevalia baibui huku akiwa na 'niqab' au 'ninja' kama wengi walivyoitambua..

Alikua pale chini akiugulia maumivu huku akishikilia sana sehemu ya ubavu wake wa kushoto.

"Nisaidiee..., naumiaaa, nisaidiiieeee....." Ndiyo sauti aliyokuwa akitoa dada yule ambaye mpaka muda huu nilikuwa na uhakika kuwa mimi ndiye niliyemgonga na pikipiki yangu.

"Pole sana dadaa, pole sana... Nakusaidia na utakua poa usijali" Nilijaribu kumfariji huku nikishika mkono wake wa kulia kujaribu kumnyanyua.

"Mamaaaa... Naumia hukoooo..." Alipiga kelele akiashiria anapata maumivu makali sana katika mkono wake wa kulia nilioshika, kitendo kilichofanya niuachie haraka sana..

Nilifikiria njia ya haraka ya kumsaidia, nikaamua nianze kusimamisha magari yanayopita kuelekea mjini ili nipate angalau msamaria mwema atakayeweza kuniwahishia huyu dada hospitali.

Nilijaribu kupunga mkono kwa magari zaidi ya matatu bila mafanikio, kila mmoja alinipita bila kujali nini kinaendelea pale.

Nikapata wazo la kuwapigia simu ofisini kwa madhumuni mawili; kwanza, kuwaeleza juu ya mkasa huu ulionikuta, ambao nilikua na uhakika kuwa utanichelewesha kazini kama si kunifanya nisifike kabisa.

Pili, kuwaomba kama wanaweza kutoa gari ya ofisi ije inipe 'msaada kwenye tuta' ambao ulishanipa wakati mgumu.

Nikapiga simu ya Mkurugenzi Mtendaji, lakini haikupokelewa... Nikajaribu kupiga ya msaidizi wake, haikupatikana kabisa..

Nikajaribu simu ya rafiki yangu Zuber ambaye nilisoma nae chuo kikuu ninayefanya nae kazi ofisi moja, simu yake iliita mwisho ikakatwa. Kisha nikaona ujumbe ukiingia "Am driving".

Niliishiwa pozi.. Nikajikuta nimeshika kiuno nikiwa sijui cha kufanya, na sauti ya yule dada pale chini akigumia ilizidi kunipa wakati mgumu.

Ghafla nikasikia honi kali ya gari nyuma yangu.. Nikageuka na kukutana na mdomo wa konda wa daladala inayotokea Pangani kuelekea mjini ukiniambia "Wacha ujinga braza utakufa weweee.. Unasimama katikati ya barabara kama chumbani kwako banaa..."

Kwakweli nilibaki nimeduwaa hata sikuwa na cha kujibu, kumbe nilikua katikati ya barabara... Sina habari.

Abiria wengi waliokuwa kwenye daladala ile wakachungulia, wengine walinisikitikia, wengine wenye akili kama za huyu konda walitoa matusi mazito. Ila mama mmoja alibahatika kumuona yule dada aliyelala pale chini akiugulia maumivu, akashawishi gari isimamishwe ili lijulikane tatizo niweze kupatiwa msaada. Kweli gari ilisimama, na abiria wengi wakaja kushuhudia kinachoendelea.

"Ulimgonga huyu dada?" Aliniuliza dereva wa ile gari.
"Nahisi hivyo, maana hata sijui kilichotokea.." Nilijibu swali lile nikiwa namuangalia yule dada..

"Hujui kilichotokea? Kivipi? Hebu tueleze kwa undani" Aliendelea kunitwanga maswali yule dereva.

"Jamaani, hebu tumsaidieni kwnza huyu aliye hapa chini, hayo mengine tutayajadili baadae, mwenzetu atakufa huyu.. Ohooo.. Leo kwake kesho kwako". Alisema dada mmoja aliyekuwa amevalia dera lake la pink lenye maua mekundu, juu alikuwa na mtandio mdogo uliotosha kufunika kichwa na shingo yake na kushuka hadi kwenye mabega.

Konda wa ile gari alikuwa hajasogea kabisa pale, abiria wote wakashirikiana kumbeba na kumpeleka katika gari ile aina ya 'hiace'..

Walipofika mlango wa kuingilia katika gari, konda aliyekua hapo mlangoni muda wote huo akatupia jicho lake kwa yule dada ambaye muda huu walikua wameshamvua niqab yake na mimi nikapata kuona sura yake.

Ilikua sura nzuri, nyembamba, ilyopambwa na pua ndefu iliyonyooka kama ya Kinyarwanda.. Alikuwa na lips zilizojaa vizuri. Kiufupi alikua anaweza kumvutia kila mwanamme anayeweza kumtazama. Wasiwasi wangu pia ni kuwa wanawake wenzio walitamani wapewe sura kama ile angalau kwa dakika sita tu.

"Haaaa... Hapana.. Hapana, kumbe ni huyu mal'uuni....??!!! Hapana, huyu haingii humu.. Huyu hapandi kwenye gari yangu hata siku moja, niko radhi niwaache abiria wote hapahapa lakini sio kubeba afiriti huyu.. Hata siku moja" Konda aliongea maneno haya kwa sauti ya juu na ya ukali, na kufanya abiria wote wapigwe na butwaa.

★★★★★★★★★★★★★★

Usikose *SEHEMU YA PILI*

Kwa story hii na nyengine nyingi..
Nitafute Whatsapp.. +255718274130
 
*STORY*: KARIBU UANI
*MTUNZI*: JK
0718274130

*SEHEMU YA PILI*
**************
Nikapigwa na butwaa baada ya kuona jinsi yule konda alivyokomalia yule dada asiingie mle kwenye ile gari. Abiria wengine wote pamoja na dereva pia waliungana na mimi katika kushangaa.

Kila mmoja akiwa anajiuliza swali lake kichwani.

Mmoja kati ya wale abiria ambaye alionekana kuguswa sana na jambo la yule dada, alianza kubishana na yule konda.. Kijana yule wa miraba minne, aliyevalia t-shirt nyeusi alionekana kutofurahishwa hata kidogo na kitendo kile cha konda. Misuli ya kifua chake ilionekana vizuri akiwa na 'six packs' za maana.
"Tuachie ujinga wewee... Sisi tushindwe kumsaidia mtu kwa ujinga wako, pumbaavuuu.." Alisema yule kijana ambaye baadae nilitambua kuwa anaitwa Thomas. Alimsukuma pembeni yule konda, na akaruhusu waliombeba yule dada kupita nae hadi ndani ya gari.

Wanawake wawili wakajitolea kumpakata katika mapaja yao huku dereva ambaye alionekana kuguswa sana na tukio lile, akipanda na kuwasha gari tayari kwa kuondoka.

Hapa nilipata wakati mgumu sana, nilifikiria ile pikipiki nitaibebaje, au ntamwachia nani..??!! Na ilikua lazima mimi niende hospitali, maana haswa mimi ndiye mwenye mgonjwa wangu. Nikawaza na kuwazua harakaharaka wakati abiria wengine wakiendelea kupanda katika gari tayari kwa kuondoka..
Nikiwa katika dimbwi hili la mawazo, simu yangu ikaanza kuita, alikuwa Zuber..
"Haloo kaka vipi, nilikua naendesha, ndio nimefika ofisini saa hii..."

"Kaka majanga, nimegonga mtu, wewe kama vipi njoo na hii njia ya Pangani nyooka tu moja kwa moja, nataka uje uibebe hii pikipiki yangu mimi naongozana na wasamaria wema kumpeleka huyu dada hospitali..." Niliongea moja kwa moja bila nukta.

"Sawa kaka, dakika sifuri" Zuber naye alijibu bila kuuliza swali lolote.

★★★★★★★★★★★★★★

Moja kati ya vitu ambavyo vinanisumbua siku nyingi sana ni hili jambo la mapenzi. Yaani tangu hapo nilipoanza kufanya mapenzi, siku yoyote ambayo nitajamiiana na mwanamke, basi yanayofuata ni majanga mfululizo ndani ya siku mbili.

Zamani nilikuwa sijagundua, lakini baadae nikachunguza na kuona kuwa kuna kitu kinaendelea kwangu mimi..

Kabla babu yangu hajafa miaka saba nyuma, niliwahi kumuelezea hali hii. Yeye alinieleza kuwa inawezekana ni moja kati ya vitu viwili, aidha niliwahi kufanya mapenzi na jini bila kujua, ama ninalo jini ambalo halipendi nifanye mapenzi ovyo (ngono zembe).

Babu hakuishia hapo, alinipatia baadhi ya dawa ambazo nilitumia kwa muda, hali ile ilipungua, japo kwa kiasi kidogo.. Kabla sijampa 'feedback' babu akawa ametangulia mbele za haki.

Kwa kipindi chote hicho sikumweleza mtu mwingine yeyote..lakini bado nilisumbuka.

Sasa hii ya jana ilikuwa kali zaidi, kwani wakati narudi zangu nyumbani nikitokea kazini, njiani nilimpa 'lift' dada mmoja mrembo wa wastani. Aliniuliza naishia wapi..nikamwmbia 'Mtakuja' akasema kuwa yeye nitamwamcha hapo halafu atakata kulia kuelekea nyumba za hapo karibu ni kwa dada yake.

Wakati niko nae barabarani nikiendesha mdogo mdogo kama kawaida yangu, nilipiga nae story mbili tatu, ndipo nikagundua kuwa amefukuzwa nyumbani alipokuwa anakaa na bwana wake aliyeishi nae kinyumba kwa mwaka mzima sasa..

Hili liliashiria kuwa dadaake hana taarifa na ugeni huu.. Ndipo nikapata mwanya wa kumshawishi aungane na mimi jioni ile pamoja na usiku wake kwani mimi niko 'alone'.

Akanikubalia na tukaenda nyumbani. Nilikuwa na usiku mzuri sana, maana nilipikiwa, nikala chakula kizuri, na nikapata kupiga story mbili tatu kwani upweke ulikuwa ukiniandama sana..

Nilikaa nae sebuleni kwa muda tukipeana story mbili tatu huku muda mwingi akitumia kunieleza maswahibu yake na aliyekua mumewe.
Nilimuonea huruma ingawa alionekana kufarijika sana.

Mpaka ilipofika saa tano za usiku tulipokubaliana twende kulala.

Mimi nikaamua niingie bafuni kwanza kuoga. Nikavua suruali yangu na kubaki na bukta na kuchukua taulo kujifunga kiunoni. Wakati huu dada huyu mrembo aliyenambia anaitwa Subira alikuwa amekaa kitandani akifanya 'subira' mimi nikaoge kwanza.

Nilimuona akiniangalia kwa jicho la kuiba, labda kwa kufikiria kitakachoendelea baada ya pale..
Mimi nikatokomea bafuni kwa kujifanya simuoni..!!

Nilitumia dakika kadhaa kisha nikatoka bafuni, swali la kwanza nililomuliza baada ya kutazamana..
"Utaenda kuoga amaa..?"

"Yeah, ila ntabadilishia wapi nguo jamanii...?" Alijibu na kuuliza swali kwa pamoja.

"Hapahapa.. Kwani mi nimebadilishia wapi..?" Nilimjibu nikiweka pembeni sura ya utani.

"Mmmh, mi nasikia aibu hapa bana..wewe sijakuzoea.." Alideka..
"Usijali, nafumba macho" Nilitania.

Akachomoka pale kitandani, na kuanza kusaula.. Hapa ndipo nilihisi damu ikienda kasi kuliko kawaida..

Nikajaribu kujikaza nisiangalie kilichopo mbele yangu, ila macho yalinizidi nguvu.. Nikajikuta nimekodoa..Tofauti na nilivyotegemea.., alisaula hadi akabaki na kufuli tu.. Kisha akanigeukia na kuniuliza..

"Kuna kanga humu ndani?" Mimi nilibaki nimekodoa tu, 'network error!!'
★★★★★★★★★★★★★★
Usikose sehemu ya Tatu.

Umeipenda hii?! Zipo nyingine ..

Call/sms/whatsapp..
+255718274130
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom